
Moshi Abraham Nkonkota
Hayo aliyasema wakati wa ufunguzi wa shina la vijana 84 wa kudi la Tabora Music Association (TMA) kata ya Gongoni wanaojishughulisha na muziki, ujasiriamali na kilimo cha umwagiliaji.
Alisema endapo vijna hao watakubali kutumika na wanasiasa kama daraja la kutafutia uongozi nchi haitakuwa salama.
Nkonkota alisema eneo lolote duniani nchi hutumia vijana kujiletea maendeleo hivyo kundi la vijana ambalo ni kubwa linapaswa mnapaswa kuwa makini.
Aidha mwenyekiti huyo alisema vijana kuwa makini na dhana ya ubaguzi kwenye siasa,dini na ukabila kwani athari yake ni kubwa mbele ya jamii.
Alisema siku vijana mnatakiwa kuweka mbele utaifa na ubinafsi usiwe na nafasi kwa sasa hasa kipindi hiki cha uchaguzi 2015.
Kuhusu kikundi hicho kujihusisha na kilimo cha umwagiliaji,muziki na ujasiliamali mwenyekiti huyo aliwaeleza atashirikiana nao kutafuta ufadhili ndani ya serikali na wadau wa sekta hizo.
Alisema kwa kuwa kwa sasa muzki ndiyo wanaendelea nao aaliwasisitiza kutobweteka kwani muziki kwa sasa ni ajira.
No comments:
Post a Comment