Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday, 7 June 2015

KINGWANGALLAH AINGIA UWANJANI, ASEMA "FIKIRI TOFAUTI, AMUA MABADILIKO SASA!"


Na Hastin Liumba, NzegaMBUNGEE wa jimbo la Nzega mkoani Tabora Dkt Hamis Kigwangallah ametangaza nia ya kugombea nafasi ya Urais akiwa jimboni kwake na kusema Tanania aitakayo ni ipi na kutaja vipaumbele vyake vitatu.
Dhamira hiyo aliitangaza akiwa kwenye viwanja vya Parking wilayani Nzega na kusema siyo lazima uwe mtoto wa tajiri ndiyo uoneshe kipaji chako.
Alisema hili ndilo peke yake linanipa sababu ya ziada ya kwa nini nitamani kuota kuwa Rais, ambapo anataka awe mfano hai wa mafanikio ya Ndoto ya waasisi wa Taifa letu, kuwa sote ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tuna haki na fursa sawa bila kujali nani anatokea familia ipi.
Dkt alisema hii ni Tanzania ya ndoto za waliotutangulia, ni lazima atokee kiongozi wa kizazi hiki anayetamani kuiongoza Tanzania itakayodumu kwenye misingi hii kwamba sisi sote ni ndugu, na tuna fursa sawa.
Alisema kimaisha na kibinafsi ni haki ya binadamu na si hisani kwamba, mtoto wa mama ntilie kama nilivyokuwa mimi hapa, ana haki na fursa ya kuwa mbunge ama Rais wa nchi, sawa kabisa na mtoto wa Mbunge.
Aidha anasema amefika hapa kwa sababu chama changu kina mfumo mzuri ulioasisiwa na Mwl. Nyerere na umelindwa na Wenyeviti waliomfuatia mpaka na sisi tumeukuta.
“ Leo nimefika hapa kwa sababu Rais Jakaya Kikwete na wajumbe wenzake wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu walitumia misingi imara iliyowekwa na waasisi wa Chama changu kuamua kuwa nami nina haki ya kuwa Mbunge.”alisema.
Alisema Babu na Baba yake waliishi Kijijini Goweko, Mlimani, na alikuwa mfugaji mkubwa wa ng’ombe na mrina asali mashuhuri.
Anasema anainaishi nikiamini kuwa hadithi ya maisha yangu ni mfano hai kwa maisha ya watanzania wengi.
Dk Kigwangallah alisema kazi yake imenifikisha sehemu nyingi za nchi yetu, vijijini na kwenye majiji, imenikutanisha na watu wa kila aina, matajiri kwa maskini, wazee kwa vijana – hakuna hata mmoja kati ya watu hawa anayetegemea Serikali itamtatulia kero zake zote.
Aidha anasema nenda kwa wafanyabiashara wakubwa kule Pugu Road viwandani, kwa watumishi pale hospitali ya Taifa Muhimbili, ama pale sokoni Kariakoo kwa wafanyabiashara, wote watakuambia hawapendi kuona kodi zao zikitafunwa na wachache pale TRA, ama kulipa posho za bure kwa wabunge na mawaziri kule Bungeni, kulipia mashangingi ya viongozi na watendaji, kulipia tiketi za ndege daraja la kwanza kwa ajili ya safari za viongozi.
Aidha kingine ni wataalamu wetu kwenda kujifunza kupambana na umaskini wakati wakirudi wanauacha uzoefu uwanja wa ndege, ama kulipia semina, warsha na makongamano ya wataalamu ya kuandika sera za MKUKUTA, MKURABITA na kuandaa bajeti zisizotekelezwa kila mwaka.
Watanzania wanataka kupata huduma bora za afya, elimu, maji, miundombinu. Watu hawatarajii serikali itabeba mizigo yao yote.
Alisema serikali yake ananaamini kabisa, kwamba tukibadili kidogo tu vipaumbele vyetu, tukibadili namna tunavyoendesha serikali, tukibadili kidogo namna tunavyoendesha uchumi wetu, tutaweza, kwa kiasi kikubwa, kubadili muelekeo mzima wa maisha ya baadaye.
