Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 30 June 2015

WALIOMUUA ALBINO MWAKAJILA WA MBEYA LEO WAMEHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA


Hakimu Mwakalinga siku alipohukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa mauaji ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe. Leo amehukumiwa tena kunyongwa mpaka kufa katika mauaji ya mlemavu wa ngozi Henry Mwakajila.


Na Daniel Mbega
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Mbeya leo hii imewahukumu kunyongwa mpaka kufa watu wanne kati ya watano waliomuua Henry Mwakajila (17) ambaye ni mlemavu wa ngozi (albino).

U15 YAREJEA DAR KUTOKA MBEYA

Peter Manyika, kocha wa U15


Kikosi cha timu ya Taifa cha vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U-15) leo kinarejea jijini Dar es salaam kikitokea mkoani Mbeya ambapo jana kiliibuk ana ushindi wa ushindi wa mabao 4-1.

STARS KUWAFUATA UGANDA ALHAMISI

 Wachezaji wa Taifa Stars wakisikiliza maelekezo.
 Wachezaji wa Stars wakiwa mazoezini.
Makocha na viongozi wakiangalia mazoezi ya Stars.

Timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager inatarajiwa kuondoka nchini siku ya alhamis kuelekea nchini Uganda kwa ajili ya mchezo wa marudiano utakaofanyika siku ya jumamosi nchini humo.

FDL KUCHEZWA MAKUNDI MATATU 2015/2016


Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kwa msimu wa 2015/2016 itachezwa katika makundi matatu ya timu nane nane kwa mtindo wa nyumbani na ugenini.

TANZANIA YAPONGEZWA KWA KUPUNGUZA VIFO VYA WAJAWAZITO NA WATOTO

Mwakilishi kutoka Ofisi ya Katibu Mkuu wa Vizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Mushi (wa kwanza kulia) aliyemwakilishi Dk Donan Mmbando akizungumza na washiriki wa Mkutano unaojadili mchango wa haki za binadamu unavyoweza kuboresha huduma za afya kwa watoto na kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano (5) nchini Tanzania. Mkutano huo unafanyika jijini Dar es Salaam kwa siku mbili mfululizo. 
Mwakilishi kutoka Ofisi ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Mushi (wa kwanza kulia) aliyemwakilishi Dk Donan Mmbando akizungumza na washiriki wa Mkutano unaojadili mchango wa haki za binadamu unavyoweza kuboresha huduma za afya kwa watoto na kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano (5) nchini Tanzania. Mkutano huo unafanyika jijini Dar es Salaam kwa siku mbili mfululizo.

WAZIRI CHIKAWE AZINDUA KIKOSI KAZI CHA KUPAMBANA NA UHALIFU WA KIMAZINGIRA NCHINI

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akizungumza na viongozi wa wizara mbalimbali pamoja na Mashirika ya Kimataifa kabla ya kuzindua kikosi kazi cha kupambana  na uhalifu wa kimazingira nchini kitakachokabiliana na Uvuvi haramu, Uwindaji haramu, Uvunaji wa miti haramu pamoja na uchimbaji wa madini haramu. Kikosi kazi hicho kimeundwa kwa kushirikisha Wizara za Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara Maliasili na Utalii, Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi na Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira). Tukio la uzinduzi huo lilifanyika katika Hoteli ya Hyatt, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

MAABARA YA MAFUNZO ITEMBEAYO YAZINDULIWA RASMI

DSC_0080
Mganga Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa jamiii, Dk. Magreth Mhando akisoma hotuba ya uzinduzi wa maabara itembeayo kwa ajili ya mafunzo ya upasuaji. Kulia ni Naibu Balozi wa Ireland nchini, Maire Matthews na kushoto ni Mkurugenzi wa ECSA anayeshughulikia Afya ya jamii Prof Yoswa Dambisya.

