Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 13 April 2016

CHUO KIKUU ARDHI CHAWAPA MWONGOZO WANAFUNZI WA SHULE ZA SEKONDARI ZA JIJI LA DAR ES SALAAM KUHUSU NAMNA BORA YA KUJIUNGA NA MASOMO YA ELIMU YA JUU KULINGANA NA UFAULU WAO JUU


Mtaalam wa Jiografia kutoka Chuo Kikuu Ardhi Dkt. Mlenge Fanuel Mgendi  akiwahamasisha wanafunzi wa kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Jangwani  kupenda kusoma na kuweka bidii katika masomo ambayo wana uwezo nayo ili yawasaidie kuendelea na Elimu ya Juu katika chuo Kikuu Ardhi na vyuo vingine leo jijini Dar es salaam. Chuo Kikuu Ardhi kinaendesha Programu ya utoaji elimu kwa wanafunzi wa sekondari katika shule mbalimbali kwa lengo la kuwasaidia  kufanya uchaguzi sahihi wa kozi za masomo wanazotarajia kuendelea nazo pindi watakapohitimu masomo ya elimu ya Sekondari.

Mwanataaluma wa Chuo Kikuu Ardhi Bi. Latifa Litwe (kushoto) akitoa elimu kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Jangwani namna ambavyo Chuo Kikuu Ardhi kinawajengea uwezo kielimu wanafunzi wanaosoma katika chuo hicho kukabiliana na mabadiliko ya Tabia Nchi na majanga mbalimbali yanayoihusu sekta ya Ardhi kwa ujumla hapa nchini ikiwemo uhifadhi wa Ardhi na Sayansi ya Udongo.

Baadhi ya wanafunzi wa Kidato cha Sita wa Shule ya Wasichana ya Jangwani wakiangalia na kufurahishwa na moja ya Kazi ya Ubunifu wa Majengo na mitaa iliyofanywa na wanafunzi wa Chuo Kikuu Ardhi mwaka wan nne leo jijini Dar es salaam.


No comments:

Post a Comment