 “Tutatoa fursa sawa kwa kila mtanzania kuishi kwa matumaini, kwamba atabadili maisha yake wakati wowote ule kuanzia leo. ……Tutaweza kuamsha ari ya kila mtanzania kuongeza bidii kwenye kazi akitumaini na kuamini kuwa kesho yake itakuwa bora kuliko jana yake, kuwa naye ataishi kwa heshima, raha na starehe ndani ya nyumba yake.”alisema.
Alisema harakati za kutafuta uongozi siyo vita ya kufa na kupona, ni mpango wa Mungu kwa watu wake, kuwa lazima apatikane kiongozi miongoni mwetu; kwamba apatikane kiongozi atakayetatua kero zetu na kupambana na changamoto zetu kwa dhati, kiongozi mwenye hofu ya Mungu na anayechukia rushwa, ubadhirifu na ufisadi.
 Dk anasema ni lazima apatikane kiongozi atakayekemea uzembe, uvivu na kuhamasisha uchapakazi wa bidii na uwajibikaji,na ukimtazama machoni uione hofu yake kwa Mungu na utayari wake wa kuwatumikia wenzake,Hii ni safari iliyojaa imani na ndoto za watu, si safari iliyojaa tamaa na ulaghai wa wachache kwa maslahi ya wachache.
Alisema kuna hoja ya ujana na uzoefu kwenye uongozi, haswa haswa kwenye serikali, ni hoja dhaifu, sababu kwanza, hakuna mwenye uzoefu na Urais ukiondoa Hayati Baba wa Taifa, Julius K. Nyerere, Mzee Ali Hassan Mwinyi, Mzee Benjamin W. Mkapa , na anayemalizia muda wake, Dkt. Jakaya M. Kikwete.
Wengine sisi, sote tuna uzoefu kwenye mambo mengine tu, siyo Urais, na uzoefu uko kwenye namna nyingi mbalimbali, uzoefu wa mtu mmoja siyo wa mwingine.
Alisema  uchaguzi siku zote unahusu mambo ya baadaye, siyo ya zamani, unahusu ndoto ya kuwaletea wananchi maisha bora ya kesho kuliko ya jana. Tupimeni kwa maarifa yetu, kwa uthabiti wa nia zetu, kwa uadilifu wetu na kwa kiasi gani tumeonekana tuna hofu ya Mungu wetu.
Aidha alisema ni nani kati yetu ataweza kuwa Amiri-jeshi-mkuu, siyo kwa uanajeshi wake bali kwa uwezo na utayari wake wa kuwashirikisha wataalamu wa majeshi na kuamua kwa busara kutumia nguvu za kijeshi pale inapolazimika baada ya kupima na kuchambua aina nyingine zote za kutafuta suluhu za migogoro kabla ya kuamua vita.
Aidha ni nani kati yetu anayeamini katika Haki ya kupata huduma bora za afya, elimu, maji, kama wanavyopata wabunge na mawaziri wetu, kama wanavyopata mahakimu na majaji wetu, kama wanavyopata wafanyabiashara na wakurugenzi wetu.
“Nani kati yetu ataweza kuhakikisha kuwa watanzania wote wanapata haki hizi bila kutazama hali zao kiuchumi ama daraja zao kijamii," alisema.
Alisema yeye natangaza rasmi sasa, kuwa nina dhamira ya dhati ya kuwapeleka watanzania kwenye nchi ya ndoto na ahadi za waasisi wetu; na kwamba kama nitateuliwa na Chama changu kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2015 vipaumbele vyake vitatu anavitekeleza vyema.
