Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Meck Sadiki akikabidhi madawati 400 yenye thamani ya shilingi milioni 66 kwa mwenyekiti wa halmashauri ya Mwanga Theresia Msuya yaliotolewa na Kampuni ya Tigo, Kulia ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini George Lugata.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Meck Sadiki(Kulia), akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mwanga Theresia Msuya(katikati) Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini George Lugata.
Aprili 20 2016 Mwanga: Kampuni ya Tigo
Tanzania imetoa msaada wa madawati 400 yenye thamani ya shilingi milioni 66 kwa
shule nane za msingi katika manispaa ya Mwanga, mkoa wa Kilimanjaro, ikiwa ni
mchango wa kampuni hiyo katika kuisaidia serikali kukabiliana na upungufu wa
madawati katika shule za msingi nchini.
Akizungumza leo katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika
katika shule ya msingi Reli Juu katika manispaa ya Mwanga, Mkurugenzi wa Tigo
Kanda ya Kaskazini George Lugata amesema mchango huo ni sehemu ya utekelezaji wa
dhamira ya kampuni hiyo ya kuunga mkono jitihada mbalimbali za kuleta maendeleo
nchini.
“Mchango huu ni sehemu ya jitihada mbalimbali
zinazofanywa na Tigo katika kusaidia utekelezaji wa miradi yenye tija kubwa kwa
jamii. Tunaamini kwamba kupitia msaada huu, Tigo inatoa mchango wake katika kujenga
viongozi wa baadaye wa taifa hili na wanataluuma mbalimbali wakiwamo madaktari,
wahandisi na wengineo, "amesema Lugata.
Lugata amesema mwaka jana Tigo
ilikabidhi msaada kama huo wa madawati katika shule za msingi katika mikoa ya
Shinyanga, Mbeya Iringa na Morogoro na kuongeza
kwamba kampuni hiyo itaendelea kutoa madawati zaidi sehemu mbalimbali nchini
siku za zijazo.
Makabidhiano yalihudhuriwa na Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro mheshimiwa Meck Sadiki ambaye alisema madawati hayo 400
yataboresha mazingira ya kujifunzia kwa watoto katika Mkoa wa Kilimanjaro na
kutoa wito kwa wadau wengine kuunga mkono zoezi hilo.
“Tunapenda
kutoa shukrani zetu za dhati kwa kampuni ya Tigo kwa kuwa mdau muhimu kwetu
katika jitihada zinazoendelea za kujaribu kupunguza tatizo la ukosefu wa
madawati ya kutosha katika shule za msingi za mkoa wetu wa Kilimanjaro. Ni dhahiri
kwamba msaada huu wa madawati 400 yatawawezesha mamia ya wanafunzi wetu kupata
sehemu za kukaa na hivyo kujipatia elimu zao katika mazingira bora zaidi,”
alisema Sadiki
Madawati
hayo yametolewa kwa shule za msingi nane
kama ifuatavo, Mramba,Kawawa, Mwanga, Naweru,Kiboriloni, Lawate na Reli Juu.
|
Twitter Buzz
....
...
IMETOSHA!
Featured post
KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO
Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...
Saturday, 23 April 2016
TIGO WAKABIDHI MADAWATI 400 KWA WILAYA YA MWANGA KATIKA SHULE 8
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment