Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. George Simbachawene (kulia)
akiongea na Mama Graca Machel (kushoto) alipomtembelea ofisini kwake jana jijini
Dar es salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),
Mhe. George Simbachawene akiongea na Mama Graca Machel (hayupo pichani)
alipomtembelea ofisini kwake jana jijini Dar es salaam.
Mama Graca Machel akiongea na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani)
alipomtembelea ofisini kwake jana jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),
Mhe. George Simbachawene (kulia) akiteta jambo na Mama Graca Machel (kushoto)
mara baada ya mazungumzo ofisini kwake jijini Dar es salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),
Mhe. George Simbachawene (kulia) akiagana na Mama Graca Machel (kushoto) mara
baada ya mazungumzo ofisini kwake jana jijini Dar es salaam.
(Picha
na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
Na Rebecca Kwandu
Watoto wa
kike 20,000 kutoka mkoa wa Mara watanufaika kwa fursa ya kupata elimu kupitia Mfuko
wa Graca Machel (Graca Machel Trust) ambao umejikita katika kusaidia wanawake
na watoto nchi kadhaa za Afrika.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI), Mhe. George Simbachawene mara baada ya mazungumzo na Mama Graca
Machel alipomtembelea ofisini kwake jana jijini Dar es salaam.
“Ni fursa
nzuri ya kushirikiana na wadau wa ndani na nje ya nchi kuwasaidia watoto wetu
wa kike kielimu ambayo itawasaidia kutoka katika jamii ya umasikini na
kuhakikisha wamepata fursa ya kuvuka umri wa vishawishi na maamuzi yasiyo
sahihi” alisema Waziri Simbachawene.
Watoto hao
watakaonufaika na Mfuko huo mkoani Mara watatoka katika shule 104 ambapo
inatarajiwa kuwafikia watoto wa kike wengi zaidi mara baada kuanza kutoa huduma
hiyo mkoani humo.
Waziri
Simbachawene amesema kuwa Mama Graca Machel amechagua kuja katika Tanzania
kutokana ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Msumbiji kwa kuzingatia
mchango mkubwa wa Tanzania kwa nchi hiyo.
Aidha, Waziri
Simbachawene amemshukuru Mama Graca Machel kwa kujali na kuuchagua mkoa wa Mara
ambao ndio mkoa alipozaliwa Mwasisi wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Kwa upande
wake Mama Graca Machel amemshukuru Waziri Simbachawene kwa mapokezi na ushirikiano
alioupata katika Serikali ya Awamu Tano iliyopo madarakani na kuahidi kuendelea
kusirikiana nao ambapo anaamini mpango wa kuwasaidia watoto wa kike kupita
taasisi yake utapanuka na hatimaye kuweza kuwafikia watoto wa kike wengi zaidi
kupitia mikoa yote nchini.
“Lengo ni
kuwabakisha watoto wa kike shuleni ili wapate elimu, ni lazima tusaidiane wote,
tuna kila sababu ya kusaidiana” alisema Mama Graca Machel.
Uhusiano wa
Tanzania na Msumbiji ni wa kihistoria kwani wananchi wa nchi hizo walishirikiana
katika shughuli mbalimbali chini ya mwavuli wa unasaba na ushirikiano katika
biashara na tamaduni kwenye miji ya Unguja, Kilwa, Lindi na Mtwara kwa upande
wa Tanzania na katika miji ya Chilimbo, Tete, Pemba na Sofala nchini Msumbiji.
No comments:
Post a Comment