Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 4 March 2016

'TAMASHA LA INJILI NI ZAIDI YA HUDUMA'

Addo November

Na Mwandishi Wetu
CHAMA cha Muziki wa Injili Tanzania (CHAMUITA) kimeeleza  kwamba Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Pasaka  iliyo chini ya Kampuni  ya  Msama Promotions  inatekeleza neno la Mungu na si huduma kama inavyodhaniwa na jamii.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Chamuita, Addo November ndio maana mwaka huu wamelihamishia tamasha hilo mikoa ya Kanda ya Ziwa na kuachana na Dar es Salaam kama ilivyozoeleka.
November alisema kwa kuwa Msama ameonesha kwamba tamasha hilo ni sehemu ya huduma ametumia fursa hiyo kuwaomba wakazi wa mikoa ya Geita, Mwanza na Wilaya ya Kahama na mikoa ya jirani kujitokeza kwa wingi ili kupata ujumbe wa neno la Mungu kutoka kwa waimbaji mbalimbali.
November alisema kampuni ya Msama imejipambanua kwamba kupitia tamasha la mwaka huu kuwasaidia walemavu ambako watakabidhiwa baiskeli zaidi ya 100.
Aidha naye Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema wanaendelea na mchakato wa kufanikisha ibada hiyo muhimu kupitia waimbaji na viongozi wa dini.
Msama alisema tamasha hilo linatarajia kuanza Machi 26 mkoani Geita, Machi 27 Mwanza na Kahama itakuwa Machi 28 ambako waimbaji mbalimbali wamethibitisha kushiriki katika tamasha hilo.
“Nawaomba wakazi wa mikoa ya Kanda ya ziwa kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha msaada kwa wenye uhitaji maalum kama yatima, walemavu na wajane, hivyo wakazi wa mikoa wajitokeze,” alisema Msama.
Msama alisema viingilio katika tamasha hilo ni shilingi 5000 kwa wakubwa na shilingi 2000 kwa watoto ambako waimbaji waliothibitisha kushiriki katika tamasha hilo ni Rose Muhando, Upendo Nkone, Bonny Mwaitege, Jesca BM, Joshua Mlelwa, Jenipher Mgendi, Faustin Munishi, Kwaya ya Wakorintho Wapili na Kwaya ya AIC Makongoro.

No comments:

Post a Comment