Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 1 March 2016

SIKU YA WANAWAKE MACHI 8, 2016 KUHIMIZA #UWIANOSAWAKIJINSIA


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wakati wa matembezi Machi 5, kabla ya kilele cha Siku ya Wanawake Duniani.
Maonyesho ya mwaka huu yanaandaliwa na kuratibiwa na Taasisi ya Wanawake Wenye Mafanikio (Tanzania Women of Achievement -TWA), ambao wameeleza kwamba mbali ya matembezi hayo, Machi 6 kutakuwa na kongamano kubwa la kujadili usawa wa kijinsia litakalofanyika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan.
TWA kupitia maadhimisho ya siku ya wanawake, wanaendelea kuhimiza usawa wa kijinsia ambapo jumbe mbalimbali zimeandaliwa kuhamasisha kampeni hizo.
Unaweza kupata taarifa zaidi kupitia tovuti yao:  http://twa.or.tz/pledge/

Jumuika ńa #HatujafikaBado ńa utume ujumbe kuhamasisha upatikanaji wa #UwianoSawaKijinsia @TWAorg #PledgeForParity

No comments:

Post a Comment