Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (wa pili kushoto) akimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara ya Saudi Arabia Dk. Abdulrahman Al-Zamil (wa tatu kushoto) jijini Riyadh, Saudi Arabia. Wengine katika picha kutoka kulia ni Mshauri wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Mamlaka ya Wanyamapori ya Saudia Mohammad Sulayem; Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii Dk. Adelhelm Meru na Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Prof. Abdillah Omari.
Twitter Buzz
....
...
IMETOSHA!
Featured post
KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO
Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...
Thursday, 15 January 2015
WEAR SWAHILI DESIGN BY MARIAM IKOA @ DAR FREE MARKET
Some men shirts and ladies outfit in her own design. The design collection is called WEAR SWAHILI. Her main goal is to promote our own fabric in a modern way and comfortable way. Any age can wear and still look stylish at an effective cost price.
TANGO KUWA NA MKUTANO WA HADHARA MNAZI MMOJA LEO KUJADILI MALENGO YA SDGS
Meneja wa sera na ushirikishaji wa TANGO, Zaa Twalangeti, akizungumza na Modewjiblog kwenye mahojiano maalum yaliyofanyika katika ofisi za TANGO jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mratibu wa kitaifa wa Mtandao wa Asasi zisizo za kiserikali za haki za binadamu kusini mwa Afrika(SAHRINGON), Bi. Martina Kabisama.
RAMBIRAMBI MSIBA WA STEPHEN NSOLO
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko taarifa ya msiba wa Katibu Mkuu wa zamani wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Shinyanga (SHIREFA), Stephen Nsolo (pichani juu) uliotokea Januari 13, mwaka huu jijini Mwanza.
KOCHA NOOIJ KUTAJA STARS MABORESHO
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij anatarajia kutaja kikosi cha Maboresho kitakachoingia kambini Januari 18 mwaka huu kujiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Rwanda itakayofanyika Januari 22 mwaka huu jijini Mwanza.
RAUNDI YA PILI TAIFA CUP WANAWAKE JUMAMOSI
Mechi za kwanza za raundi ya pili ya mashindano ya Taifa ya mpira wa miguu kwa wanawake (Taifa Cup Wanawake) zinachezwa wikiendi hii (Januari 17 mwaka huu) kwenye miji minane tofauti nchini.
POLISI MARA YAZUIWA KUCHEZA UWANJA WA KARUME MUSOMA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeizuia timu ya Polisi Mara kutumia Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma kwa mechi zake za Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kuanzia leo mpaka hapo itakapotangazwa vinginevyo.
SERIKALI YAUNDA TIMU KUTEMBELEA MAENEO SUGU YA UTEKAJI, UUAJI ALBINO, YAPIGA MARUFUKU WAPIGA RAMLI NCHINI
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (katikati meza-kuu) akizungumza na
waandishi wa habari kuhusiana na Serikali kuunda timu maalumu ya kutembelea
maeneo yaliyosugu kwa utekaji na mauaji ya albino nchini ambapo timu hiyo
inatarajiwa kuanza kazi wiki mbili zijazo kwa kuanza na mikoa sugu ya matukio
hayo ambayo ni Mwanza, Geita, Simiyu, Tabora na Shinyanga na baadaye itafuata
mikoa mingine. Pia Waziri Chikawe katika mkutano huo, alitangaza kupiga
marufuku wapiga ramli wote nchini kwa kuwa wanasababisha kuendelea kwa matukio
ya kinyama wanayotendewa albino. Hata hivyo, katika mapambano ya kusambaratisha
unyanyasaji huo, waziri huyo alitangaza kushirikiana ipasavyo na viongozi wa
dini pamoja na mashirika ya kijamii ili kusaidia kutoa elimu kwa wananchi kutokana
na uhalifu huo dhidi ya albino. Kulia meza kuu ni Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini, IGP Ernest Mangu na kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Albino nchini
(TAS), Ernest Kimaya. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa
wizara hiyo, jijini Dar es Salaam juzi.
HUDUMA ZA UMMA HAKUNA TEMEKE, KISA MSIBA!
Tangazo katika Ofisi za Idara ya Elimu (Msingi) katika Manispaa ya Temeke kuonyesha kwamba hakuna huduma zozote kwa sababu ya msiba.
