Timu pekee iliyobakia kwenye mashindano ya shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika kutoka Tanzania, Yanga, imeendelea kuweka matumaini hai ya kusonga mbele baada ya kuiangushia kipigo kikali timu ya Platnum ya Zimbabwe kwa mabao 5-1.
Mchezo huo wa raundi ya kwanza ya vilabu vinavyoshiriki Kombe la Shirikisho la CAF, ulifanyika Jumapili jijini Dar es Salaam.
Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa kufungana mabao 2-1.
Kipindi cha Pili ndicho kilichokuwa kiama chya Platnum baada ya kuruhusu mabao matatu zaidi.
Wafungaji wa timu ya Yanga ni Mrisho Ngasa aliyefunga magoli mawili, Haruna Niyonzima, Salum Telela, na Amisi Tambwe walifunga bao moja kila mmoja. Kwa matokeo hayo Yanga imejenga mazingira ya kusonga mbele.
Michezo mingine ya Shirikisho ilikuwa katika ya Orlando Pirates ya Afrika kusini dhidi ya URA ya Uganda, hadi mwisho wa mchezo Orlando mabao ilitoka na ushindi wa 2-1. Nayo Vita klabu ya DR Congo iliiadhibu Ferrroviario Beira ya Msumbiji mabao 3-0.
CREDIT SOURCE: BBC
No comments:
Post a Comment