Wizara
ya Fedha na Mipango imekamilisha ujenzi wa mfumo wa malipo moja kwa moja
kupitia akaunti za walipwaji katika mtandao wa malipo wa Benki Kuu ya Tanzania (Tanzania
Interbank Settlement System – TISS), katika mkoa wa Morogoro, hatua
inayolenga kuongeza ufanisi wa miamala mbalimbali inayofanywa na serikali.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James amezitaja Halmashauri ya
Manispaa ya Morogoro, Halmashauri za Wilaya ya Kilombero, Morogoro, Mvomero,
Kilosa na Ulanga, kwamba zitaanza kufanya malipo hayo kwa mfumo huo wa TISS
kuanzia mwezi Desemba mwaka huu.
“Nia
ya Serikali ni kuhakikisha kwamba ifikapo mwezi Desemba, 2016 Halmashauri zote
zilizopo katika Mkoa wa Morogoro ziweze kufanya malipo kwa kutumia mfumo wa
malipo wa TISS” alisema Dotto James.
Amesema
kuwa malipo hayo yatafanyika kwa
kutumia mfumo wa malipo wa TISS uliojengwa katika mikoa yote Tanzania Bara
ikiwemo Ofisi za Hazina Ndogo na Sekretariati za Mikoa, Wizara, Idara za
Serikali zinazofanya malipo yake kupitia Ofisi Kuu ya Malipo (CPO) iliyopo
Hazina, malipo ya Pensheni kwa wastaafu, Kitengo cha Kupambana na Fedha Haramu,
Mfuko wa Bunge, Mfuko wa Mahakama na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi.
“Hivi
karibuni mfumo huu wa malipo umeunganishwa katika Halmashauri ya Jiji la Dar es
salaam, Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Kinondoni na Temeke. Katika Halmashauri
ya Jiji la Mwanza, mfumo huu umeunganishwa katika Halmashauri za Wilaya ya Ukerewe, Magu, Sengerema, Kwimba, na Misungwi”
alifafanua Katibu Mkuu huyo.
Ameongeza
kuwa katika mkoa wa Mbeya, mfumo huo umefungwa katika Halmashauri ya jijini la Mbeya,
Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, Kyela, Mbarali, Chunya, Mbeya, Mbozi na Ileje
wakati mkoani Arusha maeneo yanayohusika ni Halmashauri ya Jiji la Arusha, Halmashauri ya
Wilaya ya Arusha, Longido, Meru, Monduli, Karatu, Ngorongoro.
Halmashauri
ya Manispaa ya Dodoma mfumo huu umeunganishwa katika Halmashauri ya Wilaya ya
Bahi, Kongwa, Mpwapwa, Chamwino, na Kondoa wakati mkoani Tanga, Halmashauri ya
Jiji la Tanga, Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga, Pangani, Muheza, Handeni,
Kilindi, Korogwe, Lushoto na Mji wa Korogwe zimeunganishwa katika mfumo huo.
Kuanzia
Julai, 2010 hadi katikati ya Mwezi Novemba, 2016 mfumo huu ulikuwa tayari
umeunganishwa katika Serikali Kuu na Mamlaka za Serikali za Mitaa zilizopo
katika Mikoa ya Dar es salaam, Mwanza, Mbeya, Songwe, Arusha, Dodoma na Tanga
ambapo umeonesha mafanikio makubwa” Alisema Bw. Dotto James
Katibu
Mkuu huyo amewataka wadau wote wanaofanya biashara na maeneo yaliyofungwa mfumo
huo mkoani Morogoro, kuwasilisha taarifa muhimu ili ziweze kuingizwa katika
Mtandao wa malipo wa Serikali [Intergrated Financial Management System (IFMS)]
ili uanze kutumika kuanzia Mwezi Desemba mwaka huu kufanya malipo.
Taarifa
hizo zinahitajika kwa kuwa ni muhimu ili kuwezesha malipo kufanyika kwa
mlipwaji, ikiwa ni pamoja na Namba ya akaunti ya benki, Namba ya tawi la benki, Jina la akaunti, Aina ya akaunti, Namba ya kuandikishwa
biashara, Namba ya kuandikishwa Kampuni, Namba ya Mlipakodi, Jina la benki na Jina
la Tawi la benki.
“Hivyo
Makampuni na watu wanaofanya biashara na Halmashauri
ya Manispaa ya Morogoro, Halmashauri za Wilaya ya Kilombero, Morogoro, Mvomero, Kilosa, na Ulanga
wanashauriwa kuwasiliana na Halmashauri husika ili waweze kupatiwa fomu
maalum za kujaza taarifa hizo muhimu” Alisisitiza Dotto James.
Amesema
kuwa zoezi hilo ni endelevu ambapo
Serikali itaendelea kufunga mfumo huo kwenye mikoa na Wilaya zote zilizobaki
upande wa Tanzania Bara.
Imetolewa
na :
Benny Mwaipaja
Kaimu Mkuu wa Kitengo
cha Mawasiliano
Wizara ya Fedha na
Mipango
No comments:
Post a Comment