Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimevuna wanachama 60 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kitongoji cha Wangbay, kijiji cha Logia, Kata ya Sigino Wilaya ya Babati.
Akikabidhi kadi wanachama wapya Mbunge wa Viti Maalum, Paulina Philipo Gekul, jana, katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Logia aliwaasa wananchi kuwa wavumilivu iwapo makada wenzao wanaogombea udiwani wakishindwa kwenye kura za maoni.
Aidha Bi Gekul amewataka waliochukua fomu za kugombea udiwani watakaoshindwa kutogawanyika na kukimbilia CCM badala yake wakubalina ndio watakao kuwa mameneja kampeni katika vijiji wanavyotokea maana wao wanajulikana kwa wapenzi, washabiki na wanachama wa Chadema.
Wanachama walio hamia Chadema walioongozwa na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Wangbay Kijiji cha Logia, Fabian Mathe ambaye alikuwa na haya ya kusema “Mimi nimekwishapigika na mateso nilionayo ni mengi CCM wamenitesa sana polisi kwenda ni kawaida leo nimeamua ninajua mnanionea huruma naomba msiendelee kuvumilia huko nimeona chama changu cha CCM kinamiliki wana watu wawili.”
“Mtendaji wenu ni wakala wa CCM hawa watendaji ndio wasimamizi wakuu bana mkurugenzi wanasema eti huyu sio mjumbe wa serikali ya kijiji, hivyo namna moja ya kukombolewa ni kuhama ndio kupatahaki,” alisema.
“Mbona wengine mlikuwa mnaniombea kura mlikuwa CCM? Karibu kwenye jeshi la ukombozi tupambane,” alisema.
Alikemea wananchi wa Singu wanaowakatalia wenyeviti kusoma mapato na matumizi eti waliteuliwa CCM akasema sasa hivi nimiliki ya Chadema hivyo wananchi wasahau ya kale wagange ya sasa na kuwataka wakubali kusomewa mapato na matumizi kuanzia tarehe 25 Desemba 2014.
Aliongezea kuwa endapo wananchi wakikataa wawafungie simu viongozi wajimbo na wilaya iliwaje wamalize tatizo hilo.
“Wale wanaojipanga kuvuruga ya Singu ya kusoma mapato na matumizi wanakosea sana maana mikutano hii po kwa mujibu wa sheria, mlishindwa kuwaondoa viongozi wenu kuanzia mwaka 2013,” alisisitiza.
“Kile kilichowafitinisha CCM ni kutofuata haki siku zote katika kura za maoni upo uwezekano wa kufunga na kama wamefunga na nivyema wajipange upya,” alisema.
Miongoni mwa sababu zilizotajwa na wanachama hao kukihama chama cha mapinduzi ni kunyimwa viwanja, ufisadi uliokithiri huku Emmanuel Demai, akisema matatizo mengi yanatatuliwa na Chadema.
Wakati Bashir Rajab akilizungumziasuala la Edward Lowasa kuhamia Chadema kuwa amelipokea kwa furaha kubwa maana yeye atakuwa kiungo muhimu katika Chadema.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment