Dk. Nalin Nag Mshauri Mwandamizi wa madawa, aleji, upungufu wa kinga pamoja na magonjwa ya kuambukiza kutoka hospitali za Apollo; New Delhi.
Na Mwandishi wetu,
Na Mwandishi wetu,
Siku
ya UKIMWI duniani inaadhimishwa tarehe mosi desemba kila mwaka, kutoa
fursa kwa jamii kuungana ulimwenguni kupiga vita gonjwa la UKIMWI,
kuwapa moyo wale wote wanaoishi na virusi vya ukimwi na kuwakumbuka wote
waliokufa kwa ugonjwa huu. Siku ya ukimwi duniani iliadhimishwa kwa
mara ya kwanza mwaka 1988.
Zaidi
ya miaka 30 toka ukimwi ulipoanza kusambaa nchini Tanzania, msisitizo
umewekwa kwenye maendeleo ya mikakati na mbinu zaidi za kupunguza
maambukizi na kuongeza huduma za matibabu. Kwa mwaka 2011, inakadiriwa
watanzania milioni 1.6 walikuwa wanaaishi na virusi vya UKIMWI na
miongoni mwao, milioni 1.3 ni wenye umri zaidi ya miaka 15, hiyo ni kwa
mujibu wa takwimu za mwaka 2012 kutoka shirika la umoja wa mataifa la
kupambana na UKIMWI (UNAIDS). Licha maambukizi ya UKIMWI kwa Tanzania
bara yamepungua kutoka asilimia 7.0 hadi 5.3 katika kipindi cha mwaka
2003/2004 mpaka 2011/2012 miongoni mwao wakiwa watu wenye umri wa miaka
15-49 na kutoka asiimia 6.3 mpaka 3.9 ambao ni wanaume katika kundi
hilo, na hakuna takwimu nzuri za kuonyesha kupungua kwa maabukizi kwa
upande wa wanawake.
Kwa
mujibu wa TACAIDS taarifa za mwaka 2013, kwa tanzania bara maambukizi
kimikoa yanatofautiana kutoka asilimia 1.5 kwa mkoa wa Manyara hadi
asilimia 14.8 kwa mkoa wa Njombe.
“Kufikia
sifuri tatu” ndio kauli mbiu iliyochaguliwa na kampeni ya siku ya
ukimwi duniani kuadhamisha ya siku ya UKIMWI duniani kwa mwaka huu.
Kwetu tanzania kupitia TACAIDS tunahamasisha “kufikia sifuri tatu”
tukimaanisha “sifuri katika maambukizi mapya ya UKIMWI”, sifuri katika
kuwanyanyapaa na kuwanyanyasa waathirika, na sifuri katika vifo
vinavyohusisha UKIMWI”. Maudhui hayo yalipitishwa tokea mwaka 2011
yatumike mpaka 2015, yakitafsiri yale malengo ya UNAIDS ya kufikisha
kiwango cha “kufikia sifuri katika maambukizi mapya ya UKIMWI”, na
sifuri katika vifo vinavyohusisha UKIMWI”. Maamuzi ya kuchagua “kufikia
sifuri tatu” yalifikiwa baada ya mahojiano ya kina na watu wanaoishi na
virusi vya UKIMWI, wanaharakati wa afya na taasisi ya kijamii.
Katika kuweka msisitizo katika maudhui ya mwaka huu, “kufikia sifuri tatu”, Dk. Nalin Nag mshauri mwandamizi wa madawa, aleji na upungufu wa kinga pamoja na magonjwa ya kuambukiza kutoka hospitali za Apollo; New Delhi
anawaasa watanzania kuepuka maambukizi mapya ya UKIMWI, kuepuka
kunyanyapa waathirika wa UKIMWI katika familia na jamii zetu na
ikiwezekana kufuta kabisa vifo visababishwavyo na UKIMWI.
”UKIMWI
ni kitu ambacho kipo ndani ya uwezo wetu na tunaweza kupambana nacho
kwa urahisi zaidi ya mashambulizi ya kigaidi yanayofanywa kwa
kushtukizwa- “kufikia sifuri” katika maambukizi ya UKIMWI inawezekana
kabisa kama wote tukidhamiria. Alisisitiza Dk. Nalin Nag
Mtazamo
chanya katika maisha, ushirikiano kutoka katika familia na marafiki,
malalamishi ya ukandamizwaji kutoka kwenye jamii kwa wingi wa watu
wanaoishi na virusi vya UKIMWI ni tatizo la muda tu. Sheria kali
zinahitajika kulinda na kutunza utu wa wahanga wa janga hili. Aliongeza Dk. Nalin Nag.
Dk. Nalin Nag
anasisitiza kuwa wagonjwa UKIMWI wafanye vipimo vyote vya afya zao mara
kwa mara, vipimo vya damu maabara, ufanisi wa ini, figo, kifua na
tatizo la hepatitis B. magonjwa nyemelezi kama kifua kikuu, pneumonia na
mengineyo yanatakiwa kudhibitiwa muda wote kabla ya kuanza kutumia dawa
za ARV.
“mlo
sahihi, uongezaji wa kinga, mitindo ya maisha, na namna ya kupambana na
msongo wa mawazo ni vitu vinavyojumuisha mlolongo wa kuboresha maisha
bora kwa waathirika ambao kwa sasa wanatarajia kuongeza muda wa maisha
yao kwa matumizi sahihi ya ARV. Alisema.
Dk. Nalin Nag anaelimisha
jamii kuhusu umuhimu wa matumii ya dawa za ARV kwa waathirika wote wa
UKIMWI. Hii imebadilisha kabisa makali ya ugonjwa na kuongeza ujasiri
katika kutokomeza maambukizi mapya. Dawa tofauti za ARV zinapatikana na
zinatumika zikiwa na kinga za aina 4 tofauti kwa ajili ya kudhibiti
nguvu za virusi na kupunguza makali ya ugonjwa.
“katika mazingira mengine huwa virusi havionekani kwenye damu hadi mwishoni mwa miezi sita hadi mwaka” aliongeza Dk. Nalin Nag kutoka Hospitali za Apollo Indraprastha.
Katika
kitengo cha afya ugonjwa wa UKIMWI unabaki kuwa changamoto kubwa
ulimwenguni, hasa kwa wananchi wenye kipato cha chini au cha kati. Na
matokeo ya hivi karibuni kuhusu upatikanaji rahisi wa ARV, kumefanya
wagonjwa wa UKIMWI kuweza kuishi maish marefu zaidi yenye afya bora. Kwa
kuongezea, imedhibitishwa kuwa ARV inaepusha maambukizi endelevu ya
UKIMWI.
UKIMWI
umeendelea kuenea ulimwenguni, kwa mujibu wa taarifa za sasa za shirika
la umoja wa mataifa la kupambana na UKIMWI (UNAIDS) takwimu za mwaka
2012, inakadiriwa watu milioni 34 wanaishi na virusi vya UKIMWI zaidi ya
jinsi ilivyokuwa awali nah ii pia ni kutokana na matumizi ya dawa za
ARV. Nchi zilizopo chini ya jangwa la Sahara zimebaki kuwa nchi
zilizoathirika zaidi na janga hili la UKIMWI. Mwaka 2011, ilikadiriwa
kuwepo kwa maambukizi mapya milioni 1.8 kwa nchi hizo; asilimia 69 ya
watu wote wanaoishi na virusi vya UKIMWI wanapatikana katika nchi
zilizopo chini ya jangwa la Sahara barani Afrika (UNAIDS, 2012).
No comments:
Post a Comment