Msiba wa mmoja wa wafanyakazi wa Idara ya Elimu Msingi katika Manispaa ya Temeke umesababisha kusimamishwa kwa huduma zote za umma na kufungwa kwa ofisi leo hii.
Tuesday, 13 January 2015
HIKI NDICHO KIKOSI BORA CHA DUNIA
Shirikisho la soka dunia Fifa limetangaza kikosi cha wachezaji bora wa dunia.
MISHAHARA YA WABUNGE VURUGU BURKINA FASO
Wastani wa mshahara nchini Burkina faso ni takriban dola 150 kwa mwezi, kwa mujibu wa Mbunge kutoka baraza la mpito nchini humo, mishahara inahusisha malipo ya vikao vya bunge, malipo ya shughuli za ofisi, malipo kwa ajili ya huduma za afya na gharama za mafuta.
PAPA FRANCIS ZIARANI SRI LANKA
Papa Francis amewasili nchini Sri Lanka ambako anatarajiwa kusisitiza umhimu wa mazungumzo baina ya makundi mbalimbali ya imani hasimu za kidini nchini humo.
KATUNI YA MTUME MOHAMMAD KUCHAPISHWA
Gazeti la Vibonzo la Charlie Hebdo
Gazeti la kila wiki la vibonzo la Charlie Hebdo la ufaransa toleo la kesho jumatano litarajiwa kuchapisha kibonzo cha Mtume Mohamed katika ukurasa wake wa mbele chini ya kichwa cha habari "Yote yameshasamehewa".
MH. CATHERINE MAGIGE AZINDUA DUKA JIPYA LA UREMBO LA ZuRii LILILOPO DAR FREE MARKET
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Catherine Magige (kushoto) akiwasili kuzindua rasmi duka la urembo la ZuRii House of Beauty linalomilikiwa na mwana Diaspora ambaye pia ni mwanalibeneke Jestina George Meru (kulia) ndani ya jengo la Dar Free Market jijini Dar es Salaam jana.
UKOSEFU WA KAZI KWA VIJANA NI JANGA LA DUNIA
Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari (UTPC), Abubakar Karsan akionyesha gazeti la "Tuwasiliane" linalochapishwa na UTPC na kusambazwa kwa wadau na maeneo mbalimbali ya jijini Mwanza kwa Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez aliyetembelea makao ya ofisi hizo kwa ajili ya mazungumzo na kuboresha ushirikiano baina ya Umoja wa Mataifa Umoja huo wa vilabu vya waandishi wa habari nchini.
COASTAL UNION YAITUMIA SALAMU YANGA
NA MWANDISHI WETU, TANGA
TIMU ya soka Coastal Union ya Tanga imeitumia salama timu ya Yanga kuwa isitarajie itaweza kuchukua pointi tatu kirahisi kwenye mechi yao itakayochezwa Jumatano wiki hii ya Ligi kuu kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani badala yake ijiande kwa kipigo kutokana na maandalizi walioyafanya kuelekea mchezo huo.
MAKATIBU TAWI NA KATA WA CCM WAMSUSA RAGE
Mbunge wa Tabora Mjini, Ismail Aden Rage
Na Mwandishi Wetu, Tabora
VIONGOZI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Matawi na Kata za Misha na Kabila wamerudisha baiskeli zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Tabora Mjini, Ismail Aden Rage kutokana na madai ya maneno waliyodai ni kashfa kwao na kuona kama wamedhalilishwa na mbunge wao.
MVUA ZA MASIKA ZALETA MAAFA NZEGA
Na Hastin Liumba, NzegaWATU watatu katika matukio mawili tofauti wamefariki dunia katika Kijiji cha Ugembe wilayani Nzega mkoani Tabora kutokana na mvua za masika zinazoendelea kunyesha.
MSIWATAFUTE VIONGOZI WA SERIKALI WAKATI MNA SHIDA NA HARAMBEE - MCHUNGAJI
Na Mwandishi Wetu, Arusha
IMEELEZWA kuwa tabia ya baadhi ya taasisi za dini kuwakwepa viongozi wa dini na kisha kuwatafuta wakati wakiwa na uhitaji ni chanzo mojawapo cha kusababisha hata hekima ndani ya uongozi wao kuweza kupungua kwa kiwango kikubwa.
