Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday 23 December 2015

UDHAIFU WA USIMAMIZI WA MIRADI MBALIMBALI NI CHANGAMOTO KATIKA KULETA KASI YA MAENDELEO NDANI YA JAMII

  Viongozi wa mitandao ya wilaya za Bukombe na Mbogwe mkoani Geita wakiwa katika kikao cha pamoja kilichofanyika katika kata ya Masumbwe hivi karibuni 


 
“Ni vigumu kuamini kama mpango huu umekuwa mkubwa kiasi hiki. Tulianza watu 12 tu miaka mitano iliyopita, lakini leo tupo waraghbishi zaidi ya 400. Kwa hakika haya ni mafuriko ya waraghbishi, kwani sasa kila sehemu wanapatikana,” alisema Ndugulile.
Baada ya kikao hicho, yalifuata mafunzo maalumu ya uraghbishi kwa siku tatu yakiendeshwa kila wilaya. Mafunzo hayo yalilenga kufundisha namna ya kutafuta na kupata taarifa na kutambua changamoto zinazoikabili jamii na njia za kuzitatua.
“Nilikwenda ofisi zetu za halmashauri kuulizia vyanzo vya mapato vya wilaya na kuelezwa kuwa Mgodi wa Mwadui hauchangii chochote pamoja na kuwa upo katika eneo hilo. Taarifa hii niliwashirikisha na wenzangu pia.”
Hayo ni maneno ya mraghbishi Fredina Said kutoka kijiji cha Negezi, wilayani Kishapu mkoani Shinyanga. 
Pamoja na kwamba hakuweza kulifikisha mbali suala hilo, angalau aliweza kufahamu kilichokuwa kikiendelea Pamoja na mambo hayo, walifundishwa pia namna ya kujiamini kupitia mafunzo ya uraghbishi waliyokuwa wakiyapata kwa mara ya kwanza.
Mafunzo haya yalitolewa kwa nadharia na vitendo ambapo waraghbishi baada ya kupatiwa mafunzo ya darasani walipewa kazi ya kutembelea ofisi za halmashauri za wilaya zao.  Lengo ni moja tu, kuwajengea uwezo wa kuongea na viongozi wa kitaifa kama mkuu wa wilaya au mkurugenzi baada ya awali kuonyesha hofu na kutojiamini. 
“Ilikuwa mara ya kwanza kuonana na mkuu wa wilaya na kumuulizia masuala ya pembejeo za kilimo. Nilikuwa na hofu, hata hivyo kinyume na matarajio yangu, maswali yote aliyajibu ingawa siyo kwa kiwango nilichotarajia,” alisema mraghbishi Fedson Yaida wa Kijiji cha Shenda, wilaya Mbogwe, mkoani Geita Matokeo ya kutembelea ofisi hizo yalionekana pale walipopatiwa majibu ya maswali yao. 

