Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Saturday 19 December 2015

WATUMISHI WAASWA KUWAHI KAZINI KUWATUMIKIA WATANZANIA

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Dkt. Hamisi Kigwangalla akifuatilia geti kungwa saa 1:30 asubuhi ambao ndiyo muda wa mwisho wa watumishi kufika kazini ili kusimamia suala la nidhamu ya kujali muda wa kuwahi kazini kwa watumishi wa wizara hiyo jana jijini Dar es salaam.


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa amekwisha amuru geti kungwa mara baada ya saa 1:30 asubuhi ambao ndiyo muda wa mwisho wa watumishi kufika kazini ili kusimamia suala la nidhamu ya kujali muda wa kuwahi kazini kwa watumishi wa wizara hiyo jana jijini Dar es salaam.


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Dkt. Hamisi Kigwangalla akisaini moja ya vitabu vya mahudhurio ya wafanyakazi katika Wizara hiyo mara baada ya saa 1:30 asubuhi ambao ndiyo muda wa mwisho wa watumishi kufika kazini ili kusimamia suala la nidhamu ya kujali muda wa kuwahi kazini kwa watumishi wa wizara hiyo jana jijini Dar es salaam.


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Dkt. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akiongea na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu Bw. Michael John (kulia) kujua utaratibu mzima wa watumishi kufika kazini ambapo Naibu Waziri huyo amefuatilia kwa wiki nzima na kubaini kuwepo uchelewaji kazini mara baada ya kuamuru geti kungwa mara baada ya saa 1:30 asubuhi ambao ndiyo muda wa mwisho wa watumishi kufika kazini ili kusimamia suala la nidhamu ya kujali muda wa kuwahi kazini kwa watumishi wa wizara hiyo jana jijini Dar es salaam.




Moja ya Daftari ya mahudhurio ya wafanyakazi ambayo imesainiwa tayari na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Dkt. Hamisi Kigwangalla jana jijini Dar es salaam.




Na Eleuteri Mangi- MAELEZO
Wafanyakazi Wizara wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee wametakiwa kuzingatia suala la muda wa kufanyakazi kuanzia kuingia kazini hadi muda wa kutoka baada ya muda uliopangwa.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Dkt. Hamisi Kigwangalla alipokuwa akifuatilia suala la nidhamu ya kujali muda wa kuwahi kazini kwa watumishi wa wizara hiyo jana jijini Dar es salaam.
“Wafanyakazi wanawajibu wa kuwahi kazini saa 1:30 asubuhi kama ilivyopangwa kwa mujibu wa taratibu za utumishi wa umma na kutoka saa 9:30 baada ya muda wa kazi, hatuwezi kuendelea kuvumilia tabia ya watu kuendelea kumwibia mwajiri muda wa kufanyakazi”,
“Sisi tumewahi kazini, Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na viongozi wengine, halafu watumishi wanachelewa, tumeonesha mfano, tunawahi na tunachelewa kuondoka” akisema Dkt. Kigwangalla.
Kwa mujibu wa taratibu za kazi, ilipofika saa 1:30 asubuhi, Dkt. Kigwangalla aliamuru walinzi kufunga geti na kutoruhusu waliyechelewa kuingia hadi atakapo maliza kusaini madaftari ya mahudhurio kulingana na idara na vitengo vilivyopo waizarani hapo.
Idara hizo ni pamoja na Utawala, Kinga, Mafunzo, Tiba, Udhibiti na Uhakiki Ubora, Mganga Mkuu, Uhasibu, Sera na Mipango, Wauguzi na Famasia pamoja na vitengo vya Sheria, Mawasilano Serikalini na Tehama.
Akisisitiza Dkt. Kigwangalla alisema kuwa wanachokifanya ni kuahakikisha zoezi la kukomesha tabia ya uchelewaji linakuwa endelevu kwasababu watumishi wameajiriwa ili kuwahudumia wananchi, ufuatiliaji huo utakomesha tabia ya watumishi kuchelewa kufika kazini na kuondoka mapema kabla ya muda wakazi.
Vilevile Dkt. Kigwangalla alisema kuwa watumishi wafanye kazi kwa kujitolea, maana Tanzania itajengwa na zama za kazi ambapo wao viongozi wamewapa watumishi mfano wa kuwahi kazini.
Kuhusu watumishi waliochelewa Dkt. Kigwangalla ameagiza waandike barua za kujieleza ni kwake na azipate jana hiyo hiyo ambapo zoezi hilo la amemkabidhi Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Bw. Michael John.
Aidha, katika kudhibiti tabia ya uchelewaji, Dkt. Kigwangalla amemwagiza Bw. Michael ammueleze kwa maadishi ni kwanini Wizara hiyo haijachukua hatua ya kuingia katika mfumo wa dijiti (Biometric) wa watumishi kuweka vidole au kutumia kadi wakati wa kuingia kazini ili mfumo mzima wa ofisi ujue mtumishi fulani amefika kazini saa ngapi na kama atatoka ajulikane yupo wapi na kwa nini.
Dkt. Kigwangalla amesema kuwa amefikia hatua hiyo ya kusimamia kukomesha tabia ya uchelewaji kutokana na Wizara hiyo kulaumiwa kwa na urasimu, kumbe watumishi hawawahi kazini ambapo yeye mwenyewe amejionea nia watu wangapi wameahi kazini.
Zaidi ya hayo, Dkt. Kigwangalla ameagiza kupewa maelezo ya kina juu ya watumishi wa afya nchi nzima kuanzia Madaktari, Wauguzi, Wafamasia ili aweze kujua kuna mfumo gani wa kuangalia watumishi wamefika ofisini na wanafanya kazi ipasavyo.

No comments:

Post a Comment