WAKUU WA IDARA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI WAMPA ZAWADI KATIBU MKUU WAO BAADA YA KUTUNIKIWA NISHANI YA UTUMISHI MREFU NA MAADILI MEMA DARAJA LA (I)


 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (kulia) akimkabidhi zawadi ya Ngao ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil, kwa niaba ya Wakuu wa Idara na Vitengo wizarani humo. Zawadi hiyo ya kushtukiza iliandaliwa na viongozi hao wa Idara baada ya hivi karibuni Rais Jakaya Kikwete kumvisha Nishani ya Utumishi Mrefu na Maadili Mema Daraja la (I), Katibu Mkuu wao katika tukio lililofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa wizara hiyo, Lilian Mapfa. Picha zote  na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

BALOZI WA NORWAY NCHINI AMTEMBELEA WAZIRI CHIKAWE OFISINI KWAKE, JIJINI DAR ES SALAAM LEO


 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akizungumza na Balozi wa Norway nchini, Hanne-Marie Kaarstad masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Norway na Tanzania. Mazungumzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Waziri Chikawe, jijini Dar es Salaam leo.  Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

WADAU WA MODEWJI BLOG WAJUMUIKA KUSHEREHEKEA MIAKA 7 YA MTANDAO HUO NDANI YA VIWANJA VYA SABA SABA

IMG_5219
Mdau wa modewjiblog, Ray the hustler (kushoto) aliyeambatana na ndugu zake kutembelea banda la Modewjiblog katika picha ya pamoja na Mwandishi wa habari mwandamizi wa mtandao wa Modewjiblog, Andrew Chale.

MO ASSURANCE YAJIPANGA KUTOA HUDUMA BORA KWA WATANZANIA MAONYESHO YA SABASABA

IMG_5136
Meneja mwendeshaji wa Kampuni ya bima ya MO (MO ASSURANCE), Ravinshankar Venkatrama ( wa pili kushoto) akiwa na timu ya wafanyakazi wa kampuni hiyo watakaokua wanatoa huduma katika Banda la MO ASSURANCE lilipo ndani ya mabanda ya MeTL Group kwenye maonyesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam yaliyoanza kurindima jana kwenye mabanda ya Sabasaba katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Afisa wa kampuni ya MO ASSURANCE, Mariot Ndomba, Ofisa Mtendaji Masoko wa Kampuni ya bima ya MO (MO ASSURANCE), Tawheeda Isaack pamoja na Meneja masoko msaidizi wa kampuni ya MO ASSURANCE, Esther Moringi.

KONGAMANO LA SDG’s LAFANYIKA KWA MAFANIKIO DODOMA

IMG_4628
Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Taasisi Huru ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida, akitoa maelezo ya kongamano kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kulifungua kongamano kubwa la siku mbili la kujadili namna taifa linavyojiandaa kutekeleza malengo mapya ya Maendeleo endelevu (SDGs) limefanyika mwishoni mwa wiki mjini Dodoma ambalo liliandaliwa na taasisi yake.

NJOO SABASABA UJUE UMOJA WA MATAIFA, MIAKA 70 YA KUTETEA USTAWI WA DUNIA

DSC_0598
Muonekano wa nje wa Banda la Shirika la Umoja wa Mataifa (UN), Tanzania lililopo ndani ya Karume Hall wanaoshiriki katika Maonesho ya 39 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam ya sabasaba yaliyoanza kurindima jana kwenye katika viwanja vya Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya Kilwa, jijini Dar.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).

Sunday 28 June 2015

11 WAUAWA KWENYE MAPIGANO MAKALI MALI


Takriban watu 11 wameuawa magharibi mwa Mali wakati wa mapigano kati ya wapiganaji wa kiislamu na jeshi.

BLATTER ASEMA, HAKUJIUZULU KAMA RAIS WA FIFA!

Sepp Blatter
Rais wa shirikisho la soka duniani Sepp Blatter amekariri kuwa hakujiuzulu kama rais wa shirikisho hilo.

ZAIDI YA WATU 500 WAJERUHIWA KWA MOTO TAIWAN


Zaidi ya watu 500 wamejeruhiwa kufuatia kutokea kwa mlipuko na moto kwenye bustani moja ya burudani nchini Taiwan.

HATARI: WANAWAKE WAJITOA MUHANGA NIGERIA, WAUA WATATU


Wanawake wawili washambuliaji wa kujitoa muhanga wamewaua takriban watu watatu kwenye shambulizi katika mji wa Maiduguri ulio kaskazini mashariki mwa Nigeria.

RAIS KIKWETE AWAVISHA VYEO VYA MRAKIBU MSAIDIZI WAHITIMU 104 WA JESHI LA MAGEREZA, JIJINI DAR ES SALAAM

Displaying PIX 1.JPG
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini (CGP), John Minja akimkarisha Rais Jakaya Kikwete (kushoto) katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kufunga mafunzo ya uofisa wa Cheo cha Mrakibu Msaidizi wa Jeshi hilo. Maafisa 104 wa kozi hiyo walihitimu mafunzo hayo na kuvishwa vyeo hivyo. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

WATU 15 KATI YA WALIOUAWA TUNISIA NI WAINGEREZA


Maelfu ya watalii wanaondoka Tunisia baada ya shambulio katika hoteli ya watalii iliyosababisha vifo vya watu 38 wengi wao wazungu.

UGIRIKI YAIDHINISHA KURA YA MAONI


Bunge la Ugiriki limeidhinisha kura ya maoni iliyokuwa imetishwa na waziri mkuu wa nchi hiyo Alexis Tsipras kuhusu mpango wa kuisaidia kiuchumi nchi hiyo uliopendekezwa na wakopeshaji wake.

SIMBA WAREJEA RWANDA BAADA YA MIAKA 20


Mfalme wa mwituni Simba, atarejea Rwanda kwa mara ya kwanza tangu aangamie wakati wa mauaji ya kimbari mwaka wa 1994.

KENYATTA ASEMA AL SHABAAB INAISHIWA NGUVU

Rais Kenyatta huku amevaa sare ya jeshi
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amelaani siasa kali za baadhi ya Waislamu Afrika Mashariki.

MAMBO YAMEIVA: UCHAGUZI KUFANYIKA KESHO JUMATATU BURUNDI

Balozi wa Burundi katika Umoja wa Mataifa amesema uchaguzi utafanyika Jumatatu.
Balozi wa Burundi kwenye umoja wa mataifa amesema kuwa uchaguzi utaendelea jinsi ulivyopangwa siku ya Jumatatu licha ya ombi kutaka uahirishwe kutoka kwa katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki moon.

Saturday 27 June 2015

ZUKU OPENS ANOTHER SHOP IN DAR

                                                                           
Dar es Salaam,  June 24, 2015. Zuku Company that deals in selling decoders in the country has launched another shop at Victoria in Kinondoni District, Dar es Salaam.

KINANA ASABABISHA WAPINZANI LUKUKI KUHAMIA CCM MAGU

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipokea kadi za vyma vya upinzani kutoka kwa watu waliovihama vyama hivyo na kujiunga na CCM, katika mkutano wa hadhara akatika Mji wa Kisesa, wilayani Magu, mkoani Mwanza leo,wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi pamoja na kusikiliza  kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.Kushoto ni Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Miraji Mtaturu. Zaidi ya wapinzani 50 walijiunga papo hapo.

Friday 26 June 2015

WAPINZANI BURUNDI KUSUSIA UCHAGUZI

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon ameitaka Burundi kusitisha uchaguzi.
Nchini Burundi hali ya kisiasa inaendelea kutokota, huku vyama vya upinzani vikitangaza kususia uchaguzi mkuu unaotarajiwa kuanza wiki ijayo.

WATU 27 WAUAWA HOTELINI TUNISIA


Watu wenye silaha wameshambulia hoteli moja ya kitalii iliyoko kwenye pwani ya Tunisia na kuwauwa watu 27.

NAPE AMALIZA MGOGORO UHURU


 Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Siasa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (kushoto), akiagana na wafanyakazi wa kampuni ya Uhuru Publications Ltd (UPL), inayochapicha magazeti ya Uhuru na Mzalendo waliofika kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM jijini Dar es Salaam jana, kwa ajili ya mazungumzo naye na baadae kupata muafaka kufuatia mgogoro uliokuwa ukifukuta katika kampuni hiyo.

