Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday 25 October 2016

WAFANYAKAZI WA NMB,TAWI LA NELSON MANDELA WATOA MSAADA NA ZAWADI KWA WAGONJWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA KILIMANJARO,MAWENZI.

Kaimu Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Kilimanjaro,Mawenzi Dkt Josephat Boniface akitoa maelzo mafupi kwa wafanyakazi wa Benki ya NMB tawi la Nelson Mandela waliofika hosptalini hapo kwa ajili ya kutoa zawadi kwa wagonjwa pamoja na msada wa vitendea kazi vya kufanyia usafi kwa hospitali ya Mawenzi.

UN YAADHIMISHA MIAKA 71, YAAHIDI KUWEZESHA VIJANA

Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (wa tatu kulia) akiwasili kwenye viwanja vya Karimjee akiwa ameambatana na mwenyeji wake Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa pili kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Celestine Mushy (kushoto) kwenye sherehe ya kupandisha bendera ya Umoja wa Mataifa katika kuadhimisha miaka 71 ya umoja huo ambapo kila mwaka Oktoba 24 huadhimishwa.(Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog)

MATUKIO MBALIMBALI UFUNGUZI WA MKUTANO WA KIUCHUMI WA KOREA NA AFRIKA MJINI SEOUL, KOREA KUSINI

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.  Dkt. Philip Mpango (Mb), akipokea zawadi ya kitabu kinachoelezea njia zilizotumiwa na nchi ya Korea Kusini, kupiha hatua kubwa ya maendeleo, kutoka kwa Afisa Mikopo wa Benki ya Exim ya Korea Kusini, Park Gil Jong, kabla ya kuhudhuria ufunguzi wa mkutano wa tano wa ushirikiano wa Korea Kusini na nchi za Afrika  (KOAFEC), Mjini Seoul, Korea Kusini.

ASILIMIA 90 YA MAONI YA WADAU YAMEJUMUISHWA KWENYE MUSWADA WA HABARI


Na Georgina Misama-MAELEZO
Serikali imesema asilimia 90 ya maoni yaliyotolewa na wadau mbalimbali wa sekta ya habari nchini yanaohusu Muswada wa Huduma ya Habari wa mwaka 2016 yamechukuliwa na kujumuishwa kwenye muswada huo.

SERIKALI YAKABIDHI HATI ZA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI NYAKATO

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Bunge), Dkt. Hamisi Mwinyimvua akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya MOIL, Sharif Mansoor , hati za ujenzi wa shule ya sekondari ya Nyakato,  kutokana na hiyo na  makumpuni ya mafuta mengine ya OILCOM na GBP waliahidi kuijenga shule hiyo iliyobomoka kutokana na tetemeko la ardh mkoani Kagera, Septemba, 2016, makabidhiano hayo yamefanyika tarehe, 23 Oktoba jijini Dar es salaam.

WATANGAZAJI WA LAKE FM MWANZA KUTAMBULISHWA KWA WANANZENGO KWENYE USIKU WA MSHIKE MSHIKE NA KHADIJA KOPA

Usisahau kuhusu Show ya Usiku wa Mshike Mshike na Mfalme wa taarabu Afrka Mashariki na Kati iliyoandaliwa na 102.5 Lake Fm Mwanza.

RAIS DKT MAGUFULI AMKARIBISHA MFALME MOHAMED VI WA MOROCCO IKULU JIJINI DAR ES SALAAM, MIKATABA 21 YA USHIRIKIANO YASAINIWA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Mtukufu Mfalme wa Morocco Mohamed VI wakilakiwa na wafanyakazi pamoja na wageni mbalimbali katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili.

MKURUGENZI WA JIJI LA MWANZA ASHIKILIA MSIMAMO WAKE DHIDI YA WATENDAJI WA SERIKALI ZA MITAA

Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba, akihojiwa na Waandishi wa Habari Jijini Mwanza, kuhusiana na sakata la Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Jijini Mwanza kugoma kukabidhi mihuri yao ya utendaji kazi.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AMEKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA ITALIA NCHINI


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Italia nchini Mhe. Roberto Mengoni (kushoto) ,Ikulu jijini Dar es Salaam.

