Mkurugenzi wa Sikika Bw. Irenei Kiria akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya Serikali kuongeza bajeti ya dawa muhimu na vifaa tiba kwa mwaka wa fedha 2015/16.
Utangulizi
Uwepo
na upatikanaji wa dawa muhimu na vifaa tiba katika vituo vya huduma za afya vya
umma ni moja ya viashiria vya huduma bora za afya katika nchi yoyote ile. Nchini Tanzania,
kumekuwa na uhaba wa mara kwa mara wa dawa muhimu na vifaa tiba katika vituo
vya huduma za afya vya umma ambao umekuwa ukizorotesha utoaji wa huduma za afya
na hatimaye kuzorotesha afya za wananchi walio wengi.
Tunatambua
jitihada za Serikali katika kuboresha upatikanaji wa dawa muhimu na vifaa tiba
nchini kama vile kutengeneza mipango mbalimbali ya kuboresha huduma hii.
Mathalani, Mpango Mkakakati wa tatu wa sekta ya afya una lengo la
kuboresha upatikanaji wa dawa muhimu na
vifaa tiba katika vituo vyote vya huduma za afya vya umma nchini. Pia, Mpango wa matokeo makubwa sasa (BRN) uliozinduliwa mapema mwaka huu unalenga
kuhakikiksha uwepo na upatikanajii wa dawa na vifaa tiba kwa asilimia 100
ifikapo mwaka 2019. Mbali na mipango na jitihada zote hizi, bado kumekuwa na
uhaba mkubwa wa dawa muhimu na vifaa tiba nchini
Uhaba wa dawa muhimu na vifaa tiba
Kwa
mujibu wa utafiti uliofanywa na Taasisi ya Ifakara nchini, (Ifakara Health
Institute) ilibainika kuwa, dawa muhimu zilikuwepo katika vituo vya huduma za
afya kwa asilimia 41 tu katika mwaka 2012 (MOHSW, 2013)[1]. Hii inamaanisha kuwa kwa takribani asilimia
60 ya dawa muhimu hazikuweza kupatikana katika vituo vya huduma za afya. Katika utafiti huohuo, ilibainika kuwa dawa
za antibiotks zilipatikanna kwa asilimia 57 tu kitu ambacho ni hatari sana kwa
magonjwa ya milipuko ambayo yamekuwa yakisababisha vifo kwa watoto na watu
wazima. Kwa upande wa vifaa tiba, utafiti uliofanywa na Sikika mwaka 2011[2],
ulionesha kuwa, asilimia 42 ya waganga wakuu wa wilaya waliohojiwa (N=71)
walikiri kutokuwa na akiba ya gozi kwa muda kati ya miezi mitatu hadi sita.
Moja
ya sababu zinazochangia uhaba wa mara kwa mara wa dawa na vifaa tiba ni ufinyu
wa bajeti inayotengwa kwa ajili ya dawa muhimu
na vifaa tiba. Ufinyu huu wa bajeti umekuwa ukiendelea siku hadi siku.
Hali halisi ya mwenendo wa bajeti ya Afya
Kwa
takribani miaka minne iliyopita, bajeti ya dawa muhimu na vifaa tiba imekuwa
ikishuka na kusababisha ongezeko kubwa la uhaba wa dawa muhimu huku waathirika
wakuu wakiwa ni wananchi wa hali ya chini kabisa. Kiuhalisia, bajeti inayopangwa
imekuwa haiendani na mahitaji halisi ya dawa muhimu na vifaa tiba nchini.
Makidirio ya dawa muhimu na vifaa tiba nchini yamekuwa yakiongezeka wakati
bajeti inayopangwa imekuwa ikishuka siku hadi siku. Mathalani, mahitaji ya dawa
muhimu na vifaa tiba yameongezeka
kutoka shilingi Bilioni 188 (2011/12) hadi shilingi Bilioni 577 ( 2014/15) huku bajeti
inayopangwa ikiwa ni shilingi Bilioni 123.6 (2011/12) na makadirio ya shilingi Bilioni 36.2 kwa mwaka
wa fedha 2015/16.
