Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Wednesday, 24 September 2014

SERIKALI YAWATAKA WASIMAMIZI NA WADADISI WA UTAFITI WA TATHMINI YA HUDUMA ZA AFYA KUZINGATIA WELEDI

Picha na 1
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid akifungua mafunzo ya siku 27 kwa wakufunzi na wadadisi  kutoka  Tanzania Bara na Zanzibar  watakaoendesha  Utafiti wa Tathmini ya utoaji wa Huduma za Afya nchini 2014/15 leo mkoani Kilimanjaro.
Picha na 2Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akizungumza na washiriki wa mafunzo ya Utafiti wa Tathmini ya utoaji wa Huduma za Afya nchini  leo mkoani Kilimanjaro.
Picha na 3Mkufunzi wa mafunzo ya wasimamizi na wadadisi wa Utafiti wa Tathmini ya Utoaji wa Huduma za Afya nchini Bi. Saumu Said akiendelea kutoa mafunzo kwa washiriki wa utafiti huo mkoani Kilimanjaro leo.
Picha na 4
Picha na 5Washiriki wa mafunzo ya Wasimamizi na wadadisi wa Utafiti wa Tathmini ya Utoaji wa Huduma za Afya nchini wakiendelea na mafunzo  yatakayowawezesha kufanya utafiti huo mkoani Kilimanjaro leo.
 Picha na 6
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid akisalimiana na wakufunzi na wadadisi  kutoka  Tanzania Bara na Zanzibar  watakaoendesha  Utafiti wa Tathmini ya utoaji wa Huduma za Afya nchini 2014/15 walio kwenye mafunzo leo mkoani Kilimanjaro.
Picha na 7
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid akiwa katika picha ya pamoja na wakufunzi na wadadisi  kutoka  Tanzania Bara na Zanzibar  watakaoendesha  Utafiti wa Tathmini ya utoaji wa Huduma za Afya nchini 2014/15 leo mkoani Kilimanjaro.
 
Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro
Aidha, imewaagiza Waganga Wakuu wa MikoaWilaya,madakatari na wafanyakazi wa vituo vyote vya kutolea hudumaza afya nchini  kutoa ushirikiano kwawadadisiwatakaoendesha utafiti huo ili waweze kufika kwenye vituo vya kutolea huduma za afya vilivyopo katika maeneo yaokwa lengo lakupata taarifa sahihi zitakazofanikisha utafiti huomuhimu kwa maendeleo ya taifa.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid akizungumza wakati akifungua mafunzo ya siku 27 kwa wakufunzi na wadadisi  kutoka  Tanzania Bara na Zanzibar  watakaoendesha  utafiti huo  amesema kuwa wakufunzi, wadadisi na wataalam  hao wanayo nafasi kubwa ya kufanikisha upatikanaji wa takwimu sahihi zitakazotoa taswira halisi ya utoaji wa huduma ya afya nchini kwa mwaka 2014/2015.
Amesema utafiti huo utaiwezesha serikali kutathmini utekelezaji wa mipango mbalimbali na kufikia malengo iliyojiwekea kitaifa na kimataifa kwa kuboresha na kuendelea kutoa huduma bora za afya kwa wananchi wake.
Amesema Serikali imekuwa ikitekeleza programu mbalimbali za kuboresha huduma za afya na maisha ya Watanzania kwa kupitia Mikakati ya Kimataifa na Kitaifa ikiwemo ile ya Malengo ya Milenia ya Mwaka 2015 na Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011 -2016).
Dkt. Seif amesema katika juhudi hizo Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imekuwa na jukumu la kusimamia programu mbalimbali za afya na kufuatilia utekelezaji na utoaji wa huduma za afya nchini.
Amesema kumekuwa na maboresho makubwa katika sekta ya afya hadi kufikia mwaka 2013 ambapo takwimu zinaonyesha kuwepo kwa  vituo  6767 vya kutolea huduma ya afya nchini , hospitali 256, vituo vya afya 701 na zahanati 5810.
Nyote ni mashahidi kuwa toka kipindi hicho mpaka sasa serikali imeendelea kusogeza huduma za afya karibu na wananchi wake,sasa tuna huduma ya kuzuia maambukizi ya UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto ambayo inapatikana  katika vituo vyote vinavyotoa huduma za mama mjamzito” Amesisitiza.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akizungumzia mafunzo hayo amesema kuwa washiriki watakaofaulu na kukidhi vigezo vilivyowekwa  watashiriki katika zoezi la kukusanya takwimu za utafiti huo  kwa kipindi cha miezi minnekuanzia  tarehe 13 Oktoba 2014 .
Amesema utekelezaji wa utafiti huona mafunzo hayounafanywa kwa pamoja na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii – Tanzania Bara, Wizara Afya – Zanzibar, Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, na Shirika la ICF International la Marekani ambao pia wanatoa ushauri wa kitaalamu katika kufanikisha utafiti huo.
 Dkt. Chuwa amefafanua kuwa utafiti huo utahusisha ukusanyaji wa takwimu katika sehemu za kutolea huduma za afya kwa lengo la  kufahamu utayari wa vituo vinavyotoa huduma za afya na huduma bora za afya kwa wananchi.
 Aidha amezitaja huduma zitakazoguswa na utafiti huo kuwa ni pamoja pamoja na Huduma za Afya ya Uzazi, Afya ya Watoto, Maradhi ya Kuambukiza kama vile Kifua Kikuu, UKIMWI, Malaria pamoja na Maradhi yasiyo ya kuambukizakama vile magonjwa ya Kisukari na Moyo.
  Amefafanua kuwa lengo la kufanyika kwa utafiti huo ni kuiwezesha serikali kujua ni kwa namna gani vituo vinavyotoa huduma ya afya vimejipanga kutoa huduma bora ya afya kwa kuangalia upatikanaji wa huduma mbalimbali, vifaa, dawa, miundombinu na rasilimali watu kwa kada mbalimbali.
Naye mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt. Ibrahimu Msengi akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo amesema kuwa mkoa huo unaendelea na juhudi za kuboresha huduma  za afya zinazotolewa katika vituo vya  afya pamoja  kwa lengo la kuboresha hali ya maisha ya wakazi wa Kilimanjaro na kukuza pato la mkoa huo.
Amesema mkoa umeweka kipaumbele katika kuboresha miundombinu ya afya iliyopo ili iweze kuakisi ukuaji wa Pato la Mkoa na mahitaji ya wananchi katika kupata huduma za afya zilizo bora kulingana na ongezeko la idadi ya Watu.
Amefafanua kuwa utafiti huo umekuja wakati muafaka ambapo mkoa huo na mikoa mingine nchini inahitaji kuboresha huduma za afya katika vituo vyotevya kutolea huduma.

No comments:

Post a Comment