AJALI ZA BARABARANI ZAENDELEA KUUA NA KUACHA MAJERUHI MKOANI MWANZA.

Baada ya Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani kufanyika Kitaifa mkoani Geita kuanzia Septemba 29 hadi Oktoba Mosi Mwaka huu, Maadhimisho kama hayo kwa mkoa wa Mwanza yamezinduliwa hii leo kwenye Uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza ambapo imeelezwa kwamba bado juhudi za kila mtumiaji wa barabara zinahitajika ili kutokomeza ajali za barabarani.

TIGO YAKABIDHI KISIMA CHA MAJI WILAYA YA USHETU

Mkurugenzi wa Mtandao wa Tigo kwa kanda ya Ziwa Ali Maswanya( fulana ya Blue) akimkabidhi kisima cha maji Mwenyekiti wa kijiji cha Ulowa 4 Hamad Mohamed kisima cha maji kilichojengwa na mtandao huo,wilayani Ushetu Mkoani Shinyanga.Kina thamani ya shilingi milioni16 /-.

MPAMBANO WA ISHA MASHAUZI, MALKIA LEYLA ULIKUWA ‘BALAA’!

dar-live1
Kabla ya mpambano Abubakari Soud ‘Amigo’ wa Jahazi alipanda jukwaani kuwanogesha mashabiki.

WILAYA YA HAI WAZINDUA KAMPENI YA KUCHANGISHA FEDHA KWA AJILI YA UJENZI WA MADARSA KWA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Said Mecky Sadiki akishiriki katika uchimbaji wa msingi kwa ajili ya ujenzi wa madarasa matatu katika shule ya msingi Msamadi ,uchimbaji ulioenda sanjari na uzinduzi rasmi wa kampeni ya kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika wilaya ya Hai.

CHAWABATA CHAIOMBA SERIKALI KURUDISHA MUDA WA ZAMANI WA KUFUNGUA BAA NCHINI

Mwenyekiti wa Chama cha Wahudumu wa Baa Tanzania (Chawabata), Ali Hussein (kulia), akizungumza na  waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa ombi kwa serikali la kuomba kufunguliwa baa muda wote ili kunusuru biashara hiyo. Kushoto ni Katibu wa chama hicho, Boniface Lameck. 

Sunday 23 October 2016

PROF. OLE GABRIEL AHIMIZA VIJANA KUFANYA KAZI KUCHANGIA UCHUMI WA TAIFA

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akifungua kongamano la vijana kutoka shule na vyuo mbalimbali nchini Oktoba 18, 2016 jijini Dar es salaam wakati wa wiki ya maadhimisho ya Umoja wa Mataifa unaofikisha miaka 71 tangu kuasisiwa kwake. Maadhimisho ya hayo yanaongozwa na kaulimbiu kwa upande wa Tanzania inayosema “Jukumu la Vijana wa Tanzania katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii”.

KAMPENI YA KUPIGA VITA NDOA NA MIMBA ZA UTOTONI YA BINTI WA KITAA YAFANYIKA TABATA JIJINI DAR

Bibi Pili Abdallah akielezea kwa kina maisha ya Mabinti wadogo yanayowapelekea kupata Mimba za utotoni na kuolewa wakiwa wadogo, pia alizungumzia Tamaa na Matamanio yalivyo na nguvu ya kuwafanya watoto wakike kujiingiza katika maswala ya ngono wakiwa wadogo na kupelekea kupata mimba, mwisho aliwashauri wazazi wenzake kuwatambua watoto  wao.

MKUTANO WA KWANZA WA BIASHARA NA UWEKEZAJI BAINA YA TANZANIA NA MOROCCO


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye mkutano wa kwanza wa Wafanyabiashara wa Tanzania na Morocco utakaoainisha fursa za uwekezaji baina ya nchi hizo mbili uliofanyika kwenye Hotel ya Hyatt Regency.

SHAMBA LA MITI LUNGUZA WAZIPIGA JEKI SHULE ZA MSINGI MUHEZA WAKABIDHI MADAWATI 200

Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia akipokea madawati 200 kutoka kwa Meneja wa Shamba la Miti Lunguza, yaliyotolewa na wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) Abdallah Mchomvu katika halfa iliyofanyika leo

WAZIRI KAIRUKI AMALIZA ZIARA YA SIKU 2, KUWATEMBELEA, KUWASIKILIZA NA KUZUNGUMZA NA WANUFAIKA TASAF WA MANISPAA ZA KINONDONI NA TEMEKE JIJINI DAR ES SALAAM


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki, akipokewa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva, alipowasili Ofisi za mkuu huyo jana kwa ajili ya kuhitimisha ziara yake ya siku mbili kuwatembelea, kuwasikiliza na kuzungumza na wanufaika hao wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf ) wa Manispaa za Kinondoni na Temeke jijini Dar es Salaam. 

HUU NDIO MRADI MKUBWA WA UJENZI WA HOTELI YA KITALII KATIKA KIJIJI CHA MATEMWE, ZANZIBAR

Mmiliki wa Mradi wa Hoteli ya Kitalii katika eneo la Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja, Mkurugenzi wa Mradi huo Brain Thomson, akitowa maelezo kwa waandishi wa habari walipofika kutembelea mradi huo kujionea maendeleo ya matayarisho yake na kuwaonesha michoro ya picha za majengo ya Mradi huo mkubwa utakaokuwa na uwanja vya ndege. na kutengeneza visiwa kwa ajili ya wageni wanaofika katika Visiwa vya Zanzibar. 

HUDUMA YA MCHUNGAJI DANIEL KULOLA WA KANISA LA EAGT LUMALA MPYA JIJINI MWANZA YAFANA MKOANI DODOMA

Huduma ya injili iliyofanywa na mchungaji kiongozi wa Kanisa la "EAGT Lumala Mpya Internationa Church " lililopo Sabsaba Ilemela Jijini Mwanza, Dkt.Daniel Moses Kulola (pichani), mkoani Dodoma imekuwa ya kufana na watu wengi wameokoka na kubarikiwa.

PIKIPIKI YAZUA HOFU BAADA YA KUTELEKEZWA MWAKA MZIMA JIJINI DAR ES SALAAM, UKIIKARIBIA, UKIIGUSA INAJIWASHA POLISI WAGWAYA KUIPELEKA KITUONI

 Mwananchi akipita kwa kuikwepa pikipiki yenye namba za usajili T 684 CJZ aina ya Fokon iliyotelekezwa kwa zaidi ya mwaka mmoja katika Kituo cha waendesha bodaboda cha Maganga Veterinary Dar es Salaam.

Saturday 22 October 2016

MUUGUZI HOSPITAL YA WILAYA YA CHUNYA MBEYA ATIWA MBARONI KWA KUSABISHA KIFO CHA MTOTO MCHANGA

Mkuu wa Wilaya ya Chunya Rehema Madusa akizungumza na watumishi wa hospital ya Wilaya ya Chunya kufuatia tukio la mama mjamzito kifanyiwa vitendo vya unyanyasaji na mmoja wa watoa huduma hospitalini hapo hali iliyopelekea mtoto kupoteza maisha .

