Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday 19 December 2015

WAZIRI UMMY MWALIMU AKABIDHIWA OFISI NA MTANGULIZI WAKE DK. SEIF


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Ummy Mwalimu akimsikiliza aliyekuwa Waziri wa iliyokuwa Wizara ya Afya na Usatawi wa Jamaii ya Serikali ya Awamu ya Nne Dkt. Seif Rashid wakati wa kukabidhiwa rasmi ofisi leo jijini Dar es salaam.



Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Ummy Mwalimu akipokea taarifa ya makabidhiano ya ofisi na aliyekuwa Waziri wa iliyokuwa Wizara ya Afya na Usatawi wa Jamaii ya Serikali ya Awamu ya Nne Dkt. Seif Rashid wakati wa kukabidhiwa rasmi ofisi leo jijini Dar es salaam.



Aliyekuwa Waziri wa iliyokuwa Wizara ya Afya na Usatawi wa Jamaii ya Serikali ya Awamu ya Nne Dkt. Seif Rashid (kushoto) akisalimiana na Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Dkt. Hamisi Kigwangala (kulia) leo jijini Dar es salaam.(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)




Na Eleuteri Mangi-MAELEZO
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Ummy Mwalimu amekabidhiwa rasmi ofisi na aliyekuwa Waziri wa iliyokuwa Wizara ya Afya na Usatawi wa Jamaii ya Serikali ya Awamu ya Nne Dkt. Seif Rashid leo jijini Dar es salaam.
Akipokea ofisi hiyo, Waziri Ummy alimshukuru Dkt. Seif kwa jitihada kubwa waliyofanya ya kupambana na magonjwa kwa wananchi na kufanikisha Tanzania kuwa miongoni mwa nchi duniani ambayo imetatua tatizo la ugonjwa wa polio na kuwa “polio free”.
Aidha, Waziri Ummy amemhakikishia Dkt Seif kuendelea kushirikiana naye pale msaada wake utakapohitajika kwa kuwa anauzoefu katika masuala ya afya ili kuwahudumia Watanzania na kupambana na adui wa taifa ambaye ni magonjwa.
Akikabidhi ofisi, Dkt Seif aliwapongeza Waziri Ummy Mwalimu na Naibu wake Dkt. Hamisi Kigwangalla kwa kupewa nyadhifa hizo na kuahidi kuwapa ushirikiano wake paleutakapohitajika.
Dhana ya “Hapa Kazi Tu” imechukua mkondo wake ambapo hadi sasa Mwaziri na Manaibu waziri wanatekeleza dhana hiyo kwa vitendo na siyo kukaa ofisini, kwa kwa juhudi hizo viongozi kwa kushirikiana na wananchi, Tanzania itafanikiwa kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025 ikiwa na watu wenye afya bora inayowaruhusu kufanyakazi kwa juhudi na maarifa ili kuwa maendeleo yenye tija kwa Wtanzania.
 

No comments:

Post a Comment