Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk. John Pombe Magufuli akiwapungia mikono wananchi ikiwa ni ishara ya kuwasalimia alipowasili kwenye mkutano wa kampeni mjini Mbinga, Mkoa wa Ruvuma leo, ambapo aliahidi kuboresha kiwanda cha kukoboa kahawa na kujenga barabara ya lami kutoka Mbinga hadi Mbamba bay.
Twitter Buzz
....
...
IMETOSHA!
Featured post
KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO
Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...
Monday, 31 August 2015
MAOFISA WA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI WATEMBELEA KIWANDA CHA TBL DAR
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kanda ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Peter Sima na baadhi ya askari wa kikosi hicho wakimsikiliza kwa makini mtaalamu wa kusindika bia wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Emanuel Sawe (kushoto), walipotembea kiwanda hicho, Dar es Salaam kushiriki semina fupi ya wiki ya nenda kwa usalama na TBL.
TANZANIANS URGED TO OBSERVE PEACE TOWARDS GENERAL ELECTIONS
Ms Martha Nghambi, the Country Director for Global Peace Foundation Tanzania (GPFTZ), addressing a press conference in Dar es Salaam during the official launch of the peaceful awareness national campaign named “Amani Kwanza” on Monday, August 31, 2015. On the right is Reverend Thomas Ngoda, Director for the Inter Religious Council for Peace in Tanzania (IRCPT) and left is GPFTZ Administration Officer, Ms Hilda Ngaja.
GLOBAL PEACE FOUNDATION, TAWI LA TANZANIA KUHAMASISHA AMANI NCHINI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Global Peace Foundation Tawi la Tanzania (GPFTZ), Martha Nghambi (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha amani nchini Tanzania katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu. Kulia ni Mkurugenzi wa Baraza la Taasisi ya Viongozi wa Dini Tanzania (IRCPT), Mchungaji Thomas Goda na kushoto ni Ofisa Utawala wa GPFTZ, Hilda Ngaja.
STARS YAMALIZA KAMBI UTURUKI
Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro chini ya Kocha wake Mkuu Charles Boniface Mkwasa imefanya mazoezi yake ya mwisho leo asubuhi katika viwanja vya hoteli ya Green Park Kartepe – Kocaeli nchini Uturuki.
HALMASHAURI NZEGA YAJIPANGA KUTOA HUDUMA BORA YA MAJI
Mhandisi wa maji Halmasauri ya wilaya ya Nzega mkoani Tabora Mariam Majala akitoa ufafanuzi. Picha na Hastin Liumba.
Na Hastin Liumba, NzegaSERIKALI ya Tanzania ahadi yake kubwa siku zote inatekelezwa chini ya Ilani ni pamoja na suala zima la upatikanaji wa huduma za msingi kwenye maisha ya kila Mtanzania.
MGOMBEA UBUNGE MOSHI MJINI KUPITIA CHADEMA NA UKAWA AZINDUA KAMPENI ZAKE.
OLE KWA WATANZANIA, SHERIA YA MAKOSA YA MITANDAO KUWAFUNGA WENGI
Maxence Mello, Mkurugenzi wa kampuni ya Jamii Media wamiliki wa JamiiForums na Fikra Pevu, akifafanua madhara ya Sheria ya Makosa ya Mtandao kwa wahariri na waendhsa blogu (blogger) wakati wa warsha ya siku moja iliyofanyika kwenye Hoteli ya Kebbys, Mwenge jijini Dar es Salaam Agosti 27, 2015. (Picha na Daniel Mbega).
LOWASSA ASEMA, TUKISHINDWA SASA BASI TENA!
Mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa akimnadi mgombea ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa kwenye mkutano uliofanyika Uwanja wa Sabasaba jana. Picha na Edwin Mjwahuzi
Na Fidelis Butahe na Edwin Mjwahuzi, Mwananchi
Iringa. Mgombea urais wa Chadema anayeungwa mkono na vyama vinavyounda Ukawa, Edward Lowassa amesema kama Watanzania watashindwa kufanya mabadiliko kwa kupiga kura kuing’oa CCM madarakani mwaka huu, hawataweza kufanya hivyo tena, huku akihoji kama vyama tawala mbalimbali katika nchi za bara la Afrika vimeng’oka madarakani: “Kwa nini isiwe CCM”.
UN YAFANYA USAFI SOKO LA TEMEKE STEREO KUADHIMISHA MIAKA 70
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema (katikati) kabla ya kuanza zoezi la usafi katika soko la Temeke Stereo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
WHO YATOA DAWA ZA MILIONI 42.2 KUPAMBANA NA KIPINDUPINDU NCHINI
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Donan Mmbando (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam mwishoni mwa wiki wakati akipokea msaada huo kutoka WHO. Kulia ni Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Nchini Dk. Rufaro Chatora.
