Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya (kulia) akisikiliza kesi yake
Mahakama ya Kimataifa kuhusu Uhalifu wa Kivita (ICC) imefunga kesi yake dhidi ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.
Alikuwa ameshtakiwa na uhalifu dhidi ya binaadamu kufuatia ghasia zilizojiri baada ya uchaguzi wa mwaka 2007.
Mwezi Disemba kiongozi wa mashtaka alimuondolea mashtaka kiongozi huyo akisema kuwa serikali ya Kenya imekataa kuipatia mahakama hiyo ushahidi muhimu.
Hatahivyo mahakama hiyo imesema kuwa upande wa mashtaka una uwezo wa kuanzisha mashtaka mapya katika siku za usoni iwapo ina ushahidi wa kutosha.
Kesi ya naibu wa rais William Ruto inaendelea katika mahakama hiyo.
Mawakili wake walishindwa kuiondoa kesi yake.
CREDIT SOURCE: BBC
No comments:
Post a Comment