Na Hastin Liumba, Kaliua
WANANCHI wa kata ya Zugimlole wilaya ya Kaliua mkoani Tabora
wamemkataa mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Zugimlole Azbert Kamala kwa hatua
yake ya kujigeuza afisa mtendaji wa kata na askari mgambo na kushirikiana na
askari mgambo wengine kukamata wahalifu.
Hayo yalibainika kwenye mkutano wa hadhara kufuatia ziara ya
mbunge wa viti maalumu (CUF) Magdalena Sakaya.
Wananchi hao walimueleza mbunge huyo kuwa wamefikia mahali
wamechoshwa na mwalimu mkuu huyo licha ya kutoa taarifa serikalini lakini hadi
sasa mwalimu yupo kwenye kituo chake cha kazi.
Selegedu Dushonde mkazi wa kata ya Zugimlole alisema mwalimu
mkuu huyo aliwahi kumkamata mchungaji wa n g`ombe zake 20 Mayala Joseph (18)
mwezi April 2014 na kumwambia ni mtoro wa shule.
Alisema wakati anakamatwa kwa kushirikiana na baadhi ya
mgambo walimchukua hadi kwa mama yake mzazi na kisha walilazimisha wapewe sh
500,000 fedha ambazo walipewa ili Joseph aachiwe na kesi ifutwe.
Alisema walilifikisha kwa mwenyekiti wa kitongoji Jidagina
Luboke na mratibu kata elimu Siphela Charles.
Hata hivyo alisema mwenyekiti wa kitongoji alilazimika kumuita
mwalimu mkuu huyo lakini aligoma hadi alipokamatwa na kulala kituo cha polisi
Kaliua siku mbili.
Alisema siku chache alikamatwa na polisi bila kosa na
kuwekwa ndani ambapo mama yake mzazi alilazimika kutoa sh 300,000 ana aliachiwa
toka kituo cha polisi.
Hata hivyo hadi sasa licha kuachiwa bado mwalimu huyo
hajachukuliwa hatua yoyote na ameachiwa na kuendelea kutanua na kutoa vitisho
kuwa yeye ni serikali hakuna wa kumbabaisha.
Wakichangia kwenye mkutano huo baadhi ya wananchi
walimueleza Sakaya afanye awezavyo mwalimu huyo aondoke kijijini kwao
vinginevyo watachukua hatua ya kumtoa mbio.
‘Mkuu tusaidie tuondokane na hii kero mwalimu mkuu huyo
hatumtaki kijijini kwetu……nenda katusemee kwa mabosi wake aondoke hapa
tutamshughulikia tumechoshwa naye.’walisema.
Mwalimu mkuu Azbert Kamala alipotwafutwa shuleni na nyumbani
kwake hakupatikana ambapo gazeti hili lilifanya jitihada na kufanikiwa kuonana
naye lakini hakutoa ushirikiano na aligoma kuongea wala kukanusha tuhuza hizo.
Mbunge wa viti maalumu (CUF) Magdalena Sakaya aliwaeleza
wananchi hao suala hilo analichukua na mwalimu mkuu huyo ataondoka kwani
amesikia kilio chao.
‘Ndugu zangu nimewasikia huyo mwalimu ataondoka nitakula
naye sahani moja kuhakikisha hatua za kinidhamu zinachukua mkondo wake……hatuwezi
kuvumilia wezi kama hawa alikuja kufundisha au kuwa mgambo.”alisema.
No comments:
Post a Comment