Kiongozi Mkuu wa Jeshi la Muungano wa Afrika linalohudumu nchini Somalia, anasema kuwa wanajeshi watatu wa kikosi hicho wameshtakiwa kuhusiana na mauaji ya mwezi uliopita ya kundi moja la raia.
Maman Sidikou aliomba msamaha na akatoa kile ambacho amesema ni rambirambi kwa jamaa ya watu saba wa familia moja waliopigwa risasi katika mji wa Merka, kusini mwa mji mkuu Mogadishu.
Kwa mjibu wa kundi moja la kutetea haki za binaadamu- Human Rights Watch, wanajeshi wa umoja wa Afrika kutoka Uganda waliwashambulia kwa risasi watu waliokuwa wakihudhuria harusi baada ya msafara wao kulipuliwa kwa bomu.
Askari hao watahukumiwa katika mahakama ya kijeshi.
CREDIT: BBC
No comments:
Post a Comment