WANAFUNZI FEZA SCHOOLS WASHINDA KIMATAIFA 'GENIUS OLYMPIAD'

Mwanafunzi wa Shule ya Kimataifa ya Fedha mwaka 11, Khalfan Kikwete (kulia) ambaye alishinda medali ya dhahabu pamoja na mwenzake Seif Yahya Mhata wakizungumza na waandishi wa habari. Mwanafunzi wa Shule ya Kimataifa ya Fedha mwaka 11, Khalfan Kikwete (kulia) ambaye alishinda medali ya dhahabu pamoja na mwenzake Seif Yahya Mhata wakizungumza na waandishi wa habari.

VILABU VPL VYATAKIWA KUWASLISHA MAJINA YA MAKOCHA WA MAKIPA


Shirikisho la Mpira wa Mpira wa Miguu nchini (TFF) linaviomba vilabu vyote vinavyoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom kuwasilisha jina la kocha wa magolikipa kufikia jumatatu ya tarehe 29 Juni, 2015 katika ofisi za TFF.

SITA ZAPANDA DARAJA KUCHEZA SDL


Abajalo FC ya Tabora, Alliance FC (Mwanza), Changanyikeni Rangers FC (Dar es Salaam), Coca-Cola Kwanza FC (Mbeya), Madini SC (Arusha), na Sabasaba United FC (Morogoro) ndizo timu zilizopanda kucheza Ligi Daraja la Pili (SDL) msimu wa 2015/2016.

TFF YAVIAGIZA VYAMA VYA MKOA KUWA NA VITUO VYA MPIRA WA MIGUU


Kufuatia pendekezo la sekretariet ya TFF ambalo baadae lilipitishwa na Mkutano Mkuu wa TFF kila mkoa unatakiwa kuwa na kituo chake cha kulea na kukuza vipaji vya mpira wa vijana umri kuanzia miaka 8-17. 

STARS YAANZA MAZOEZI


Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kinachodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager kimeanza mazoezi leo asubuhi katika uwanja wa Boko Veterani kujiandaa na mchezo wa marudaino kuwania kufuzu kwa CHAN dhidi ya uganda mwishoni mwa wiki ijayo.

TFF YAFUNGUA KOZI YA MAKOCHA WA VIJANA


Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) leo limefungua kozi ya makocha wa mpira wa miguu kwa watoto na vijana kwa nchi nzima kwa lengo la kuhakikisha vijana wengi wanapata nafasi ya kufundishwa mpira na kuucheza mpira kuanzia katika umri mdogo.

MAUAJI MARIKANA: WAPINZANI AFRIKA KUSINI WATAKA MKUU WA POLISI AFUTWE KAZI


Upinzani nchini Afrika Kusini unaitaka serikali imfute kazi mkuu wa polisi Riah Phiyega baada ya tume maalum ya uchunguzi wa mauaji ya wachimba mgodi wa Marikana 2012 kuwalaumu kwa kusababisha vifo hivyo.

VUNA MBEGU ZA KIUME MKIFIKISHA MIAKA 18!


Mbegu za uzazi wa wanaume zinapaswa kuvunwa na kuhifadhiwa pindi mtu anapotimiza umri wa miaka 18.

WAERITREA WAANDAMANA KUPINGA UTAWALA WA UDHALIMU

Rais Isaias Afeworki
Mamia ya wakimbizi wa Eritrea wanaoishi nchini Ethiopia wameandamana mbele ya majengo ya muungano wa afrika AU wakiitaka muungano huo kuchukua hatua zaidi kumaliza ukiukaji wa haki za kibinadamu nchini mwao.

SAFARI YA CHIFU MKALA FUNDIKIRA

Gari lenye namba za usajili T 607 CVL likiwa limeegeshwa pembezoni mwa barabara baada ya kuharibika

Leo hii asubuhi nikitokea Singida kwenda Dar kwa basi la Shabiby Line, lenye nambari za usajili T607 CVL iliondoka stendi ya Misuna Singida mnaomo saa 12.48 (moja kasoro 12) za asubuhi. 