Kwa
miaka ya fedha 2011/12 na 2012/13 kulikuwa na ongezeko kubwa kidogo la bajeti
ya dawa muhimu na vifaa tiba ambazo ni shilingi Bilioni 123.4 na shilingi
Bilioni 80.5 ingawa hakukuwa na matokeo chanya ya upatikanaji wa dawa muhimu na
vifaa tiba katika vituo vya huduma za afya vya umma kwani takwimu zinaonesha
uhaba wa dawa hizo kwa takribani asilimia 60. Kama uhaba ulionekana kwa zaidi
ya asilimia 50 katika vipindi ambavyo bajeti angalau ilikuwa juu, hivyo ni
dhahili kuwa hali itakuwa mbaya mara
dufu kwa mwaka wa fedha 2015/16 ambao makadirio ya bajeti ya dawa muhimu na
vifaa tiba yameshuka hadi kufikia shilingi Bilioni 36.2 huku mahitaji
yakiongezeka kwa zaidi ya mara tatu ya
mwaka 2011/12. Makadirio ya bajeti ya mwaka 2015/16 yameshuka kwa zaidi ya
asilimia 48 kutoka katika bajeti ya mwaka uliopita(Jedwali 1) , cha kujiuliza hapa ni je hii bajeti inaendana
na malengo ya BRN ya kuhakikisha upatikanaji wa dawa muhimu kwa zaidi ya
asilimia 80 ifikapo mwaka 2016? Je bajeti hii imeangalia pia masuala ya
ongezeko la watu, ongezeko la vituo vipya vya huduma za afya ,ongezeko la
magonjwa na mahitaji halisi ya nchi?. Ni dhahili kuwa bajeti hii ni ndogo
ambayo sio tu itaathiri utoaji wa huduma za afya nchini bali pia itakuwa ni
mzigo mkubwa kwa wananchi hususani wa hali ya chini.
Jedwali 1 : Mwenendo wa bajeti ya dawa
muhimu na vifaa tiba
Chanzo
|
2010/11
|
2011/12
|
2012/13
|
2013/14
|
2014/15
|
2015/16
|
Fedda za Ndani (bn.)
|
30.3
|
49.8
|
34
|
34
|
60
|
36.2
|
Fedha za Nje (bn.)
|
33.6
|
73.6
|
46.5
|
30
|
10.5
|
0
|
Jumla (bn.)
|
63.9
|
123.4
|
80.5
|
64
|
70.5
|
36.2
|
Mahitaji
|
-
|
188
|
198
|
549*
|
577*
|
577+
|
Pengo (bn.)
|
|
64.6
|
117.5
|
485
|
506.5
|
540.8+
|
* Makadirio ya mahitaji kwa
mujibu wa hotuba ya Waziri wa Aya na Ustawi wa Jamii 2014/15 Bungeni
Kuchelewa kutolewa na kutotolewa kwa Fedha
yote Inayoidhinishwa
Pamoja
na bajeti ya dawa muhimu na vifaa tiba kuwa ndogo, kuna changamoto nyingine
kama vile kuchelewa kutolewa kwa fedha zilizo idhinishwa na kutotolewa kwa
fedha zote. Kuchelewa kutolewa kwa fedha kuna athiri mfumo mzima wa ununuzi na usambazaji
wa dawa hiyo hivyo kuchangia tatizo la upungufu wa dawa muhimu na vifaa tiba
katika vituo vya kutolea huduma. Kwa mfano, kipindi cha miaka minne iliyopita
(ukiondoa mwaka wa fedha 2012/13 ambapo fedha yote iliyoidhinishwa ilitolewa,) ni
asilimia 78 tu ya wastani wa fedha zinazoidhinishwa ndizo zimekuwa zilizokuwa, (jedwali 2 ).
Kuchelewa kutolewa kwa fedha na kutolewa kasi kisicho kamili kumeendelea
kuongeza tatizo la uhaba wa dawa nchini ambao tayari umesababishwa na bajeti
ndogo inayotengwa.
