Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) Kagyabukama Kiliba (aliyevaa miwani) akishuhudia Majuto Alli Majuto
akiendelea na kazi yake ya kukaanga samaki aina ya pweza katika soko la samaki
la Feri jijini Dar es salaam.
Vijana wakiendelea kazi ya kukaanga samaki katika soko la Feri katika mazingira
ambayo hali ya usafi siyo ya kuridhisha kwa ajili ya kulinda afya ya mlaji.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya
Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Kagyabukama Kiliba
(wa tatu kutoka kushoto) akiwa na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Dar es salaam
na Halmashauri ya Wilaya ya Ilala wakiwasili eneo la soko la Feri jijini Dar es
salaa kujionea hali ya usafi wa soko hilo.
Baadhi ya wahudumu
wakiendelea na usafi eneo la soko la Feri jijini Dar es salaa huku Naibu Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Kagyabukama
Kiliba na msafara wake wakikagua na kujionea hali ya usafi wa soko hilo.
Kijana Hamisi Misango
akimnyanyua samaki aina ya taa ili amuandae tayari kwa kumuuza kwa wateja
wanafuata kitoweo katika soko la samaki la Feri jijini Dar es salaam.
Msafara wa Naibu Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Kagyabukama Kiliba wakishuhudia moja ya shimo la maji mchafu ambayo yanaweza
kuhatarisha usalama wa afya ya wananchi wanaofika katika soko la samaki la Feri
jijini Dar es salaam au wale watakaotumia samaki hao kama hawatakuwa wameandaliwa
katika hali ya usafi na salama. Lengo ni wananchi wengi wanaofika sokoni hapo
ni kununua samaki waweze kuwauzia watu wasoweza kufika sokoni hapo na wengine
kwa ajili ya matumizi yao ya nyumbani.
Mama lishe Zainabu Hamad
anayefanya shughuli zake za kutoa huduma ya chakula katika soko la Feri zoni 4
kizimba namba 12 akiongea na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Kagyabukama Kiliba alipotembelea sokoni
hapo kwa lengo la kuhamasisha suala la usafi kwa manufaa ya kulinda afya ya
wananchi wanatumia huduma hiyo wakiwa sokoni humo.
Biashara mbalimbali ikiwemo
ya kijana aliyekuwa akiuza mayai zikiendelea katika eneo la soko la Feri jijini
Dar es salaam bila ya kuzingatia kanuni za afya na hatari iliyopo ya magonjwa
wa mlipuko ikiwemo kipindupindu.
Mfanyabiashara wa Soko la Kariakoo
Mwajabu Mdeme akimueleza Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Kagyabukama Kiliba kero zinazowasumbua
sokoni hapo ikiwemo huduma mbovu ya maji, maji machafu kutapakaa sehemu
mbalimbali, huduma duni ya choo na joto kali eneo la Shimoni.
Baadhi ya maeneo
yaliyokithiri kwa uchafu katika soko la Kariakoo.
Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) Kagyabukama Kiliba na msafara wake wakiwa katika eneo la soko la
Kariakaoo kukagua suala la usafi unavyozingatiwa sokoni humo. Licha ya uchafu
uliopo katika soko la Kariakoo, wafanyabiashara wa matunda hawachukui tahadhari
yeyote ya kulinda afya za walaji wa matunda ambapo wanauza matunda aina ya
mananasi bila kuyafunika sa kusababisha inzi kuyazonga zonga matunda hayo kitu
ambacho ni hatari kwa suala la usalama wa afya ya malaji.
Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) Kagyabukama Kiliba akijionea wafanyabiashara wadogo walivyovamia
miundombinu ya Mradi wa Mabasi yaendayo kwa kasi katika eneo la Kariakoo jijini
Dar es salaam huku mafundi wakiendelea na kazi ya kupaka rangi.
Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI) Kagyabukama Kiliba akitembelea maeneo mbalimbali ya soko la Kariakoo
jijini Dar esa salaam.
(Picha
na Eleuteri Mangi-MAELEZO)
No comments:
Post a Comment