WAZEE WALIA NA HALI NGUMU YA MAISHA, WAOMBA SERIKALI NA WAHISANI KUWANUSURU
Na Mwandishi Wetu, Arumeru
WAZEE Wilaya ya Meru wameomba ,Serikali na wahisani kuwasaidia kukabiliana na hali ngumu ya maisha inayokabili ikiwa inachangiwa na mabadiliko ya tabia nchi ,ambapo wamelazimika kuacha shughuli za kilimo walizokuwa wanazitegemea.
CCM LINDI YAKUTANA KUWEKA MIKAKATI MIZURI
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Ndugu Nape Nnauye akitoa salaam za pongezi kwa wananchi wa kijiji cha Kilangala B kata ya Kilangala kwa kuipa ushindi CCM kwenye uchaguzi serikaliza mitaa uliofanyika desemba 2014, Katika mkutano huo Nape aliwaeleza wananchi hao CCM ndio chama pekee kinachotoa majibu kwa matatizo ya wananchi.
COASTAL YAANZA KUANDAA SILAHA ZA KUIANGAMIZA POLISI MORO
Kikosi cha Coastal Union kilichocheza mechi ya kirafiki na Mombasa Kombaini na kutoka sare ya kufungana bao 1-1,Mkwakwani.
WAONYWA KUTOINGIZA SIASA KWENYE MIRADI
Na Hastin Liumba, IgungaSERIKALI Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora imeonya na kuwawataka wana siasa kuondoa tofauti zao za kisiasa katika kutekeleza na kusimamia mfuko wa Tasaf awamu ya Tatu.
WAKULIMA BINAFSI WA TUMBAKU WAONYWA
Na Hastin Liumba,TaboraCHAMA kikuu cha wakulima wa zao la tumbaku kanda ya magharibi (WETCU) kimefanya mkutano wa uchaguzi wa wajumbe wa bodi ambapo Mkandala Gabriel Mkandala amechaguliwa kuwa mwenekiti mpya kwa kura 401.
KARIBU ZURII HOUSE OF BEAUTY DUKA JIPYA NA LA KISASA LA VIPODOZI
SHEIN ATIBUA NDOTO ZA LOWASSA, MEMBE
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein
Na Mwandishi
Wetu
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kinadaiwa kuwa na
mpango wa kumsimamisha Dk. Ali Mohammed Shein kuwania urais wa Muungano katika
uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Hatua hiyo itatibua ndoto za urais za Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, pamoja na Waziri
Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, ambao kambi zao zinatajwa kuwa na nguvu ndani ya
chama hicho.
Friday, 9 January 2015
KAMATI KUU YA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CCM KUKUTANA ZANZIBAR JANUARI 13, 2015
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) itakutana Zanzibar Januari 13, kwa kikao cha kawaida cha siku moja chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
TAMKO LA JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAM TANZANIA
Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu
JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAM (T)
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
17 Mfungo Sita 1436
9 Januari 2015
TAMKO LA JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAM TANZANIA KUPITIA VYOMBO VYA HABARI KWA WATANZANIA WOTE, JUU YA MUSWADA WA MAREKEBISHO YA SHERIA MBALIMBALI NA. 02, WA MWAKA 2014, HUSUSAN KUHUSU SEHEMU YA MAREKEBISHO KWENYE SHERIA YA TAMKO LA SHERIA ZA KIISLAM
Awali ya yote tunapenda kutumia fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu Muumba wa Mbingu, Ardhi na vilivyomo, na Rehma na Amani zimfikie Kiongozi wa Ummah Mtume Muhammad (SAW).
WHATSAPP YAVUNJA REKODI YA 'UJUMBE'
Kila siku zaidi ujumbe billioni 30 wa mtandao wa WhatsApp hutumwa kulingana na takwimu mpya zilizotolewa na afisa mkuu wa mtandao huo Jan Koum.
MAGARI YEYE PICHA ZA RAIS YAKAMATWA
Licha ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kuruhusu magari yanayobeba abiria nchini Kenya kuchorwa ama hata kupaka rangi yoyote ile, mabasi mawili yaliochorwa picha yake yamekamatwa na maafisa wa polisi mjini Mombasa, Kenya.
