Kamanda wa
Polisi Mkoani Arusha Charles
Mkumbo
Na Woinde Shizza, Meru
MWANAFUNZI wa
kidato cha tatu katika shule ya sekondari Kitefu iliyopo Meru mkoani Arusha amenusurika kufa mara baada ya kubakwa na
kuteketezwa kwenye korongo la mchanga na
kusababishiwa maumivu makali yaliyomsababishia kushindwa
kuendelea na masomo yake kwa muda.
Akielezea tukio
hilo mwanafunzi huyo ambae amehifadhiwa jina kwa sababu za kimaadili alisema kuwa tukio hilo lilitokea novembar 13 majira ya saa
12.30 alipotoka kwa kinyozi.
Alisema kuwa ghafla
akiwa anarudi nyumbani alikutana na mtu huyo aliyemfanyia
kitendo hicho na kuanza kumkaba shingoni na kumziba mkono ili asitoe sauti na ndipo alipomfanyia kitendo hicho cha ukatili
ambacho kimemfanyia ashindwe kuendelea na masomo yake vizuri.
"Nilijitahidi sana kupiga kelele ila kutokana na alivyokuwa
amenikaba shingoni alinifanyia kitendo hiki kikatili ambacho
kimejipelekea nishindwe kuendelea na masomo yangu kwani baada ya
vipimo nimeonekana aliniumiza sehemu nyingi ikiwemo hata kifua
changu" alisema mwanafunzi huyo.
Kwa upande wake mama mzazi
wa mwanafunzi huyo aliyejitambulisha Rambikiaeli Akyoo
alisema kuwa kutokana na vitendo vya ukatili kukithiri kwa mabinti zao ni vema serikali ikawa inawachukulia hatua mapema wanaohusika
kwani tangu akamatwe mtuhumiw huyo na kupellekwa kituoni bado
hajasomewa shtaka linalomkabili hivyo kufanya wanaohusika na
vitendo hivyo kuona wako sawa kwa vile hakuna hatua kali
inayochukuliwa mapema dhidi ya matukio hayo.
Naye mkuu wa
shule hiyo Nkoe Nicolaus alisema kuwa tukio hilo limemfanya mwanafunzi huyo aathirike kisaikolojia kwani tangu afanyiwe ukatili
huo ameshindwa kiendelea na masomo yake vizuri hivyo anawashauri
wazazi wa binti huyo kumuhamisha shule hiyo na kumuhamishia
nyingine ili kimbadilisha mawazo ya kifkra.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa kitongoji cha kitefu tanesco Samweli
Matayo alikiri kutokea kwa tukio hilo katika kitongoji chake na
kusema kuwa mara baada ya taarifa walifanikiwa kumtia hatiani
mtuhumiwa aliyetambulika kwa jina la Wilson Elias ambae
ndie aliyehusika na ukatili huo na kumfikisha katika
kituo kidogo cha polisi usa river ili kukabiliana na shutuma hizo.
Kamanda wa polisi Charles Mkumbo amethibitisha
kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo ambapo limesema kuwa
mtuhumiwa alikamatwa kwa rb namba RB/R/4250/2016 na
atafikishwa mahamani upelelezi
ukikamilika.
No comments:
Post a Comment