Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday 11 December 2015

MKUU WA WILAYA YA ARUSHA ASISITIZA MSHIKAMANO KUWALETEA WANANCHI MAENDELEO

   Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Fadhil Nkurlu akifungua rasmi Baraza la Madiwani wa Jiji la Arusha.

 Mwenyekiti wa muda wa Mkutano wa Baraza Ndg. Daniel Machunda ambaye pia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha  akikabidhi madaraka hayo  kwa Mstahiki Meya mara baada ya kuchaguliwa kwa kura 33 kati ya kura 34 zilizopigwa.

Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Ndg. Juma Iddi ambaye pia ni Katibu wa Mkutano wa Baraza akitoa muongozo wa namna Mkutano huu wa kwanza unavyoendeshwa kwa mujibu wa kanuni,kushoto ni Katibu Tawala mkoa wa Arusha,Addoh Mapunda.

Diwani wa Kata ya Sokon I, Mheshimiwa Calist Lazaro Bukhai(Chadema) akikishukuru baada ya kuchaguliwa kuwa Meya wa Jiji la Arusha. 

 Mstahiki    Meya wa Jiji la Arusha ,Mhe Calist Lazaro Bukhai akiwa na Naibu Meya wake  Viola Lazaro Likindikoki kwenye Mkutano wa kwanza wa Baraza la Madiwani 

Diwani wa Kata ya Kaloleni Mhe Lewis Kessy (Kushoto)  na Diwani wa Kata ya Levolosi Mhe. Efatha Nanyaro wakiwa kwenye Kikao cha kwanza cha Baraza la madiwani wa Jiji la Arusha

  Mhe. Abdulrasul Tojo (kulia) ambaye ni diwani pekee wa CCM kwenye  Baraza la Halmashauri ya Jiji la Arusha alipokua akiomba kura katika nafasi ya  Naibu Meya wa Jiji hilo.



Mstahiki Meya Mhe. Calist Bukhai (aliyevaa Taji) Naibu Meya Mhe. Viola Likindikoki (tatu kushoto) Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Fadhil Nkurlu (nne kulia), Mkurugenzi wa Jiji, Ndgugu Juma Iddi (tatu kulia) pamoja na Madiwani wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya Kikao cha Baraza la Madiwani.

No comments:

Post a Comment