Mwandishi Wetu, BrotherDanny Blog
ARUSHA: ASASI ya Initiative for Youth (INFOY) ya jijini Arusha imeomba Serikali kushirikiana nayo kupiga vita tabia ya baadhi ya watu wazima kuoga katika mito kwani wanaoga katika mito wanaaaribu watoto wadogo ambao nao bado wanakuwa.
Mbali na watu wazima kuoga katika mito mbalimbali ya jiji la Arusha hasa wanaume lakini pia asasi hiyo imesema kuwa kwa upande wa wanawake wanatakiwa nao kuachana na tabia ya kuoga pamoja na watoto wao.
Akizungumza mapema janana wazazi pamoja na walezi wa watoto wa kata ya daraja mbili mratibu wa asasi hiyo Laurent Sabuni alisema kuwa inasikitisha kuona kuwa pamoja na kuwa serikali inapinga na kukataza unyanyasaji wa watoto lakini wamesahau kuwa hata kuonesha maumbile kwa watoto ni kuwanyanyasa.
Alisema kuwa wale wanaoga katika mito mbalimbali bado hawafanyi vizuri kwani wanaijengea jamii taswira ambayo si nzuri hasa kwa watoto ambao wanawashuhudia wakioga kwenye mito hivyo kuna haja ya serikali kuwakata wanaume kuoga katika mito hasa Mto Themi.
Alisema kuwa wale wanaoga katika mito mbalimbali bado hawafanyi vizuri kwani wanaijengea jamii taswira ambayo si nzuri hasa kwa watoto ambao wana washuhudia wakioga kwenye mito hivyo kuna haja yaserikali kuwakataza.
lakini pia alisema mbali na wanaume wengi kuonekana wakiwa wanaoga katika mito hata kwa upande wa wanawake nao wanatakiwa kujua na kutambua kuwa hawapaswi kuoga na watoto wao hata kama ni wadogo.
Sabuni alisema waki mama ambao wanaoga pamoja na watoto wao huwa hawawajengei picha nzuri kwani hiyo ndiyo sababu mojawapo ambayo wakati mwingine insababisha watoto kufanya au kuharibu maadili huku utandawazi nao ukisingiziwa.
"sasa tunatakiwa kuamka na kisha kujijenga vizuri tujiulize wale wanaoga katika mito mfano wa mto themi je ni watoto wangapi wanaagalia na je ni haki kweli wanavyofanya watoto wanajifunza nini na kwa upande wa kina mama inakuwaje unaoga na mtoto wako au unamruhusu msichana wa kazi kuoga na mtoto wako kwa kweli hii sio nzuri hata kidogo tujirekebishe kwa kweli" aliongeza Sabuni.
Pia aliiomba serikali kuweza kuwasaidia kupiga vita tabia hiyo kwani mbali na kuwaharibu watoto lakini ni uharibifu wa mazingira kwani mito mingi inategemewa na wananchi walio nje ya miji kwa matumizi mbalimbali ya kila siku ikiwemo unyeshehaji wa mazao.
nao wazazi walisema kuwa suala zima la maadili na haki za mtoto linapswa kutekelezwa na wana ndoa wote wawili na wala sio mwana ndoa mmoja kwani bado jamii ina dhana potofu kuwa zoezi la kuwalea watoto ni la mwanamke pekee.
No comments:
Post a Comment