WANAHABARI WAPIGWA MSASA KUHUSU KINGATIBA YA MABUSHA, MATENDE, USUBI, KICHOCHO, TRAKOMA


 Ofisa Mradi wa Mpango wa Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele, Oscar Kaitaba akielezea umuhimu wa vyombo vya habari kuelimisha umma kujenga tabia ya  kutumia Kingatiba ya magonjwa ya kichocho, Minyoo ya Tumbo, Usubi Matende na Mabusha wakati wa Warsha iliyoshirikisha wanahabari, Dar es Salaam leo. Kampeni ya kuwapatia wananchi Tibakinga kwa wakazi takribani mil. 4 wa Jiji la Dar es Salaam itaanza Oktoba 25 waka huu. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA

Friday 21 October 2016

NAIBU WAZIRI MASAUNI AZINDUA KITUO KINACHOTOA HUDUMA ZA MAGARI

Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), Katibu wa baraza hilo ambae pia ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Mohamed Mpinga (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya maatairi ya Superdoll, Seif Seif (kulia) wakikata utepe jana kuashiria uzinduzi wa kituo cha kisasa kinachotoa huduma za magari upande wa matairi kilichopo maeneo ya Magomeni Usalama, Dar es Salaam. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

TOA MAONI, BORESHA MUSWAADA WA SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI

Na Mwandishi Wetu
Mwanadamu katika maumbile yake amejengeka katika falsafa ya kufafuta ukweli na kuupambanua na taarifa zinazokinzana na ukweli wa wenyewe wa jambo fulani. 

Katika kutafuta ukweli, wapo watakaoamini, wapo ambao watakuwa hawaamini na wapo ambao hawapo kwenye kuamini wala kutokuamini.

WANAFUNZI WALIOHITIMU DARASA LA SABA 1993 SHULE YA MSINGI NYAKATO JIJINI MWANZA WAIKUMBUKA SHULE YAO

Baadhi ya Wanafunzi waliohitimu darasa la saba mwaka 1993 (1987-1993) Shule ya Msingi Nyakato Jijini Mwanza (kushoto), wakimkabidhi Afisa Mtendaji wa Kata ya Muhandu ilipo shule hiyo, vifaa mbalimbali vya kurudufu taarifa ambavyo ni printa pamoja na kompyuta walivyovitoa kwa ajili ya shule yao hii leo. 

LIGI YA TAIFA YA WANAWAKE

Ligi ya Taifa na Wanawake itaanza Novemba 1, 2016 kama ilivyopangwa awali kwa kushirikisha timu 12 zilizopangwa kwenye makundi mawili yenye majina ya ‘A’ na ‘B’. Kila kundi lina timu sita.
Timu za kundi A lina timu za Viva Queens ya Mtwara, Fair Play ya Tanga, Mlandizi Queens ya Pwani pamoja na Mburahati Queens, Evergreen Queens na JKT Queens za Dar es Salaam wakati kundi B zimo Marsh Academy ya Mwanza, Baobab Queens ya Dodoma, Majengo Women ya Singida, Sisters FC ya Kigoma, Kagera Queens ya Kagera na Panama FC ya Iringa.

LIGI DARAJA LA KWANZA KUENDELEA KESHO

Na Alfred Lucas
Wakati mzunguko wa tano wa Ligi Daraja la Kwanza ukitarajiwa kuendelea kesho Jumamosi na keshokutwa Jumapili, Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeagiza makamishna na wakuu wa vituo kuzuia wachezaji wote ambao hawana leseni kutocheza.
Hii ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14 (16), inayosema: “Wachezaji wote watatambulika kwa kutumia leseni zao zitakazotolewa na kuidhinishwa na TFF. Mchezaji yoyote ambaye hatakuwa na leseni hataruhusiwa kucheza katika mchezo husika.”