FILIKUNJOMBE APINGWA KUPITA BILA KUPINGWA LUDEWA
Mgombea Ubunge Jimbo la Ludewa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Msambichaka Mkinga (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, wakati akipinga kupitishwa bila kupingwa mgombea mwenzake wa jimbo hilo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Deo Filikunjombe na kudai kulikuwa na hujuma. Kulia ni Wakili wake, Paulo Kalomo.
UZINDUZI WA TAMASHA LA KUOMBEA AMANI TAIFA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU KUFANYIKA OKTOBA 4, 2015 UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion, waandaaji wa matamasha mbalimbali kama lile la Krismas na Pasaka, Alex Msama (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam juzi kuhusu uzinduzi wa Tamasha la kuliombea Taifa kuelekea ucahguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu utakaofanyika Oktoba 4, 2015 Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
COUNTIES CAN’T RUN HOSPITALS, SAYS ATWOLI
The Central Organisation of Trade Unions (Cotu) has supported calls to have health services reverted to the National Government.
WOMEN ARE 'LIVING FOUR YEARS LONGER THAN MEN'
By EUNICE KILONZO
Women in Kenya are enjoying a higher life expectancy than men, living to an average of 67.5 years compared to 63 for men.
NIGERIA MABINGWA WA MPIRA WA KIKAPU AFRIKA
Timu ya taifa ya Nigeria ya mchezo wa kikapu imetwaa ubingwa wa mpira wa kikapu barani Afrika baada ya kuichapa Angola.
MARIA SHARAPOVA KUIKOSA US OPEN
Mcheza tenisi namba tatu kwa ubora duniani, Maria Sharapova
Nyota namba tatu wa mchezo wa Tenesi duniani kwa upande wa wanawake Maria Sharapova amejitoa kushirikia michuano US Open.
EU YAJIPANGA KUDHIBITI WAHAMIAJI
Wahamiaji wakiokolewa baharini wakati wakijaribu kwenda Ulaya
Jumuiya ya Ulaya EU imetangaza mkutano wa dharula wa Mawaziri wake wa Mambo ya nje wenye lengo la kujadili mbinu za kukabiliana na ongezeko la wahamiaji ambao unatarajiwa kufanyika ndani ya wiki mbili Septemba 14 mwaka huu.
GESI NYINGI YAGUNDULIWA MISRI
Kampuni ya mafuta ya Italia, Eni, inasema imegundua katika mwambao wa Misri, moja kati ya visima vikubwa kabisa duniani vya gesi.
Sunday, 30 August 2015
ACT-WAZALENDO YAZINDUA KAMPENI MBAGALA, DAR NA KUSEMA ZITTO KABWE KUWA WAZIRI MKUU
Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mghwira (kushoto), akihutubia katika uzinduzi wa kampeni ya chama hizo uliofanyika viwanja vya Zakhem Mbagala jijini Dar es Salaam leo. (Picha zote na Dotto Mwaibale wa habarizajamii.com).
HELIKOPTA YA NYALANDU YANOGESHA KAMPENI ZA CCM
Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu akiwa jukwaani akinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba.
MKWASA ASEMA STARS IPO KAMILI
Kocha Mkuu wa timu ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro, Charles Mkwasa amesema vijana wake wapo tayari kuwavaa Nigeria Septemba 5, 2015 katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za AFCON mwaka 2017.
CCM KUONDOA KODI ZA HOVYO, YAJA NA ELIMU YA BURE HADI KIDATO CHA NNE
Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu (hayupo pichani) akinadi Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Iramba Magharibi.
KESI YA TALAKA YA MMILIKI WA ST. MATHEW YAAHIRISHWA TENA
YA LOWASSA JANA NI BALAA
Mgombea urais kwa tiketi ya Chadema kupitia Ukawa, Mh Edward Lowassa akiongea na wakazi wa jiji la Dar waliojitokeza katika uzinduzi wa Kampeni za Ukawa katika viwanja vya Jangwani mapema jana. Mh Lowassa amesema kipaumbele chake kimoja wapo ni Elimu huku akisisitiza kuwa kampeni zao zitakuwa ni za busara na hekima bila kutumia matusi.
MAGUFULI AZIDI KUCHANJA MBUGA, AWATAKA WANANCHI WAWEKE IMANI KUBWA KWAKE NA KUMPA KURA NYINGI ZA USHINDI
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Njombe mjini katika mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika jioni ya leo katika uwanja wa saba saba. Magufuli amesema akichaguliwa kuwa rais wa awamu ya tano ataendeleza juhudi zake za kujenga barabara kwa kiwango cha lami,amesema dhamira yake aliokuwa nayo ya Uwaziri wa Ujenzi katika kujenga barabara za lami katika maeneo yote hapa nchini.
