Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Ukonga marehemu Bi. Eugen Mwaiposa ambaye amefariki usiku wa kuamkia jana Juni 2, 2015 nyumbani kwake mjini Dodoma. Taarifa za kifo chake zimetangazwa wakati bunge likiendelea na mjadala wa bajeti ya wizara ya afya hivyo kupelekea bunge hilo kuahirishwa hadi Juni 4, 2015.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mhe. Dkt Seif Rashid akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2015/2016 jana mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge Mhe. Jenista Mhagama (mwenye nguo nyekundu) akimfariji Mwenyekiti wa Bunge Bi. Lediana Mng’ong’o mara baada ya bunge kuahirishwa kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Ukonga Bi. Eugen Mwaiposa. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora Bi. Mary Nagu na kushoto ni wabunge James Mbatia na Goodluck Ole Medeye.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Anjela Kairuki (kushoto) akitoka nje ya ukumbi wa bunge akiwa ameambatana na wabunge Bi. Mary Mwanjelwa na Rita Kabati baada ya bunge hilo kuahirishwa kufuatia kifo cha Mbunge wa Ukonga Bi. Eugen Mwaiposa.
Baadhi ya wabunge wakiwa kwenye hali ya simanzi baada ya kutangazwa kifo cha aliyekuwa mbunge wa Ukonga Bi. Eugen Mwaiposa kilichotokea usiku wa kuamkia jana nyumbani kwake mjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment