Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene (kushoto) akipokea taarifa ya watumishi hewa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Felix Ntibenda (kulia) hivi karibuni katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Selemani Jaffo na katikati ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI Bw. Mussa Iyombe.
TAKRIBAN
watumishi 2,204 kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara wamekuwa wakiitia hasara serikali
ya Shs. 5.5 bilioni kila mwaka, brotherdanny.com inaripoti.
Hayo
yamebainishwa katika majumuisho ya awali ya ripoti za wakuu wa mikoa
zilizowasilishwa kwa Waziri wa Nchi (Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa), George Simbachawene, jijini Dar es Salaam Aprili Mosi, 2016
wakiitikia agizo la Rais John Magufuli la kufanya uhakiki wa watumishi hewa.
Hata
hivyo, ni Mkoa wa Shinyanga pekee ambao ubeinika kutokuwa na watumishi hewa kutokana
na mikakati iliyowekwa tangu Julai 2014 na mkuu wa mkoa aliyepita.
Inaonyesha
kwamba, Mkoa wa Arusha ndio unaoongoza kwa sasa kwa kuwa na watumishi hewa 270
ambao katika kipindi cha mwaka mmoja wamelamba kiasi cha Shs. 1.8 bilioni
ambazo ni fedha za walipa kodi.
Mkuu
wa mkoa huo, Daudi Felix Ntibenda, amesema katika zoezi hilo wamebaini idadi
hiyo ya watumishi hewa, ambao wamekuwa wakiitia hasara serikali kila mwaka.
“Mheshimiwa,
katika zoezi letu tumebaini kwamba wapo watumishi hewa 270 ambao wamekuwa
wakiisababishia serikali hasara ya Shs. 1.8 bilioni kila mwaka,” alisema.
Kwa
upande mwingine, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, alisema zoezi la
awali la uhakiki limebaini kuwepo kwa watumishi hewa 73 ambao wamesababisha
serikali ipoteze kiasi cha Shs. 316 milioni kila mwaka.
“Katika
mkoa huu tumepata watumishi hewa 73, lakini wengi watahoji kwa nini mkoa huu
mkubwa wenye idadi kuzwa ya watu na taasisi za umma una idadi ndogo ya
watumishi hewa, nataka nikuhakikishie tu Mheshimiwa Waziri, bado tunaendelea na
uchunguzi wetu wa kina,” alisema Makonda.
Katika
Mkoa wa Dodoma, wamegundulia watumishi hewa 101 na kwa mujibu wa Mkuu wa
Mkoa huo, Jordan Rugimbana, watumishi hao hewa wameisababishia serikali hasara
ya Shs. 287.3 milioni katika kipindi cha miezi sita tu iliyopita.
Mkuu
wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza, amesema katika mkoa wake wamegundua kuwepo
kwa watumishi hewa 15, lakini akasema kuna watumishi wengine 145 ambao
hajaonana nao.
“Mheshimiwa
Waziri, idadi hii inaweza kuongezeka kwa sababu wao watumishi wengine 145 ambao
sijaonana nao, bado tunaendelea na zoezi kuwabaini pamoja na kujua kiasi cha
hasara ambacho wameisababishia serikali,” alisema.
Naye
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali (mstaafu) Salum Kijuu amesema mkoa wake
wamebaini kuwepo kwa watumishi hewa 14 ambao wamesababisha upotevu wa fedha
za serikali Shs. 49.1 milioni.
Mkuu
wa Mkoa wa Katavi, Jenerali Raphael Muhuga, kwa upande wake amesema wamegundua
kuwepo kwa watumishi hewa 21 ambao wameitia serikali hasara ya Shs. 20.7
milioni.
Naye
Mkoa wa Kigoma, Bregedia Jenarali (mstaafu) Emmanuel Maganga amesema mkoa huo umebaini
kuwepo watumishi hewa 171 ambao wameitia serikali katika hasara ya Shs. 114.6
milioni.
Said
Meck Sadick, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, amemweleza Waziri Simbachawene
kwamba, ndani ya mkoa huo wamebaini kuwepo kwa watumishi hewa 111 ambao wameisababishia
hasara ya Shs. 281.4 kwa serikali.
Mkuu
waa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi, amesema mkoa wake una watumishi hewa 57
ambao wameitia hasara serikali Shs. 36.2 milioni.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Joel Bendera, amesema mkoa huo umegundua
kuwepo kwa watumishi hewa 42 ambao wameitia hasara serikali Shs. 313.9 milioni.
Katika
Mkoa wa Mara, mkuu wa mkoa huo, Magesa Mulongo, amesema wamebaini kuna
watumishi hewa 94 mkoani humo ambao wameitia hasara serikali Shs. 121
milioni.
Kwa
upande wa Mkoa wa Mbeya, Mkuu wa Mkuo huo, Amos Makalla amesema wamegundua
kuwepo kwa watumishi hewa 98 ambao wameitia hasara serikali Shs. 459 .6 milioni
kwa mwaka.
Kwenye
Mkoa wa Morogoro, mkuu wa mkoa huo, Dk. Steven Kebwe, amesema mkoa wake
umegundua kuwepo kwa watumishi hewa 122 ambao wameitia hasara serikali Shs.
450.7 milioni.
Naye
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu, amesema mkoa wake ubaini kuwepo kwa
watumishi hewa 17, huku watumishi wengine 285 uchunguzi ukiendelea.
“Watumishi
hao 17 wameitia hasara serikali Shs. 216.5 milioni,” alisema Dendegu.
Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, amesema mkoa wake umengundulika kuwa na watumishi
hewa 334.
Mkuu
wa Mkoa wa NJombe, Dk. Rehema Nchimbi, amesema mkoa wake umegundulika kuwa na watumiwa
na hewa 34 ambao amesema wamekuwa wakiitia hasara serikali Shs. 20.1 milioni
kila mwaka.
Naye
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo, amesema mkoa wake umekuwa na
watumishi hewa 150 huku hakishindwa kusema hasara ya fedha za serikali kwa
madai kuwa uchunguzi unaendelea.
Katika
Mkoa wa Rukwa, mkuu wa mkoa huo Kamishna Mstaafu Zerote Steven, amesema mkoa
wake umekuwa na watumishi hewa 18 na wametia hasara serikali Shs. 55.6 milioni.
Mkuu
wa Mkoa wa Ruvuma, Thabit Mwambungu, amesema mkoa huo umebainika kuwa na
watumishi hewa 35 ambao wameitia hasara serikali Shs. 58.4 milioni.
Mkuu
wa Mkoa Simiyu, Antony Mtaka, amesema mkoa huo umegundulika kuwa na watumishi
hewa 62 ambao wameitia hasara serikali ya Shs. 320.9 milioni.
Katika
Mkoa wa Singida, mkuu wa mkoa huo, Mhandisi Mathew Mtigumwe, amesema wafanyakazi
hewa waliobainika mkoani kwake ni 231 na kueleza kuwa uchunguzi bado unaendelea
ili kubawaini zaidi na kujua kiasi cha hasara waliyoisababishia serikali.
Mkuu
wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri, amesema katika mkoa wake watumishi hewa waliobainika
ni 48 ambapo wanaitia hasara serikali Shs. 118.7 milioni.
Naye
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela, amesema watumishi hewa waliobainika
mkoani humo ni 104 ambapo amesema tathmini ya kuhakiki bado inaendelea.
No comments:
Post a Comment