Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 4 March 2016

CITY IKO MORO, KUIVAA SIMBA JUMAPILI

Kikosi cha Mbeya City FC  kimewasili salama  mkoani Morogoro tayari kwa kambi ya muda  kujindaa na mchezo wa ligi kuu ya Soka  Tanzania  bara dhidi ya Simba Sports Club  uliopangwa kuchezwa  Jumapili hii kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na mbeyacityfc.com mapema leo asubuhi kocha msaidizi wa City, Mohamed Kijuso amesema  kikosi kimewasili salama na leo watafanya mazoezi ya jioni kwenye uwanja wa chuo cha Jordan kilichopo mkoani hapa yatakayofatiwaa na program maalumu ambazo zitakuwaa zikiongozwa na Mwalimu Kinnah Phiri  kabla ya kuivaa Simba Siku ya jumapili jijini Dar.
“Tutakuwa uwanjani jumapili dhidi ya Simba  kwenye uwanja wa Taifa,hilo ndiyo jambo kubwa naweza kusema, tumesafiri na kufika hapa Morogoro hali za wachezaji wote 18 zikiwa  salama, kwa hilo tunamshukuru Mungu,jioni ya leo tutafanya mazoezi  hapo chuoni Jordan na kesho tutakuwa na program maalumu amabazo mwalimu ameziandaa” alisema.
Kuhusu Simba, Kocha huyo kijana ameweka wazi kuwa timu hiyo kutoka mtaa wa msimbazi ni nzuri hivyo hawataibeza hata kidogo licha ya matatizo kadhaa yaliyopo kwenye kambi yake kwa sasa, na kusema kikosi chake kitaingia uwanjani kupambana kwa nguvu zote kuhakikisha City inaibuka na ushindi.
“Nafahamu Simba wana matatizo madogo kwenye kambi yao hivi sasa,jambo hilo halitufanyi kuwabeza, bado ni timu nzuri na iko kwenye nafasi ya juu kwenye msimamo wa ligi tofauti na sisi, tutaingia uwanjani kupambana kwa nguvu zote kuhakikisha tunaibuka  na ushindi ili tuweze kujiimarisha zaidi, hivi sasa tunahitaji matokeo kwenye kila mchezo jambo ambalo pekee litatutoa tulipo na kutupeleka sehemu nyingine alisema”.
Akiendelea zaidi Kijuso alisema kuwa, anafahamu Simba ina wachezaji wengi vijana na wenye kasi pia inatumia nguvu nyingi kumiliki mpira kwenye eneo la kiungo hivyo  ni wazi City itatumia kikosi tofauti na kile kilichozoeleka huku mbinu  za kuhakikisha wanaziba nafasi zote  kwenye eneo la katikati ya uwanja zikiwa tayari zimeshafanyia kazi.
DSC_0290
Vifaa vikishushwa kwenye bus tayari kwa mazoezi.


No comments:

Post a Comment