Tunaomba radhi sana kwa taarifa kwamba idadi kadhaa ya abiria wetu walishindwa
kufika kwenye maeneo waliyokusudia jioni ya Aprili 2, 2016.
Hii ilitokana na kushindwa kufanya kazi kwa
mfumo wa taa kwenye njia ya kurukia kwenye uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro na
hivyo kukosekana kwa usalama ambao
ungewawezesha marubani wetu kutua.
Huu ni mfululizo wa matukio ambayo
yalisababisha kufutwa kwa ndege mbili
miongoni mwa ndege zetu kutua usiku ule:
- Ndege Na. FN157 iliondoka
kwenye uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa 3.18 usiku ikitarajiwa kutua kwenye
Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro kabla ya muda unaotakiwa saa 4.40 usiku. Wakati ndegte
ikikaribia Uwanja wa Kilimanjaro
marubani wetu walijulishwa na mnara
wa kuongozea ndege kwamba taa
zilizopo kwenye njia ya kurukia ndege
zilikuwa hazifanyi kazi lakini hali ingetengemaa muda usiokuwa mrefu. Ndege
ilizunguka uwanja wa
Kilimanjaro ikisubiri ukarabati wa taa hizo kwa takribani dakika 30 kabla ya kurudi Dar es salaam
kwa kuwa taa hizo zilikuwa bado hazifanyi kazi.
- Ndege iliwasili tena Dar es
Salaam saa 5.20 usiku na abiria walibaki kwenye ukumbi wa kusubiria ndege wakati ndege ikijazwa mafuta tena na marubani
wakiandaa mpango mpya wa kusafiri tayari
kurudi Kilimanjaro mapema kadri
iwezekanavyo pindi ukarabati wa taa kwenye njia ya kurukia
ndege ukikamilika. Kwa bahati mbaya
taa hizo zilikuwa hazifanyi kazi
hadi kufikia saa saa 7.00
usiku wa kuamkia Aprili 3, 2016,
ambapo muda sahihi na salama kwa marubani wa ndege ukiwa umemalizika kwa kuwa
walishakuwa kazini kuanzia saa
12.30 jioni.
- Hii inamaanisha kwamba hatukuwa na mbadala wa kufuta safari, na hivyo ndege Na. FN158 ambayo
ilikuwa irudi kutoka Kilimanjaro kuja Dar es Salaam.
- Abiria wetu waliopata usumbufu
walipewa nafasi kwenye ndege iliyokuwa inafuatia na ilisafiri kutoka uwanja wa pili kurudi kule walikotoka. Baadhi ya abira walichukua mbadala huu lakini wengie
waliamua kubaki katika uwanja wa
ndege kusubiri ndege iliyofuata.
- Abiria wote walioomba kupatiwa usafiri kwenye ndege
iliyofuata walisafiri nasi kwa
kuelekea maeneo waliyokuwa wanakwenda Aprili 3, 2016.
- Tunaomba radhi kwa abiria wetu waliokuwa kwenye safari ile kwa usumbufu walioupata huku tukiwahakikishia kuwa
tunaweka kipaumbele kikubwa kwenye
usalama wa abiria wetu na marubani.
John Corse,
Meneja Mkuu, fastjet
Tanzania
No comments:
Post a Comment