U-15, MORO KOMBAINI ZATOKA SARE
TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa 15 jana ililazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Moro Kids Uwanja wa Jamhuri, Morogoro katika mchezo wa kirafiki.
KARUMA MWENYEKITI MPYA WA TWFA
Uchaguzi wa Chama cha Mpira wa Miguu nchini (TWFA) umemalizika ambapo Amina Karuma amechaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa chama hicho, kufuatia uchaguzi uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
VIJANA WATANO U-15 WAELEKEA AFRIKA KUSINI
Wachezaji watano kutoka katika kikosi cha vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U-15) wameondoka jana jijini Dar es salaam kuelekea nchini Afrika Kusini katika klabu ya Orlando Pirates kwa ajili ya kufanya majaribio.
MAGUFULI AMJULIA HALI NA KUMPA POLE MEYA WA JIJI LA MBEYA MH ATHANAS KAPINGA BAADA YA KUPATA AJALI
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Ndugu John Pombe Magufuli akimjulia hali na kumpa pole aliyekuwa Meya wa jiji la Mbeya Mh.Athanas
Kapunga aliyepata ajali wilayani Momba mkoani Mbeya wakati wa mbio za
maandalizi ya Kampeni hivi karibuni,Mh Kapunga amelazwa kwenye chumba maalum cha wagonjwa mahututi
(ICU) katika hospitali ya Rufaa mjini humo.
KULALA MCHANA KUNAZUIA MSHTUKO WA MOYO
Uchunguzi unaonyesha kuwa kulala wakati wa mchana kunapunguza shinikizo la damu na pia kupunguza hatari ya kupatwa na mshutuko wa moyo pamoja na kiharusi.
KENYA MABINGWA WA RIADHA DUNIANI 2015
Ezekiel Kemboi
Kenya kwa mara ya kwanza kabisa imeibuka mshindi wa mashindano ya riadha ambayo yamekamilika mjini Beijing nchini China.
SHEREHE ZA KUCHAGUA MKE ZA KING MSWATI ZATAKIWA KUSITISHWA
Utawala wa kifalme nchini Swaziland unaongozwa na mfalme Mswati umetakiwa kufutilia mbali sherehe maarufu za kitamaduni baada ya wasichana kadha waliokuwa wakisafiri kwenda kwa sherehe hizo kufa kwenye ajali ya barabarani.
Saturday, 29 August 2015
TAZAMA TSUNAMI YA UKAWA JANGWANI NI BALAA
Shamsa Ford, Aunty Ezekiel, Jacq Wolper, Joyce Kiria na Halima Mdee
UNAKUMBUKA FRANCO ALIVYOMPIGIA KAMPENI MOBUTU MWAKA 1984?
Wimbo huu uliimbwa na L'Okanga La Ndju Pene Luambo Luanzo Makiadi almaarufu kama Franco mwaka 1984 akiwa anampigia rafiki yake kipenzi Joseph Mobutu, au Mobutu Seseseko Nkuku Ndegbu Wa Zabanga.
Hawa jamaa walikuwa marafiki wakubwa, ingawa kuna wakati walikuwa wakitofautiana.
Friday, 28 August 2015
WANAWAKE WAMLILIA MAJI MGOMBEA MWENZA WA CCM
Mgombea mwenza wa CCM nafasi ya urais, Bi. Samia Suluhu akiwasikiliza akinamama wakimuelezea kero ya maji baada ya kumsimamisha na kumpa kero hizo Jimboni Longido.
VILABU VYATAKIWA KUWASILISHA NAKALA YA MIKATABA TFF
Klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) zinatakiwa kuwasilisha mikataba ya wachezaji wake- nakala tatu kwa kila mchezaji kwa ajili ya kuidhinishwa na TFF, kama ilivyoelekezwa katika Kanuni ya 69(1) na (8).
MALINZI AIPONGEZA GEITA GOLD SC
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi ameipongeza klabu ya Geita Gold SC inayoshiriki ligi Daraja la Kwanza nchini (FDL) kwa kupata udhamini wa shilingi milioni mia tatu (USD 150,000) toka kampuni ya uchimbaji madini ya Geita Gold Mining LTD.
TWIGA KUFUNGA DIMBA NA IVORY COAST
Kikosi cha Twiga Stars
Timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) inayotarajiwa kuondoka nchini mwishoni mwa mwezi Agosti kuelekea nchini Congo-Brazzavile kwenye Fainali za Michezo ya Afrika (All Africa Games) imepangwa kufungua dimba na timu ya Wanawake ya Ivory Coast Septemba 6, 2105.
Subscribe to:
Posts (Atom)