Jedwali 2: Fedha Iliyoidhinishwa vs. Fedha
iliyotolewa kwa ajili ya Dawa Muhimu na Vifaa Tiba
Mwaka
|
2010/11
|
2011/12
|
2012/13
|
2013/14
|
2014/15
|
Iliyoidhinishwa
|
63,900,000
|
123,400,000
|
80,500,000
|
64,000,000
|
70,500,000
|
Iliyotolewa
|
48,300,000
|
98,000,000
|
80,500,000
|
50,000,000
|
23,500,000*
|
% Iliyotolewa
|
75.6
|
79.4
|
100
|
78.9
|
33.3
|
*Kiasi
cha fedha kilichotolewa mpaka Aprili
2015
Fedha za uchangiaji (Cost Sharing) zilizoko
Halmashauri
Tunaelewa
kwamba Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inapanga kutumia mapato mbadala kutoka fedha za uchangiaji ili kusaidia
bajeti ya dawa muhimu na vifaa tiba katika mwaka wa fedha 2015/16. Hata hivyo
kutumia fedha hizi ili kuziba pengo ni kitu kisichowezekana kwa sasa. Kwa
sababu zipo changamoto nyingi zinazokabili matumizi ya mapato haya kama vile
mwongozo uliopitwa na wakati. Lakini pia, bima hizi za afya yaani NHIF na
CHF/TIKA imewafikia asilimia 20 tu ya wananchi wote nchini hivyo ni dhahiri
kabisa mapato yake hayawezi kuziba pengo la bajeti ya dawa katika mwaka wa
fedha unaokuja. Vilevile, makusanyo na matumizi ya fedha hizi katika baadhi ya
wilaya yamekuwa hayako wazi na kuibua maswali kama kuna uweledi katika matumizi
yake. Kwa sasa ni vigumu kujua ni kwa kiasi gani haya mapato ya halmashauri
yanachangia katika upatikanaji wa dawa muhimu na vifaa tiba, hivyo mapato haya
kutumika kwa sasa kuziba pengo ni kuweka maisha ya wananchi rehani. Ni sahihi
kabisa kwamba mapato haya yakiwa na mwongozo mzuri pamoja na mfumo wa uwazi na
uwajibikaji yanaweza kusaidia katika kuboresha upatikanaji wa dawa kama mkakati
wa muda mrefu na sio suluhisho la haraka kama ambavyo linavyochukuliwa kwa
sasa. Kuhamisha wajibu huu mkubwa wa
serikali wa kuwezesha upatikanaji wa dawa kwenda kwa serikali za mitaa ni
kukwepa wajibu na pia kuwanyima wananchi haki zao za msingi za afya.
Mapendekezo
- Serikali iongeze fedha za kutosha kwa ajili ya
dawa muhimu na vifaa tiba kwa mwaka wa fedha 2015/16 ili kuhakikisha
upatikanaji wa dawa nchini unaongezeka kufikia asilimia 80 mwaka 2016 kama
inavyotarajiwa na mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).
- Serikali kupitia wizara za Fedha na Afya
zinapaswa kuhakikisha fedha zilizotengwa kwa ajili ya dawa muhimi na vifaa
tiba zinatolewa kwa wakati ili kupunguza uhaba wa dawa nchini
- Wizara ya Afya
itoe mwongozo na mikakati inayoeleweka na kuwezekana katika kutumia mapato
ya afya ya halmashauri kwa ajili ya ununuzi wa dawa muhimu na vifaa tiba.
Pia ni vyema miongozo hii ikaweka wazi mifumo ya uwazi na uwajibikaji .
Mr. Irenei Kiria, Mkurugenzi
wa Sikika, S.L.P 12183 Dar es Salaam,
Simu: +255 222 666355/57, Nukushi: 2668015, Barua pepe: info@sikika.or.tz,
Twitter:
@sikika1, Facebook: Sikika Tanzania, Tovuti: www.sikika.or.tz
[1]
MOHSW (2013)
“Tanzania Service Availability and Readiness Assessment (SARA) 2012”
Ifakara
Health Institute, Dar es Salaam
[2] Sikika (2011) medicine and Medical Supplies Availability Report: Using
absorbent gauze availability survey as an entry point: A case of 71 Districts
and 30 health Facilities across mainland Tanzania, May 2011
No comments:
Post a Comment