TANZANITE YAINGIA KAMBINI


Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya Wanawake wenye umri chini ya miaka 20 (U-20) Tanzanite Stars, imeingia kambini jana jioni Mbande jijini Dar es salaam na itakua ikifanya mazoezi katika uwanja wa Azam Complex.

U15 YAENDA MBEYA


Kikosi cha timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U-15) leo Ijumaa kimesafiri kuelekea jijini Mbeya kwa ajili ya mchezo wa kirafiki na timu kombani ya mbeya U15.

VILABU VYA SOKA VYATAKIWA KUWALIPIA KODI WALIMU NA WACHEZAJI


Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeviagiza vilabu vinavyoshiriki Ligi kuu ya nchini (mpira wa kulipwa) Tanzania, kuhakikisha kuwa wanalipa kodi kutokana na kuajiri makocha na wachezaji kutoka ndani na nje ya nchi.

WAKULIMA TUMBAKU UYUI.WAINGIWA HOFU YA MASOKO



Na Hastin Liumba, UyuiWAKULIMA wa zao la tumbaku wilaya ya Uyui mkoani Tabora wako katika hali ya sintofahamu baada ya kukosa masoko ya kueleweka ya wanunuzi wa tumbaku.

WANANCHI UYUI WALIA NA MBUNGE WAO

Dk. Athumani Mfutakamba, Mbunge wa Uyui
Na Hastin Liumba, UyuiWAKAZI wa kata ya Loya wilaya ya Uyui mkoani Tabora wamemlalamikia mbunge wao Dk. Athumani Mfutakamba kwa kutowatembelea tangu walipomchagua.

VICKY KAMATA AUKUBALI MUZIKI WA KINANA GEITA

TANGAZO LA MSIBA TANZANIA NA MAREKANI

DR. ALI MZIGE wa Mikocheni, Dar es salaam anasikitika kutangaza kifo cha Dada yake MRS MARIAMU -MWAJUMA MUSISA (NEE MZIGE) kilichotokea Raleigh, North Carolina Marekani tarehe 21-06-2015. Mwili wa marehemu utaletwa Tanzania kwa ajili ya mazishi.

KINANA ALAKIWA KWA SHAMRA SHAMRA ZA SUNGUSUNGU JIMBO LA KWIMBA


 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akilakiwa na Kikundi cha Ulinzi wa Jadi cha Sungusungu, alipowasili  katika Kijiji cha Hungumalwa njaia panda ya Mwamashinga alipoanza ziara Jimbo la Kwimba, mkoani Mwanza, ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi pamoja na kusikiliza  kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

MKWASA AITA 26 TAIFA STARS

Displaying Kocha Mkwasa (kushoto) na msaidizi wake Hemed Morocco wakiongea na waandishi wa habari.jpg

Kocha Mkwasa (kushoto) na msaidizi wake Hemed Morocco wakiongea na waandishi wa habari

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine leo amemtambuisha kocha mpya wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Charles Boniface Mkwasa mbele ya waandishi wa habari.

MAYANJA ATUA COASTAL UNION, ASAINI MIAKA MIWILI KUIFUNDISHA COASTAL UNION

Displaying DSC04398.JPG
Katibu Mkuu wa Coastal Union,Kassim El Siagi akipokea mkataba wa Kocha Mkuu mpya wa timu hiyo,Jackson Mayanja mara baada ya kuusaini leo ambapo amesaini mkataba wa miaka miwili kuifundisha  timu hiyo,katika Halfa iliyofanyika mjini hapa,Picha kwa Hisani ya Coastal Union.

WAKAZI IGALULA WADAI HAWANA BARABARA

Ujenzi wa barabara mkoani Tabora

Na Hastin Liumba, Uyui 
WAKAZI wa baadhi ya vitongoji na vijiji vya jimbo la Igalula wilayani Tabora ,Uyui mkoani Tabora wamedai maeneo yao yanakabiliwa na ukosefu wa barabara za uhakika hali ambayo inasababisha kukwama kufikiwa kwa maendeleo.