LIGI KUU BARA: VIWANJA SITA KUTIKISWA KESHO, VIWILI JUMAPILI


Na Alfred Lucas
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu 2016/17, raundi ya 12 inaendelea keshokwa michezo sita ambako mabingwa watetezi Young Africans ya Dar es Salaam itakuwa mgeni wa Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba ulioko Bukoba mkoani Kagera.
Jijini Dar es Salaam, katika Uwanja wa Uhuru African Lyon itakuwa mwenyeji wa Mbeya City ya Mbeya ilihali Mwadui ya Shinyanga itasafiri hadi Mtwara kucheza na Ndanda Fc kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona wakati Stand United itakuwa mgeni wa Mtibwa Sugar ya Morogoro kwenye mchezo utaofanyika Uwanja wa Manungu, ulioko Turiani – Mvomero.

BENKI YA NMB MLIMANI CITY YATOA SEMINA FUPI KWA WATEJA WAKE KUHUSU HUDUMA WAZITOAZO

Wafanyakazi wa Benki ya NMB Tawi la Mlimani City wakijitambulisha kabla ya kuanza kwa semina hiyo.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AKUTANA NA BALOZI WA IRAN NCHINI ANAYEMALIZA MUDA WAKE


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Irani nchini Mhe.Mehdi Agha Jafari (kushoto)ambaye alifika ofisini kwa Makamu wa Rais,Ikulu jijini Dar es Salaam leo na kuaga baada ya muda wake wa kazi kumalizika nchini.

WANANCHI WABOMOLEWA NYUMBA 150 JIJINI DAR ES SALAAM, LEO KUTUA KWA MKUU WA WILAYA KUPELEKA KILIO CHAO

 Mkazi wa eneo hilo, Lukia Khalid (aliye kaa), akiwa amekaa nje na vyombo vyake baada ya kubolewa nyumba yake.

WAFANYABIASHARA PAMOJA NA WAKAZI WA JIJI LA MWANZA WATAKIWA KUITUMIA KAMPUNI YA MWANA KUIMARISHA ULINZI WAO

Kampuni ya Mwana (Mwana Company Ltd) ni Kampuni mpya inayojishughulisha na ufungaji wa vifaa vya ulinzi vya kisasa, lengo likiwa ni kuimarisha ulinzi katika maeneo ya biashara pamoja na makazi ya watu.

Thursday 20 October 2016

BARAZA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI LAKUTANA KUJADILI MAENDELEO YA MKAKATI WA KUPUNGUZA AJALI

Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani  ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wajumbe wa baraza hilo wakati wa kikao cha kujadili maendeleo ya Mkakati wa Kupunguza Ajali za Barabarani. Kulia ni Katibu Mtendaji wa baraza ambaye pia ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga.Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa wizara hiyo, Dar es Salaam. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

MCHUNGAJI WA KANISA LA EAGT MITO YA BARAKA JIJINI DAR ES SALAAM AHUDUMU KATIKA KANISA LA EAGT LUMALA MPYA JIJINI MWANZA.

Mchungaji  Bruno Mwakibolwa kutoka Kanisa la EAGT Mito ya Baraka Temeke Jijini Dar es salaam, jumapili iliyopita Oktoba 16, 2016 alihudumu katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya la Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza, baada ya kuwasili katika kanisa hilo akitokea nchini Kenya.

WASHINDI WA SHINDANO KUHUSU MASOKO YA MITAJI KWA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU NA TAASISI ZA ELIMU YA JUU WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO

Mgeni rasmi, naibu waziri wa fedha na mipango Mhe, dkt Ashatu kijaju akiwa na majaji katika hafla ya utoaji wa zawadi kwa washindi wa shindano kuhusu masoko ya mitaji kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu.

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AZINDUA KITABU KINACHOELEZEA MAHUSIANO NA URAFIKI WA TANZANIA NA USWISI


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akizungumza na Balozi  wa Uswisi nchini Tanzania Mhe. Florence Tinguely muda mfupi kabla ya kuzindua kitabu kiitwacho A-Concise Study of Contemporary Art kinachoelezea mahusiano na urafiki uliodumu baina ya nchi hizi mbili na watu wake,Ikulu jijini Dar es Salaam.

SIMBA CEMENT YAZIPIGA TAFU SHULE TATU TANGA KUPUNGUZA KERO YA MADAWATI




KUFUATIA Uhaba wa madawati katika shule za msingi halmashari ya jiji la Tanga na wanafunzi kusomea chini, Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement kimetoa madawati 100 kwa shule tatu.

SHULE YA SEKONDARI YA MALANGALI YAPATA NEEMA KUTOKA KWA MALANGALI ALUMNI ASSOCIATION (MAAS)


Hawa ndio baadhi ya wanafunzi waliowahi kusoma katika shule ya sekondari ya Malangali wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya  kuwasili katika shule hiyo na kukaangalia mazingira ya shule hiyo na kutafuta njia za kutatua baadhi ya changamoto kwa kushirikiana na serikali ya Jamhuri ya muungano ya Tanzania

MAADHIMISHO YA MIAKA 71 YA UMOJA WA MATAIFA YASISITIZA MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU

’Wito watolewa kwa kila mwananchi kuwajibika kwa malengo ya Dunia’

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. Mhe. Balozi Dkt. Mahiga, amezungumzia umuhimu wa maadhimisho wa Siku ya Umoja wa Mataifa na faida za Jukwaa la umoja huo kwa maendeleo ya Taifa. Maadhimisho hayo yatafikia kilele tarehe 24 Oktoba, 2016.(Picha zote na Reginald Kisaka wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki).

OKTOBA 24 kila mwaka Umoja wa Mataifa hufanya maadhimisho ya kuzaliwa kwake.

Mwaka huu mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania kwa kushirikiana na serikali, wadau wa maendeleo na vijana wataadhimisha miaka 71 ya uwapo wa Umoja wa Mataifa kwa staili ya aina yake.

LEYLA RASHID VS ISHA MASHAUZI JUMAMOSI HII …NI VITA YA “SURA SURAMBI” NA “NINA MOYO SIO JIWE”

 
NI vita ya “Sura Surambi” na “Nina Moyo Sio Jiwe”.  Ndiyo unavyoweza kusema kuelekea mpambano wa waimbaji nyota wa taarab malkia Leyla Rashid na Isha Mashauzi.

SHINDANO LA MISS TANZANIA 2016 JIJINI MWANZA KUWA BORA ZAIDI

Leo Oktoba 19, 2016 Kamati ya Shindano la Maandalizi ya Miss Tanzania 2016 imesema Shindano hilo linalotarajiwa kufanyika Oktoba 29,10, 2016 katika viunga vya Rock City Jijini Mwanza, litakuwa bora zaidi kutokana na maandalizi yaliyofanyika na yanayoendelea kufanyika.

MKUU WA WILAYA YA HAI ,GELASIUS BYAKANWA AMALIZA MGOGORO WA ARDHI, AREJESHA SHAMBA LA FOFO ESTATE KWA HALMASHAURI

Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi wa vijiji vinne vilivyoko kata ya Machame Narumu akitoa uamuzi juu ya mgogoro wa ardhi wa shamba la Fofo Estate.

MERCK KUTOA MSAADA WA TEMBE MILIONI 500 ZA PRAZIQUANTEL


PRESS RELEASE

Merck Kutoa Msaada wa Tembe Milioni 500 za Praziquantel

Kutoka Abidjan, Ivory Coast, Oktoba 19, 2016 –

·        Zaidi ya watu milioni 100, hususani watoto, wametibiwa ugonjwa wa kichocho tangu 2007
  • Kwa mara ya kwanza Merck kutoa takriban tembe milioni 10 kwa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Ivory Coast.

Merck (MerckGroup.com), kampuni kubwa ya sayansi na teknolojia, imetangaza leo kuwa imetoa msaada wa tembe milioni 500 za kutibu ugonjwa wa minyoo ya kichocho unaodhuru kwa siri kwa Shirika la Afya Duniani (WHO). Katika shule inayopatikana takriban kilomita 25 magharibi kaskazini mwa Abidjan, wawakilishi kutoka Merck, WHO na Wizara ya Afya ya Ivory Coast wametangaza kwa sauti moja uzinduzi wa usambazaji wa dawa hiyo nchini Ivory Coast.

MKOA WA SONGWE WAPIGWA JEKI MIFUKO 125 YA CEMENT KUTOKA TPB

Mkuu wa Mkoa wa Songwe (katikati)  Luteni Mstaafu Chiku Galawa akipokea msaada wa Cement mifuko 125 yenye thamani ya shilingi mil 2 kutoka kwa benki ya Posta Tanzania (TPB) tawi la Mbeya.kulia aliyevalia T.shart Meneja Benki ya Posta Mbeya Humphrey Julias ,kushoto Mkuu wa Wilaya ya Mbozi John Palingo na Meneja wa benki ya Posta tawi la Tunduma Teddy Msanzi aliyshikana mkono na Mkuu wa Mkoa wa Songwe.

SBL YATOA ELIMU KUHUSU UNYWAJI POMBE KISTAARABU

Meneja wa SBL wa  Uwajibikaji Katika  Jamii, Hawa Ladha  akitoa maelezo katizo kuhusu kampeni ya unywaji kistaarabu katika mkutano na wadau mbali mbali wakiwepo toka vyombo vya usalama na wafanyabiashara wanaofanya kazi na SBL na wafanyakazi wa kiwanda cha SBL moshi katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika mapema jana katika mji wa Moshi mkoani Kilimanjaro.

SERIKALI, MASHIRIKA YA KIMATAIFA YAWEKA MIKAKATI YA KUWASAIDIA NA KUWALINDA WATOTO WALIOATHIRIKA NA BIASHARA HARAMU YA USAFIRISHAJI WA BINADAMU NCHINI



 Katibu wa Sekretarieti ya Kitaifa ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Binadamu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Separatus Fella (wapili kulia-meza kuu), akitoa hotuba ya ufunguzi wa Warsha ya Siku mbili ya kujadili jinsi ya kuwalinda na kuwasaidia watoto walioathirika na biashara ya kusafirisha binadamu. Fella alisema wadau wa warsha hiyo watatoa elimu kwa umma jinsi ya kuwasaidia idadi kubwa ya watoto ambao wameathirika. Wapili kushoto meza kuu ni Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Ulaya (EU) upande wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla, Balozi Roeland Van de Geer. Kushoto ni Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) nchini, Dr Qasim Sufi, na kulia ni Mratibu wa Mradi wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM), Tamara Keating. Warsha hiyo inafanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

WASIIOONA WATAKIWA KUTOKATA TAMAA

 Mkuu wa Wilaya Temeke Mh. Felix Lyaniva (kulia) akiongea na Mkufunzi wa Mafunzo ya ushonaji kwa wasioona Bw. Abdallah Nyangalio wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo jijini Dar es Salaam. (Picha na Benjamin Sawe Maelezo).

Wednesday 19 October 2016

TAASISI YA ADLG YAANZA KUWANOA WANAHABARI JIJINI MWANZA KUHUSIANA NA SEKTA YA MADINI NCHINI

Baadhi ya wanahabari Jijini Mwanza, wakijadiliana wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kuandika habari zenye tija katika jamii kuhusiana na sekta ya madini nchini. 

MBUNGE VENNANCE MWAMOTO AGAWA VIFAA VYA MICHEZO KATIKA JIMBO LA KILOLO


 Mbunge wa jimbo la kilolo Vennance Mwamoto akikabidhi vifaa vya mchezo wa mpira wa miguu kwa wanamichezo wa kijiji cha Bomalang'ombe wakati wa mkutano wa hadhara ulifanyika katika kijiji hicho na kulia ni wachezaji wa timu ya kijiji cha Bomalang'ombe wakipokea jezi na mpira walizopewa na mbunge wa Jimbo la Kilolo.