Alitaja vipaumbele hivyo ni Kuondoa umaskini na kukuza uchumi kwa malengo ya kuzalisha fursa nyingi zaidi za ajira nchini,Kutoa huduma bora za kijamii (elimu, afya, maji na miundombinu ya barabara na umeme) na Kudumisha utawala bora nchini
Alisema anapoamua kuomba nafasi ya Urais anafahamu fika kuwa, ili tufikie malengo tuliyojiwekea tunapaswa kufanya mambo makubwa mawili, japokuwa kwa maumivu, lakini ni lazima yafanyike; kwanza, kubana matumizi ya serikali kwa kupunguza ukubwa wa serikali, kuondokana na matumizi yasiyo ya lazima ya serikali  kama safari, na kubana mianya ya kodi, kupunguza misamaha ya kodi, kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na kutanua wigo wa kodi.
Kingine ni na la pili ni kuongeza shughuli za uzalishaji ili kuongeza wigo wa kodi. Hili ni lazima liendane na kupunguza viwango vya kodi ili kutia chachu ya wawekezaji kuwekeza.
Ni dhamira yangu kuona Tanzania ikigeuka kuwa nchi mzalishaji mkubwa wa pamba kwa njia na zana za kisasa, na ikiuza nguo nje ya nchi badala ya pamba ghafi.
"Ni dhamira yangu kuona Tanzania ikiuza bidhaa za korosho zilizomenywa na kuongezewa ubora badala ya kuuza korosho ghafi," aliongeza.
Ni dhamira yangu kuona kila mtanzania anamiliki hati yake ya bima ya afya mkononi. Na kila mtanzania akipata huduma bora za afya. Natamani kuijenga Tanzania ambapo badala ya wananchi wetu kutibiwa Apollo nje ya nchi, watibiwe Muhimbili. Natamani kuijenga Tanzania ambayo Marais wetu wastaafu watajivunia kutibiwa kwenye hospitali za ndani ya nchi kama ilivyokuwa kwa Mzee Madiba.
Alibainisha kuwa asilimia 5 ya bajeti yote iwekezwe kwenye sayansi, teknolojia na utafiti. Ni dhamira yangu kuona SIDO, BICO, DIT, COSTECH, NIMR na vyuo vikuu vyetu vyote vikishiriki kikamilifu kujenga uchumi wa viwanda vidogo vidogo na kuboresha huduma za kijamii.
Alisema  na kwamba wasomi wetu wanatumia elimu, ujuzi na data kutokana na tafiti, na kwamba tafiti zinatumika ipasavyo kuleta mapinduzi ya kilimo, viwanda na biashara katika nchi yetu. Kama nikipata fursa ya kuwa Rais wa nchi yetu, nitahakikisha hili linafanyika ndani ya mwaka mmoja.
Kingine ni Mfuko wa mikopo ya nyumba bora kwa watu wote. Ni dhamira yangu kuona tukiwekeza kwenye upimaji wa ardhi nchi nzima na miji na vijiji vikichorwa na kupangwa upya.
Aidha angependa kama Rais kuona Bima ya afya kwa watu wote,Elimu ya bure kuanzia msingi mpaka high school.
Aliongeza kuwa uwepo Mfuko wa kukopesha wananchi wanaojishughulisha na kilimo, viwanda na biashara ndogo ndogo. Tutaanzisha mfuko huu wa mikopo kwa kuwekeza bilioni 500 kila mwaka na kuimarisha kitengo cha ustawi wa jamii kwenye halmashauri kwa ajili ya kuwaelimisha, kuwaunganisha kwenye vikundi vya kudhaminiana na kuratibu shughuli zao.
Alisema kukopesha wananchi wanaowekeza kwenye kilimo kikubwa cha kibiashara, viwanda na biashara ya nje ya nchi. Tutahakikisha kila mkulima mkubwa anaunganishwa na wakulima wadogo na pia anaunganishwa na viwanda na masoko. Mfuko tutauanzisha ndani mwaka mmoja, na kila mwaka tutawekeza shilingi bilioni 500.
Alisema  kwa kufanya haya tutakuwa na uhakika wa kuzalisha ajira rasmi 200,000 kila mwaka, na ajira zisizo rasmi zaidi milioni kumi kila mwaka. Na uchumi huu utamgusa kila mtanzania.

No comments:

Post a Comment