Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Sunday 10 April 2016

UMMY MWALIMU AZINDUA RASMI TAASISI YA BASILLA MWANUKUZI

Miss Tanzania 1998, Basila Mwanukuzi akiwa na Hashim Lundenga katika mkutano na wanahabari mwaka 1998.

 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

MH.UMMY MWALIMU  AZINDUA RASMI TAASISI YA BASILLA MWANUKUZI
  • Yaanza na mradi wa ‘Wezesha Mama Lishe Tanzania’
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Tanzania, Ummy Mwalimu, kesho (11.4.2016) leo amezindua rasmi taasisi ya Basilla Mwanukuzi yenye lengo la kushirikiana na wadau ili kuwawezesha wanawake na kuinua uwezo wao wa kibunifu na kiuchumi.

Taasisi ya BMF itajikita katika kuwasaidia wanawake wa makundi tofauti kujitoa kutoka kwenye hali ya kusaidiwa hadi kuweza kusimamia miradi yao wenyewe na hivyo kubadili hali zao za maisha na kiuchumi.
Kama sehemu ya uzinduzi wa taasisi, BMF pia imezindua mradi wa ‘Wezesha Mama Lishe Tanzania’ ukiwa na lengo la kuwawezesha mama lishe kwa kuwawezesha kupata elimu ya ujasiriamali, afya pamoja na kupika chakula bora chenye kuzingatia virutubisho na uwezeshaji wa kupata mikopo na kuongeza mitaji yao.Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo, Mwanzilishi wa taasisi ya BMF, Basilla Mwanukuzi alisema taasisi yake iliguswa na changamoto nyingi zinazolikabili kundi hili la mama lishe kwa kipindi kirefu bila msaada wowote.
‘Baada ya kufanya utafiti kwa muda mrefu na kuzungumza na Mama lishe tumegundua kina mama hawa katika mazingira yao tofauti ya kazi wana changamoto zinazofanana kama mazingira mabovu ya kazi na ukosefu wa mitaji, kwa hiyo mradi huu utajikita kuwasaidia kina mama lishe watambulike, waweze kujiamini na kupewa thamani katika jamii’ alisema Basilla.
Akielezea zaidi kuhusu mradi wa ‘Wezesha Mama Lishe’, Basilla alisema anaamini mama Lishe wakipata mikopo wataweza kuboresha biashara zao kwa kuandaa mazingira yao ikiwa ni pamoja na kununua viti, meza na vyombo vya kisasa vitavyowafanya wateja wawaamini zaidi na kuwapa thamani zaidi, hivyo kubadilisha mawazo hasi katika jamii kuwa mama lishe hawapiki chakula bora.
‘Nusu ya nguvu kazi ya taifa inalishwa na kina mama hawa, hivyo kuna haja kubwa kuwasaidia kurasimimisha shughuli hii, kwanza kuwasaidia kujiinua kiuchumi na pia kuchangia pato la taifa kwa kulipa kodi na kadhalika, lakini pia vyakula vya mama lishe ni tegemeo la watanzania wengi kwani bei yake huwa ni nafuu’ alisema Basilla.
Utekelezaji wa Mradi wa Wezesha Mama Lishe pia utajumuisha uundaji wa vikundi vya ushirikiano wa mama lishe ili kubadilishana uzoefu na pia uanzishaji wa shughuli za kujiingizia kipato kwa Mama Lishe kama utafutaji wa tenda za kuandaa vyakula vya harusi na kadhalika.
Mpaka sasa mradi wa Wezesha Mama Lishe umefanikiwa kuanza kuwaandikisha Mama lishe waliopo jijini Dar es Salaam, na baadhi wameanza kupata mikopo ya riba ndogo, huku ukitarajia kupanuka nchi nzima ili kuwafikia mama lishe wengi zaidi.
‘Hatua ya kwanza ni kuwatambua mama lishe, ambapo mpaka sasa tuko kwenye hatua ya kuwasajili, halafu baada ya hapo ni kutoa elimu ya afya na ujasiriamali sambamba na utoaji mikopo kwa kushirikiana na benki ya Covenant’ alisema Basilla.

IMEDHIBITISHWA NA:
Basilla Mwanakuzi



No comments:

Post a Comment