Kazi hii ilikuwa na umuhimu mkubwa katika kuwandaa waraghbishi na majukumu makubwa ya uraghbishi. 
Waraghbishi hawa walikuwa wakiwakilisha wananchi wa vijiji vyao, hivyo moja ya jukumu lao ilikuwa ni kuwashirikisha walichojifunza.  Jukumu hilo walilifanya vizuri na waliweza kutambuliwa kwa urahisi na viongozi wa vijiji pamoja na wananchi wenzao. 
Na kwa sababu walipatiwa mafunzo kupitia mradi wa Chukua Hatua, walijikuta wakiitwa kwa jina hilo hilo la Chukua Hatua. Mfano mzuri ni waraghbishi waliopo katika kijiji cha Mwime, wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Hali hii ilisababisha wananchi wengi katika vijiji ambavyo mradi wa Chukua Hatua unaendeshwa kujitambulisha kama waraghbishi na kutaka na wao wapatiwe mafunzo. 
Na hapo ndipo lilipokuja wazo la kuwawezesha waraghbishi wa zamani na wapya kufanya kazi kwa pamojaAkielezea jinsi alivyowafundisha waraghbishi jinsi ya kufanya uraghbishi katika kijiji chake na vile vya jirani, mraghbishi kutoka Kijiji cha Ololosokwani, Kootu Tome, alisema: “Nimefundisha waraghbishi wa kijiji cha jirani. Niliwaeleza maana ya uraghbishi, kwamba hawatakiwi kujionyesha wazi kwa kila jambo, badala yake wanawashawishi watu kuchukua hatua katika kile anachokuwa amewafafanulia,” 
Mraghbishi mwingine ni Julius Katende kutoka Kijiji cha Ngarwa, wilayani Ngorongongo aliwafundisha waraghbishi wapya tofauti ya uraghbishi na uhamasishaji. 
Mraghbishi si mwamasishaji, bali ni mtu anayeibua hoja katika jamii na kuzitafutia majibu kwa kushirikiana na wenzake. 
Jumla ya waraghbishi wapya 762 wamefundishwa na waraghbishi 322 wa zamani, ikiwa ni ongezeko mara mbili katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia mwezi Julai hadi Septemba na kufanya idadi yao kuwa 1,084. 
Kati yao, wanawake ni zaidi ya 400. Hili ni ongozeko kubwa ambalo ni wazi linatokana na juhudi za pamoja. 
“Tuliwafundisha kutoka katika maeneo mbalimbali ambayo wamekuwa na kawaida ya kukusanyika,” haya ni maneno ya mkurugenzi wa Tamasha, Richard Mabala, wakati akifafanua namna wanavyoendesha mafunzo hayo katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Waraghbishi kwa upande mmoja wanawakilisha wananchi wa maeneo yao na wamekuwa mstari wa mbele kusimamia rasilimali zao na kuhakikisha huduma bora za jamii zinapatikana. 
Lakini ili kufanikisha, malengo ya mpango wa Chukua Hatua, viongozi wa vijiji, hasa wenyeviti, watendaji wa kata na vijiji wanafundishwa uraghbishi pia kulingana na nafasi zao.Jukumu la kuwafundisha viongozi hawa kwa upande wa mikoa ya kanda ya ziwa wamepewa CABUIPA, shirika mdau la mpango wa Chukua Hatua lilipo Kahama. 
Akifafanua wanachofanya, mkurugenzi wa shirika hilo, David Rwegoshora alisema:“Katika kipindi cha miezi mitatu tumefundisha wenyeviti 167 na watendaji 33 ngazi ya kata. Kati yao, wanawake walikuwa sita.”
 Kwa upande wa Ngorongoro, wenyeviti 14, watendaji 14 wa vijiji na 6 wa kata walipatiwa mafunzo hayo. Kundi lingine ni Sungusungu, ambapo hadi sasa idadi yao ni 15 nao walipewa mafunzo hayo ya uraghbishi. 
Wote hawa ni waraghbishi kwa nafasi zao. Katika awamu iliyopita ilijumuisha na viongozi wa dini wakiwamo masheikh, maimamu, wachungaji na makatekista.
Katika kuhakikisha waraghbishi wanawafikia watu wengi zaidi na kuwafundisha uraghbishi, mitandao ya waraghbishi imeanzishwa katika wilaya za Mbogwe, Kahama, Maswa, Kishapu, Bariadi, Shinyanga Vijijini, Itilima na Bukombe. 
Mitandao hii ilianza rasmi mwaka 2014 na kuwaleta pamoja waraghbishi wa mikoa ya Geita, Simiyu na Shinyanga.   
Hadi sasa, kuna wenyeviti pamoja na wasaidizi wao, ambao idadi yao imefikia 32, wanawake 16, sawa na asilimia 50. Wingi huu wa waraghbishi hauangalii itikadi za vyama, badala yake unaangalia kilicho bora kwa wanajamii kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment