Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene
(kushoto) akipokea taarifa ya watumishi hewa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora
Mhe. Aggrey Mwanri (kulia) hivi karibuni katika ukumbi wa Karimjeejijini
Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri
Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Selemani Jaffo na katikati ni Katibu Mkuu Ofisi ya
Rais-TAMISEMI Bw. Mussa Iyombe.
Baadhi ya Wakuu wa Mikoa na Makatibu
Tawalawa Mikoa kutoka Tanzania Bara wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI
Mhe. George Simbachawene (hayupo pichani) katika kikao cha kujadili mwelekeo wa
bajeti za Mikoa na Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2016/2017 kilichofanyika katika
ukumbiwaKarimjeejijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene akitoa maelekezo kwa Wakuu
wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa katika kikao cha kujadili mwelekeo wa bajeti
za Mikoa na Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2016/2017 kilichofanyika katika ukumbi
wa Karimjee jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene (kushoto) akipokea taarifa ya
watumishi hewa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Felix Ntibenda (kulia) hivi karibuni
katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam. Wa
kwanza kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Selemani Jaffo na
katikati ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bw. Mussa Iyombe.
Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene
(kushoto) akipokea taarifa ya watumishi hewa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Halima Dendego (kulia) hivi karibuni
katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam. Wa
kwanza kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Selemani Jaffo na
katikati ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bw. Mussa Iyombe.
Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene (kushoto)
akipokea taarifa ya watumishi hewa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Rehema
Nchimbi (kulia) hivi karibuni katika ukumbi wa Karimjee jijini
Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri
Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Selemani Jaffo na katikati ni Katibu Mkuu Ofisi ya
Rais-TAMISEMI Bw. Mussa Iyombe.
Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene
(kushoto) akipokea taarifa ya watumishi hewa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe.
Anne Kilango Malecela(kulia) hivi karibuni katika ukumbi wa Karimjee
jijini Dar es Salaam.Wa pili kushoto ni Katibu
Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bw. Mussa Iyombe.
Na
Rebecca Kwandu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali zaMitaa
(OR-TAMISEMI) Mhe. George Simbachawene amewaagiza Wakuu wa Mikoa kuhakikisha wanakusanya
mapato vizuri kwa kutumia Mfumo wa Kielektroniki wa Ukusanyaji wa Mapato na kutumia
vizuri fedha zilizokusanywa ili kuwaletea maendeleo wananchi katika mikoa yao.
Akizungumza katika kikao kati yake na Wakuu wa Mikoa na Makatibu
Tawala wa Mikoa cha kujadili mwelekeo wa bajeti za Mikoa na Halmashauri iliyofanyika
katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam hivi karibuni Mhe. Simbachawene aliwataka
Wakuu wa Mikoa kutumia umahiri na ustadi zaidi katika kubuni vyanzo vipya vyama
pato zaidi ya vile vilivyozoeleka kila siku ili kupata fedha za kutekeleza shughuli
za maendeleo katika maeneo yao.
“Mipango ya bajeti zetu lazima zinakisi matatizo yaliyopo,
hakikisheni rasilimali chache zinazopatikana zinatumika vizuri na pia
hakikisheni Kuwa kila fedha inayopatika na inawekezwa katika eneo husika na kwa
kufanya hivyo maendeleo yataonekana”. Alisema Mhe. Waziri
Mhe. Simbachawene aliwataka Wakuu wa Mikoa kuwatumia Wakuu wa Wilaya
katika maeneo yao kutatua kero na migogoro ya wananchi kwani alisema kwa kufanya
hivyo itaepusha wananchi kufikisha malalamiko yao ngazi za juu kwa kuwa tayari matatizo
yao yatakuwa yameshughulikiwa katika ngazi za chini.
“Migogoro mingi inayowasilishwa na wananchi inahusu dhuluma,
migogoro ya ardhi na kutotendewa haki kwa wananchi. Ukiona wananchi wanakuja juu kuleta malalamiko
ujue huko chini hawakushughulikiwa vizuri. Jaribuni kumaliza matatizo ya wananchi
huko chini na kuwafanya wananchi kuishi kwa amani na furaha”. Alisisitiza Mhe.
Simbachawene
Waziri wa Nchi pia aliwataka Wakuu wa Mikoa kukuza ajira katika
maeneo yao kwa kuanzisha viwanda vidogo na vya kati ili kuwaletea vijana ajira na
kuisaidia serikali kufikia lengo lake la kuwa nchi yenye uchumi wa kati baada ya
kila Mkuu wa Mkoa kutafsiri matarajio ya Serikali Kuu kwa vitendo.
“Anza kutekeleza malengo kwa kuangalia dira ya serikali ya kuifanya
nchi yetu kufikia uchumi wa kati na wakati unapoanza kutekeleza mapema anza kuona
kama kuna vikwazo vya kufikia lengo na kuliwasilisha sehemu husika ili serikali
ione namna ya kukusaidia kufikia lengo. Alieleza Mhe. Simbachawene.
Aidha, aliwaagiza Wakuu
wa Mikoa kuhakikisha wanasimamia vizuri suala la utoaji wa Elimu Msingi bila malipo
pamoja na kuhakikisha Mamlaka za Serikali za Mitaa hazizalishi madeni na hivyo kutoruhusu
madeni kuongezeka.
Katika kikao hicho Wakuu wa Mikoa pia waliwasilisha kwa Waziri
wa Nchi-TAMISEMI taarifa za zoezi la uhakiki wa watumishi hewa katika mikoa yao
ambapo Mhe. Waziri Simbachawene alizipokea na alieleza kuwa ataziwasilisha kwa
Waziri wa Utumishi kwa ajili ya kuziweka vizuri na baadaye zitawasilishwa kwa Mhe.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
No comments:
Post a Comment