Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John William Kijazi akifungua mafunzo ya
Wakuu wa Mashirika na Taasisi za Umma yalioandaliwa na Ofisi ya Rais,
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma leo jijini Dar es salaam. Kushoto
ni Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Salome
Kaganda.
Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Salome
Kaganda akitoa maelezo mafupi yanayohusu Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili
ya Viongozi wa Umma wakati wa mafunzo ya Wakuu wa Mashirika na Taasisi za Umma
leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John
William Kijazi.
Baadhi ya Washiriki wa mafunzo ya Wakuu wa Mashirika na Taasisi za Umma
waliohudhuria mafunzo ya maadili yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais, Sekretarieti
ya Maadili ya Viongozi wa Umma leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Washiriki wa mafunzo ya Wakuu wa Mashirika na Taasisi za Umma
waliohudhuria mafunzo ya maadili yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais, Sekretarieti
ya Maadili ya Viongozi wa Umma wakimsikiliza Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
Mhandisi John William Kijazi (hayupo pichani) leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya Washiriki wa mafunzo ya Wakuu wa Mashirika na Taasisi za Umma
waliohudhuria mafunzo ya maadili yaliyoandaliwa na Ofisi ya Rais, Sekretarieti
ya Maadili ya Viongozi wa Umma wakimsikiliza Katibu Mkuu Kiongozi Balozi
Mhandisi John William Kijazi leo jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John William Kijazi akiongea na Waandishi
wa habari mara baada ya kufungua mafunzo ya Wakuu wa Mashirika na Taasisi za
Umma yalioandaliwa na Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa
Umma leo jijini Dar es salaam.
(Picha
na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi
John William Kijazi amewaasa Wakuu wa Mashirika na Taasisi za Umma kuzingatia
Maadili ya Viongozi wa Umma katika kutekeleza makujumu yao.
Katibu Mkuu alisema hayo leo jijini Dar
es salaam wakati wa akifungua mafunzo ya viongozi hao yalioandaliwa na Ofisi ya
Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ili kuhakikisha wanaendana
Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe
Mgufuli.
“Maadili yana umuhimu wake mkubwa
katika utawala wa maendeleo ya nchi, kupitia maadili mema wananchi wanajenga
imani na viongozi pamoja na Serikali yao kwa ujumla” alisema Balozi Mhandisi Kijazi.
Ili kuhakikisha mafunzo yanakuwa yenye
tija, Balozi Mhandisi Kijazi amewasisitiza viongozi hao kutumia muda vizuri na
kujikumbusha na kujifunza maadili hayo kwa manufaa ya mashirika na taasisi zao
pamoja na taifa kwa ujumla.
Balozi Mhandisi Kijazi alitaja umuhimu
wa maadili katika jamii na kusema kuwa yanasaidia kusimamia rasilimali za umma
na kuzitumia kwa maslahi ya wote, kuongeza tija na thamani ya huduma, zinazotolewa
na Serikali, kudhibiti mianya ya ukiukwaji wa
maadili na vitendo vya rushwa, kujenga ujasiri wa kusimamia Sheria,
Kanuni na Taratibu za utumishi wa umma.
Maadili pia yanasaidia wananchi,
viongozi na Watumishi wa Umma kutoa mchango wa haraka katika kutekeleza
maendeleo ya nchi, kuepuka utata wa maamuzi ya migongano ya kimaslahi,
kuwavutia wawekezaji, kujenga na kudumisha amani na utulivu pamoja na kuondoa
na kukomesha ubinafsi kwa viongozi.
Aidha, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Kijazi amesema kuwa ukiukwaji wa maadili
unaathari hasi kwa taifa ambapo alizitaja baadhi ya athari hizo kuwa ni
rasilimali za nchi kunufaisha wachache, wananchi kukosa haki zao za msingi
kutokana na rushwa na upendeleo, viongozi wa umma kujilimbikizia mali isivyostahili
bila kujali hali za wananchi wanaowaongoza, kupungua kasi ya uwekezaji pamoja
na kudhohofika kwa uchumi wa nchi.
Madhara mengine ya kutojali maadili ni
wananchi kukosa imani na Serikali yao, kuchochea vurugu pamoja na wananchi
kutotii sheria za nchi na hivyo kuhatarisha usalama, amani na utulivu wa nchi.
Kwa upande wake Kamishna wa
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda
alipokuwa maelezo mafupi kwa Mgeni Rasmi amesema kuwa misingi ya maadili na
maadili yanalenga katika kuzuia mgongano wa maslahi, upendeleo, matumizi mabaya
ya rasilimali za umma na taarifa za ofisi na mwenendo usiofaa kwa viongozi wa
umma ili kuimarisha na kuendeleza dhana za uadilifu, uwajibikaji na uwazi ambazo ni sifa muhimu za kiongozi.
Ili kuongeza ufanisi katika utendaji
kazi, Jaji Mstaafu Kaganda amesema kuwa ofisi yake inakabiliwa na changamoto
mbalimbali ikiwemo upungufu wa watumishi ambapo kuna zaidi ya viongozi 15,000
huku Sekretarieti ina wafanyakazi 200 nchi nzima.
Mafunzo hayo yamehudhuriwa na washiriki 40
ambapo yalifanyika kwa Mawaziri, Manaibu Waziri, Mkatibu Wakuu, Manaibu Katibu
Wakuu, Wenza wa Viongozi, Wakuu wa Mikoa.
No comments:
Post a Comment