Magdalena Sakaya
Na Hastin Liumba, KaliuaMBUNGE wa viti maalumu kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF) Magdalena Sakaya amemwomba Rais Dk Jakaya Kikwete kutia saini ili wauaji wanne wa watu wenye walemavu wa ngozi (Albino) waliohukumiwa kunyongwa adhabu hiyo inatekelezwa.
Sakaya alitoa ombi hilo wakati akiongea na wananchi wa wilaya ya Kaliua mkoani Tabora kwenye mkutano wa hadhara akiwa kwenye ziara yake ya siku mbili katika kata za Zugimlole,Usinge na Kaliua.
Alisema kitendo cha serikali kuendelea kukaa kimya na kusita kuchukua hatua ya kutekeleza huku hiyo baada ya Mahakama kuwatia hatiani watuhumiwa hao kunalitia doa taifa letu kwa mataifa mengine.
Mbunge huyo alisema watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) wanaishi ndani ya nchi yao kwa hofu na unyonge mkubwa hivyo ni wakati sasa serikali ikachukua hatua kukomesha mauaji haya kwa kutekeleza adhabu za kifo kwa wahusika.
Aidha alionya baadhi ya watu hasa wanasiasa kama wanahusika kuachana na dhana hiyo kwani kuna shutuma kila kona ya nchi kuwa wanasiasa wanahusika.
“Kama kweli sisi wanasiasa tunahusika ni jambo la aibu kwetu…..kwani mwanasiasa endapo unahusika unajisikiaje unapoingia bungeni ukiwa una garufu ya damu baada ya kuua Albino.”alisema.
Alisema ifikie mahali jamii ikabadilika na kuachana na imani za kishirikina kwani nchi kimataifa inazidi kuchafuka.
Sakaya aliwasihi wananchi kuungana na kuwafichua wale wote wanahusika na mipango ya kuteka,kuua na kuchukua viungo vya watu wenye ulemavu wa ngozi Albino.
“Katika hilo ndugu zangu wananchi naomba tuungane kukomesha aibu hii kwa taifa letu…namuomba tu Rais Dk Jakaya Kikwete kukubaali kuweka saini ili hawa watu wanne wanayongwa hii itasaidia sana kukomesha hali hii.”aliongeza Sakaya.
No comments:
Post a Comment