Social Media Administrator wa MultiChoice (DStv) Tanzania, Shumbana Walwa akiwa katika pozi wakati wa hafla hiyo ya siku ya Afrika ambapo wadau mbalimbali walijumuika kwa pamoja kusheherekea siku hiyo iliyofanyika usiku wa Mei 27. Jijini Dar es Salaam. (Picha na Modewjiblog)
Kampuni ya MultiChoice Tanzania wasambazaji wa bidhaa za DStv nchini usiku wa Mei 26 wameweza kujumuika kwa pamoja katika kusheherekea siku ya Afrika kwa kukutana na wadau wake Jijini Dar es Salaam na kufurahia paamoja fahari ya Afrika.
Wadau hao ni pamoja na wanahabari, Waendesha vipindi vya televisheni na radio, wasanii na baadhi ya wateja ambao walijumuika kwa pamoja usiku maalum ambao pia walipata kula na kunywa pamoja na kubadilishana mwazo.
Awali wakati wa ufunguzi wa hafla hiyo maalum, Meneja Uhusiano na Masoko wa MultiAChoice Tanzania, Bi. Furaha Samalu alieleza kuwa, MultiChoice wanajisikia fahari katika ushiriki wao wa kuleta mabadiliko na maendeleo tangu kuanzishwa hapa Barani Afrika miaka 20 iliyopit huku ldngo kuu ni kuwa na maudhui ya kila siku ya kiafrika.
Aidha, Bi. Furaha Sumalu alibainisha kuwa, kwa kuthamini Afrika, hata chaneli wameweka zinazolenga Afrika zikiwemo: Africa Magic, Maisha Magic Bongo, Maisha Magic East ambapo ndani ya chaneli hizo zimekuwa na mtazamo tofauti kuhusu Afrika hivyo watanzania na waafrika kwa ujumla ni wakati wa kuchangamkia bidhaa bora za DSTV ilikufurahia uhondo huo wa Kiafrika na mambo mbalimbali yanayotokea ndani ya Afrika nan je ya Afrika.