Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni akizungumza katika
shughuli ambapo Marekani iliikabidhi Serikali ya Tanzania Mbwa wa Maalumu wa
kubaini Madawa ya Kulevya na Pembe za Ndovu, katika tukio lililofanyika Bandari
ya Dar es Salaam leo. Wa pili kulia meza kuu ni Waziri wa Maliasili na Utalii,
Profesa Jumanne Maghembe, kulia ni Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Virginia
Blaser. Wa tatu kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Barabara, Aron Kisaka ambaye
alimwakilisha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano katika shughuli hiyo. Picha
zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kaimu
Balozi wa Marekani nchini, Virginia Blaser akizungumza katika shughuli ambapo
nchi yake iliikabidhi Serikali ya Tanzania Mbwa wa Maalumu wa kubaini Madawa ya
Kulevya na Pembe za Ndovu, katika tukio lililofanyika Bandari ya Dar es Salaam
leo. Kulia meza kuu ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne
Maghembe,wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Injinia Hamad Masauni, anayefuata ni
Mkurugenzi Msaidizi wa Barabara, Aron Kisaka ambaye alimwakilisha Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano katika shughuli hiyo. Picha na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni (kulia) akimuaga
Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Virginia Blaser mara baada ya Marekani kuikabidhi
Serikali ya Tanzania Mbwa wa Maalumu wa kubaini Madawa ya Kulevya na Pembe za
Ndovu, katika tukio lililofanyika Bandari ya Dar es Salaam leo. Kushoto ni Ofisa
Usalama Kanda, Ubalozi wa Marekani nchini, Bruce Paluch. Picha na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni
akiwafafanulia jambo waandishi wa habari mara baada ya Serikali ya Marekani
kuikabidhi Tanzania Mbwa wa Maalumu wa kubaini Madawa ya Kulevya na Pembe za
Ndovu, katika tukio lililofanyika Bandari ya Dar es Salaam leo. Kulia ni Naibu Inspekta
Jenerali wa Jeshi la Polisi nchini (D/IGP), Abdulharam Kaniki. Picha na Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni (kulia)
akisindikizwa na Kaimu Balozi wa
Marekani nchini, Virginia Blaser (kushoto) pamoja na Maafisa wengine wa ubalozi
huo, mara baada ya kumaliza shughuli ya Marekani ya kuikabidhi Serikali ya
Tanzania Mbwa wa Maalumu wa kubaini Madawa ya Kulevya na Pembe za Ndovu katika
tukio lililofanyika Bandari ya Dar es Salaam leo. Picha zote na Wizara ya Mambo
ya Ndani ya Nchi.
*****************************************************************************
No comments:
Post a Comment