Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday, 9 June 2015

AMANI KITU MUHIMU KUELEKA UCHAGUZI - PAROKO


Rais Kikwete akipiga kura mwaka 2010

Na Hastin Liumba, NzegaWATANZANIA wameaswa kudumisha amani katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge na Rais.
Hayo yalisemwa na Paroko wa Parokia ya kristo Mfalme Kitangiri wa jimbo kuu la kanisa katoliki lililopo kata ya Miguwa wilaya ya Nzega Tabora Paroko Christopher Matunda.
Paroko matunda alisema awali kabla ya ibada waumini walifanya maandamano ya kuiombea nchi amani na utulivu katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Alisema ifikie mahali kila mtu kwa nafasi yake kuomba amani,utulivu na kuienzi amani kwa vitendo na siyo maneno tu.
Aidha alitoa wito kwa watanzania katika kipindi hiki tuwe makini na wabinafsi na wale wote ambao wanawania nafasi za uongozi ngazi za Udiwani,Ubunge na Urais.
Alisema maswala haya kwa sasa yanahitaji elimu zaidi kwani elimu ni kila kitu kwa maisha ya mawanadamu.
Kwa upande wake muumini wa kanisa hilo John Dotto alisema umasiki ni jambo ambalo limekuwa likimkera na kwamba kuondoa umasikini kunahitaji kutilia mkazo kuwekeza kwenye elimu.
Dotto alisema hayo wakati wa misa hiyo na kwamba Parokia hiyo iko kwenye ujenzi wa kanisa jipya ambapo yeye binafsi amechangia kiasi cha sh milioni kumi (10).
Alisema binafsi ametoa fedha kuchangia kanisa na analosali hivyo mchango wake usihusishwe na kampeni za ubunge na kama ataingia kwenye siasa kuwania nafasi yoyote muda ukifika atafanya hivyo.
‘Ndugu zangu waumini nimechangia kiasi hicho cha fedha nia yangu nataka kanisa ninalolitumia kuabudu limalizike’alisema Dotto.
Alisema yeye amezaliwa kata ya Miguwa hivyo haoni sababu ya kusadiana na ndugu zake katika kuleta maendeleo nyumbani alikozaliwa.
Kwa upande wao waumini wa kanisa hilo kwa niaba ya wenzao Paulo Bumbi na Sophia Victoria waliunga mkono kanisa kuiombea nchi amani na utulivu.
Walisema amani ni kitu chema hasa kipindi hiki cha uchaguzi mkuu lakini elimu zaidi inahitajika kuhubiri amani na wazazi wanapaswa kuelewa hilo na kutilia mkazo.
Kanisa jipya linalojengwa hadi sasa limejengwa kwa kiasi cha sh milioni 35 na ujenzi wake unaendelea.

No comments:

Post a Comment