MWANABLOGU ACHAPWA VIBOKO HADHARANI
Mwanablogu nchini Saudia amechapwa viboko hadharani kwa madai ya kutusi dini ya Kiislamu.
PUNDA WATUZWA KWA UMINIFU
Wanyama walipatiwa tuzo mjini Bangalore na Mwanasiasa Vatal Nagaraj, Kiongozi wa chama kimoja mjini humo. Mtandao wa NDTV umeripoti.
UN YAKEMEA MSHAMBULIZI YA ALBINO
Umoja wa Mataifa umekemea wimbi la mashambulizi dhidi ya Watu wenye ulemavu wa ngozi, Albino, baada ya tukio la kutekwa kwa mtoto wa miaka minne mjini Mwanza, kaskazini magharibi mwa Tanzania.
TAHARUKI UFARANSA WATU ZAIDI WAKITEKWA
Eneo ambalo washukiwa wa Charlie Hebdo wamezingirwa nchini Ufaransa
Huku maafisa wa polisi wakiwazingira washukiwa wawili wa ugaidi , kuna taarifa mpya kwamba Mwanamume tofauti aliyejihami kwa bunduki, amewateka nyara watu ndani ya duka mjini Paris.
UN YATAKA KIPAUMBELE KUMSAKA BINTI MWENYE ALBINISM ALIYETEKWA
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akimtambulisha Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (katikati) alipoitishia mkutano na waandishi wa habari jijini Mwanza mara baada kuhitimisha ziara zake Kanda ya ziwa. Kushoto ni Mshauri wa masuala ya haki za binadamu kutoka ofisi ya mratibu mkazi wa UN Tanzania, Bi. Chitralekha Massey.
KILUVYA UTD, NJOMBE BADO ZAKIMBIZA SDL

Kiluvya United ya Pwani na Njombe Mji ya mkoani Njombe ndizo timu pekee zilizomaliza mzunguko wa kwanza wa Ligi Daraja la Pili (SDL) kwa kushinda mechi zote katika makundi yao, hivyo kujipatia pointi 15 kila moja.
TAIFA CUP WANAWAKE KUPIGWA JUMAMOSI
Mechi za kwanza za raundi ya kwanza za mashindano ya Taifa ya mpira wa miguu kwa wanawake (Taifa Cup Wanawake) zinachezwa kesho (Januari 10 mwaka huu) kwenye miji 11 tofauti nchini.
STARS MABORESHO, RWANDA KUCHEZA MWANZA JAN 22

Kikosi cha Taifa Stars Maboresho kitacheza mechi ya kirafiki na timu ya Taifa ya Rwanda itakayofanyika Januari 22 mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
COASTAL UNIONI KUKIPIGA NA MOMBASA COMBAIN KESHO
NA MWANDISHI WETU,TANGATIMU ya Coastal Union “Wagosi wa Kaya” kesho wanatarajia kucheza mechi ya kirafiki na timu ya Mombasa Combain ikiwa ni kukipa makali kikosi hicho kabla ya kucheza mechi zake zinazofuata za Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara.
WAOMBA KITUO MAALUMU CHA WATOTO WALEMAVU BUHANGIJA KUSAIDIWA ZAHANATI
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Bi. Anne Rose Nyamubi mara baada ya kuwasili ofisini kwake kwa ajili ya mazungumzo kabla ya kuelekea kwenye kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum wakiwemo walemavu wa ngozi cha Buhangija Jumuishi kilichopo mkoani Shinyanga.
COASTAL UNION YAANZA KUITAFUTIA DAWA POLISI MOROGORO
NA OSCAR ASSENGA, TANGA
TIMU ya Coastal Union “Wagosi wa Kaya”imeanza maandalizi kabambe kujiandaa na mechi yake ya Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara dhidi yao na Polisi Morogoro itakayo chezwa Jumamosi wiki.
TEMBO ZAIDI 20 WAUA SIKONGE

Na Hastin Liumba, SikongeZAIDI ya Tembo 20 wamevamia makazi ya watu na wilayani Sikonge mkoani Tabora na kuharibu mazao, kujeruhi na kuua mtu mmoja.
SERIKALI YAOMBWA KUWAJALI WAHUDUMU WA MAJUMBANI WENYE VVU
Serikali imeombwa kuwajali na kuwapa kipaumbele wahudumu wa nyumbani wa waathirika wa Virusi vya Ukimwi VVU, kwani wamekuwa wakijitolea kwa moyo mmoja kuwasaidia wagonjwa lakini wamekuwa hawawezeshwi.
TFDA YATEKETEZA VIPODOZI
MAMLAKA ya chakula na dawa TFDA, kanda ya kaskazini imeteketeza vyakula, vipodozi na dawa zenye thamani ya shilingi 8,825,500, vyenye uzito wa kilogram 167.
Wednesday, 7 January 2015
CCM YATABIRI NDOA YA UKAWA
Na Mwandishi Wetu, MERUCHAMA cha Mapinduzi kimesema kuwa Umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA)utaisha mwakani mwezi February kwa kuwa baadhi ya viongozi wa umoja huo wengi wao wana matarajio ya kuwania nafasi ya urais.
KITUO CHA HUDUMA YA MTOTO TAG BETHEL CHRISTIAN CENTER CHAFANIKIWA KUTOA HUDUMA ZA MSINGI KWA WATOTO 270 WANAOTOKEA MAZINGIRA MAGUMU
WATOTO 270 waliotokea katika mazingira magumu na familia masikini wanaolelewa na kituo cha huduma ya mtoto Bethel student center TZ -100 wamefanikiwa kupata ufadhili wa huduma za elimu,kimwili,kiroho ,kijamii na kiuchumi hali ambayo imewafanya kujikomboa katika hali ngumu ya maisha.
SERIKALI YATAKIWA KUKOMESHA UBABE KWENYE UKEKETAJI
Mratibu wa kituo cha TFGM na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Mtakatifu Catherine Laboure ya Kijiji cha Masanga kilichopo wilayani Tarime mkoani Mara, Thomas Maruga akiwatembeza maeneo mbalimbali ya shule hiyo na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA), Dkt. Natalia Kanem (kushoto) wakati wa sherehe ya mahafali ya sita ya mabinti waliokwepeshwa msimu wa ukeketaji (Waiseke wa Kisasa).
KITUO YATIMA CHASAIDIWA MAGODORO
Na Hastin Liumba, Igunga
KITUO cha kulelea watoto yatima na walio katika mazingira magumu cha Charity and Orphanage Organization (CAO) cha wilayani Igunga mkoani Tabora kimekabidhiwa msaada wa magodoro matano yenye thamani ya sh.275,000.
UWT UYUI WAASWA
Na Hastin Liumba,Uyui
JUMUIYA ya Umoja wa akinamama wa (UWT) wilaya ya Uyui mkoani Tabora, wamepongezwa kwa kujitokeza kugombea katika nafasi chaguzi za Serikali za mitaa vitongoji na Vijiji kwa kupata ushindi.
JUMUIYA ya Umoja wa akinamama wa (UWT) wilaya ya Uyui mkoani Tabora, wamepongezwa kwa kujitokeza kugombea katika nafasi chaguzi za Serikali za mitaa vitongoji na Vijiji kwa kupata ushindi.
WANANCHI WACHOMA NYUMBA TANO ZA MTUHUMIWA JAMBAZI SUGU
Na Hastin Liumba,Igunga
WANANCHI wa kata ya Igurubi wilayani Igunga mkoani Tabora, wameyakimbia makazi yao kwa ajili ya kukwepa kukamatwa na jeshi la polisi baada ya kutuhumiwa kuchoma nyumba tano za mtu anayedhaniwa kuwa ni jambazi.
REDIO YA JAMII MKOANI YAZINDULIWA KWA MBWEMBWE ZA MAPINDUZI
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (mwenye koti la suti) akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Pemba kwa ajili kuhuduria sherehe za uzinduzi wa Redio Jamii Mkoani jimbo la Mkanyageni, Kusini Pemba na kupokelewa na Afisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) Bw. Al Amin Yusuph (kulia) aliyeambatana na Mshauri na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu (aliyeongoza mbele).
Subscribe to:
Posts (Atom)





