Dirisha la usajili kwa vilabu vya Ligi Kuu nchini (VPL), Ligi Daraja la Kwanza (FDL) na Ligi Daraja la Pili (SDL) limefungwa jana ambapo vilabu vitatu tu vya VPL vimeshindwa kuwasilisha usajili wao wa wachezaji katika muda uliopangwa.
Klabu za Coastal Union ya Tanga, Stand United ya Shinyanga na Toto African ya jijini Mwanza zimeshindwa kuwasilisha usajili wao wa wachezaji, faini ni laki tano (500,000) kwa kila klabu iliyochelewesha usajili au itakayobadili majina au kuongeza majina baada ya tarehe ya jana.
Awali TFF ilitoa muda wa wiki mbili kwa vilabu vyote nchini kukamilisha usajili, ambapo vilabu 13 vya ligi kuu vimeweza kukamilisha ndani ya wakati, vilabu 24 vya ligi daraja la kwanza, vilabu 24 ligi daraja la pili pia vimeweza kukamilisha usajili wao ndani ya muda uliopangwa.
No comments:
Post a Comment