Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday, 9 June 2015

WATAWA WAKWAMA NDANI YA LIFTI KWA SIKU TATU


Watawa wawili wameokolewa kutoka kwa lifti mjini Rome baada ya kukwama kwa siku tatu bila chakula wala maji.

Watatu hao mmoja wa miaka 69 raia wa New Zealand na mwingine wa umri wa miaka 58 raia wa Ireland walikwama ndani ya lifti hiyo siku ya Ijumaa baada ya kutokea kwa hitilafu ya umeme.
Watawa hao waligunduliwa siku ya Jumatatu wakati mfanyikazi mmoja kuwaita polisi, alipokosa kujibiwa baada ya kufinya kengele ya mlango.
Watawa wakwama ndani ya lifti kwa siku 3
Wakati polisi walipoingia kwenye nyumba hiyo, waliita kutaka kujua ikiwa kulikuwa na mtu ndipo watawa hao wakaitika wakisema kuwa wako ndani ya lifti.
Walipotolewa walisema kuwa waliomba sana. Kisha walipekwa hospitali iliyo karibu ambapo walipata matibabu.
CREDIT: BBC

No comments:

Post a Comment