Mbunge wa Kigoma Kusini kwa tiketi ya NCCR- Mageuzi, David Kafulila
NA BEATRICE SHAYO
Kesi ya kashfa iliyokuwa imefunguliwa na IPTL dhidi ya Mbunge wa Kigoma Kusini kwa tiketi ya NCCR- Mageuzi, David Kafulila, imetupiliwa mbali na Mahakama Kuu.
Shauri hilo lilisimamiwa na wakili wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Jeremia Mtobesya.
Kafulila alifunguliwa keshi hiyo baada ya kuvujisha taarifa bungeni za utoaji holela wa pesa za Tegeta Escrow zaidi ya Sh. bilioni 220 kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kwa ajili ya kuwezesha uuzaji tata wa IPTL kwa Pan Africa Power Solutions Ltd (PAP).
Kati ya changamoto alizopitia ni kufunguliwa kesi hii kwa madai ya kashfa (defamation) dhidi ya IPTL.
Mtandao wa watetezi wa haki za binadamu THRDC unakumbushia sifa ulizozitoa juu ya David Kafulila wakati alipopata tuzo ya Mtoa taarifa za Rushwa ya Mwaka 2014 katika siku ya watetezi wa Haki za Binadamu '' Kafulila ni Mtetezi wa haki za binadamu, mtu aliyetayari kuhatarisha maisha yake kwa ajili ya wengine, mwanasiasa wa kitofauti duniani aliyeamua kutumikia umma na kuwaaibisha viongozi wala rushwa na wale wanaotumia vibaya madaraka ili kukandamiza haki a mwananchi wa kawaida.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment