Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(OR-TAMISEMI) George Simbachawene akiongea na wadau wa mradi wa mabasi
yaendayo haraka (hawapo pichani) yanayosimamiwa na Wakala wa Mabasi Yaendayo
Haraka (DART) jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(OR-TAMISEMI) George Simbachawene (kushoto) akiongea na wadau wa mradi
wa mabasi yaendayo haraka (hawapo pichani) yanayosimamiwa na Wakala wa Mabasi
Yaendayo Haraka (DART) jijini Dar es salaam. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Wakala
wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(OR-TAMISEMI) George Simbachawene (kulia) akiongea na wadau wa mradi wa
mabasi yaendayo haraka (hawapo pichani) yanayosimamiwa na Wakala wa Mabasi
Yaendayo Haraka (DART) jijini Dar es salaam. Kushoto ni Naibu Waziri Nchi Ofisi
ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Selemani Jaffo.
Kaimu Mtendaji Mkuu Wakala wa
Mabasi Yaendayo Haraka (DART) Mhandisi Ronald Lwekatare akitoa taarifa ya mradi
wa mabasi yaendayo haraka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) George Simbachawene (kushoto) akiongea na wadau
wa mradi wa mabasi yaendayo haraka (hawapo pichani) yanayosimamiwa na Wakala wa
Mabasi Yaendayo Haraka (DART) jijini Dar es salaam. Katikati ni Naibu Waziri
Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Selemani
Jaffo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(OR-TAMISEMI) George Simbachawene (wa pili kulia) akiongea na wadau wa
mradi wa mabasi yaendayo haraka yanayosimamiwa na Wakala wa Mabasi Yaendayo
Haraka (DART) jijini Dar es salaam.
Msajili Masaidizi wa Hazina
Jones Mwalemba akitoa ufafanuzi namna
ofisi yake inavyochangia katika kukamilisha mradi wa mabasi yaendayo
haraka wakati wa mkutano wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa (OR-TAMISEMI) George Simbachawene
alipokuwa akiongea na wadau wa mradi wa mabasi yaendayo haraka
yanayosimamiwa na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Takwimu UDART
Hamdi Al-Hadj akifafanua jambo wakati wa mkutano wa Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) George
Simbachawene alipokuwa akiongea na wadau
wa mradi wa mabasi yaendayo haraka yanayosimamiwa na Wakala wa Mabasi Yaendayo
Haraka (DART) jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa
Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) mkutano wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) George Simbachawene alipokuwa akiongea na wadau wa mradi wa
mabasi yaendayo haraka yanayosimamiwa na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka
(DART) jijini Dar es salaam.
(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
Na EleuteriMangi-MAELEZO
Waziri wa NchiOfisi ya Rais Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI)
George Simbachawene amewaagiza wadau wa mradi wa mabasi yaendayo haraka yanayosimamiwa
na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kuhakikisha wanampatia taarifa ifikapo
Aprili 3, 2016 ni lini mradi huo utaanza kutoa huduma.
Uamuzi huo wa Waziri Simbachawene
unafuatia makubaliano yaliyofikiwa wakati wa kikao na wadau hao Machi 31, 2016
kilichofanyika ofisi za DART jijini Dar es salaam ili kuhakikisha wanatoa huduma
ya usafiri wa uhakika kwa Watanzania na hasa wakazi wa jiji hilo.
“Kama mambo yote yataenda vizuri mradi
huu utaanza mapema angalau mabasi 50 yaanze kutoa huduma mapema iwezekanavyo” alisema
Simbachawene.
Simbachawene alisema kuwa hadi sasa
mabasi mawili yamesha anza kufanya majaribio katika barabara za mradi huo na kuwahimiza
wadau hao waongeze idadi ya mabasi yanayofanya majaribio angalau yafike 15 ili madereva
wazoee barabara kabla ya mradi kuanza kutoa huduma rasmi.
Ili kuongeza kasi ya kukamilisha mradi
huo, Simachawene amewataka wadau hao wa mradi wa mabasi yaendayo haraka wawe na
utaratibu wa kukutana kila siku kwa kuzingatia kazi walizojipangia na kuangalia
utekelezaji wake umefikia wapi na kumpatia taarifa kila baada ya siku mbili.
Aidha, Simbachawene amewaasa wa kazi
wa jiji la Dar es salaam wawe watulivu kwa kuwa kazi kubwa ya mradi huo imekamilika
na mradi umekaribia kuanza kuleta matunda na hivyo waitunze miundombinu hiyo ikiwemo
barabara na vifaa vitakavyokuwa vinatumika wakati wa kutoa huduma.
“Kuhujumu miundombinu ya DART ni kulihujumu
taifa letu, watu wote ni lazima wawe na uzalendo kwa mali yao ili mradi uwe wa tija
kwa manufaa ya nchi yetu” alisema Simbachawene.
Simbachawene amesema kuwa utunzaji
wa miundombinu hiyo utafanikiwa iwapo kutakuwa na ushirikiano mzuri kati ya
wananchi, wadau wa mradi wa DART na Serikali.
Katika kikao hicho na wadau wa mradi
wa DART, Waziri Simbachawene aliambatana na Naibu Waziri wake Selemani Jaffo pamoja
na viongozi mbalimbali wa Serikali.
Mabasi ya Mradi wa Mabasi yaendayo
haraka yatakuwa yanafanya safari zake ya kutoa huduma ya usafiri kwa wananchi kupitia
eneo la Kimara, Ubungo, Morocco, Magomeni, Feri na Kariaakoo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Takwimu
UDART Hamdi Al-Hadj amesema kuwa kutakuwa na jumla ya mabasi 140 ambayo yanatarajiwa
kutoa huduma katika mradi wa DART jijini Dar es Salaam.
Kikao cha Waziri Simbachawene kilihuwahusisha
wadau wa mradi huo ambao ni DART, TANROAD, Msajili wa Hazina, Kampuni ya Simon
Group, SUMARTA, Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) na Jeshi la Polisi.
No comments:
Post a Comment