Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday, 3 August 2015

RAIS MSTAAFU WA GHANA AKUTANA NA WAFANYAKAZI WA ECOBANK TANZANIA JIJINI DAR ES SALAAM

Rais Mstaafu wa Ghana Mhe. Jerry John Rawlings akisikiliza kwa makini taarifa fupi iliyosomwa mbele yake na Afisa mkuu wa ubalozi wa Ghana hapa Tanzania Dr. Ken Kwaku kuhusiana na utendaji kazi wa Ecobank nchini Ghana na bara la Afrika kwa ujumla na kuzungumzia mikakati ya kudumisha uhusiano na kupanua wigo wa kibiashara kati ya Ghana na Tanzania. (Katikati) ni Balozi wa Ghana nchini Kenya Mhe. Karim. Mkutano huu uliandaliwa na Ecobank Tanzania ambapo ulifanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.

(Wa kwanza kulia) ni Mkurugenzi mkuu wa Ecobank  nchini Tanzania Mr. Enoch Osei-Safo pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo, wateja wa Ecobank na wageni waalikwa  wakimsikiliza kwa makini Rais mstaafu wa Ghana Mhe. Jerry John Rawlings aliyekua akiongea kuhusiana na mikakati ya kupanua wigo wa biashara kati ya Ghana na Tanzania kupitia benki hiyo. Mkutano huu uliandaliwa na Ecobank Tanzania ambapo ulifanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam
Rais Mstaafu wa Ghana Mhe. Jerry John Rawlings akizungumza wakati wa mkutano uliowakutanisha wafanyakazi wa Ecobank Tanzania, raia wa Ghana wanaoishi nchini Tanzania, wateja wa Ecobank na wageni waalikwa jijini Dar es salaam kuzungumzia mikakati ya kudumisha uhusiano na kupanua wigo wa biashara kati ya Ghana na Tanzania. Mkutano huu uliandaliwa na Ecobank Tanzania ambapo ulifanyika katika hoteli ya kimataifa ya Serena, Dar es salaam
Wafanyakazi wa Ecobank Tanzania wakimsikiliza kwa makini Rais mstaafu wa Ghana Mhe. Jerry John Rawlings aliyekua akiongea na wafanyakazi wa Ecobank Tanzania, raia wa Ghana wanaoishi nchini Tanzania, wateja wa Ecobank na wageni waalikwa jijini Dar es salaam kuzungumzia mikakati ya kudumisha uhusiano na kupanua wigo wa biashara kati ya Ghana na Tanzania. Mkutano huu uliandaliwa na Ecobank Tanzania ambapo ulifanyika katika hoteli ya kimataifa ya Serena, Dar es salaam 
Wafanyakazi wa Ecobank Tanzania kwenye picha ya pamoja na Rais mstaafu wa Ghana Mhe. Jerry John Rawlings (katikati) mara baada ya kumaliza mkutano uliowakutanisha wafanyakazi wa Ecobank Tanzania, raia wa Ghana wanaoishi nchini Tanzania, wateja wa Ecobank na wageni waalikwa jijini Dar es salaam kuzungumzia mikakati ya kudumisha uhusiano na kupanua wigo wa biashara kati ya Ghana na Tanzania. Mkutano huu uliandaliwa na Ecobank Tanzania ambapo ulifanyika katika hoteli ya kimataifa ya Serena, Dar es salaam

No comments:

Post a Comment