Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Charles Kitwanga (kushoto) akizungumza katika kikao cha Mapitio ya Rasimu ya Bajeti
ya Wizara yake ya Mwaka 2016/17 kwa upande wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
pamoja na Idara ya Uhamiaji. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano
wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo, kilijumuisha Viongozi Wakuu wa
Taasisi hizo pamoja na Wakuu wa Idara wa Wizara hiyo. Wa pili kushoto ni Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira, na kulia ni Naibu Katibu
Mkuu, Balozi Simba Yahya. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Charles Kitwanga (kushoto) akimsikiliza Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji,
Victoria Lembeli (kulia) wakati alipokuwa anatoa taarifa yake katika kikao cha
Mapitio ya Rasimu ya Bajeti ya Mwaka 2016/17 kwa Idara ya Uhamiaji
kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam
leo. Kikao hicho kilijumuisha Viongozi Wakuu wa Uhamiaji na Wakuu wa Idara ya
Wizara hiyo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Charles Kitwanga akiwafafanulia jambo Viongozi Wakuu wa Jeshi la Zimamoto na
Uokoaji na Wakuu wa Idara ya Wizara yake katika kikao cha Mapitio ya Rasimu ya
Bajeti ya Mwaka 2016/17 kwa Jeshi hilo kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano
wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kulia meza kuu ni Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira. Wapili kulia ni Naibu Katibu Mkuu
wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya, na wa tatu kushoto ni Kaimu Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Rogatius Kipali. Picha na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Charles Kitwanga (wapili kulia) akizungumza na Viongozi Wakuu wa Idara ya
Uhamiaji katika kikao cha Mapitio ya Rasimu ya Bajeti ya Mwaka 2016/17 ya
Wizara yake. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo,
jijini Dar es Salaam leo, pia kilihudhuriwa na Wakuu wa Idara wa Wizara hiyo.
Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira, na wa
pili kushoto ni Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli
akifuatiwa na Mrakibu Mwandamizi wa Idara ya Uhamiaji, Joseph Mtenga. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
No comments:
Post a Comment