'Niliambiwa kuwa mimi ni mfano mbaya' anasema Karla Valentine.
Nina umri wa miaka 35 na nina Tatoo nyingi tu.
Nikuwa nafanya kazi katika shule kama msaidizi.
Niliulizwa kwa nini nilikuwa na michoro mingi au
Tatoo kwenye mwili wangu pamoja na kuhojiwa kwa nini nimejitoga sana usoni mwangu.
Tatoo zangu nilikuwa nazificha sana msimu wa baridi lakini msimu wa joto ulipoingia ikawa zinaonekana sana.
Mara tu maofisa wa shule wakaanza kunipa masharti kuhusu mavazi ninayopaswa kuvaa nikiwa kazini. Masharti hayo yalisema tatoo na kujitoga usoni havikubaliki kwani ni mfano mbaya sana kwa wanafunzi na hivyo nikatakiwa kujifunika kila wakati.
Hili lilikuwa onyo la kwanza kwangu kupata nikiwa kazini.
Niliifanya kazi yangu vyema, na watoto walinipenda sana na hata kupenda kuzungumzia Tatoo zangu.
Nilijaribu kuanzisha kampeni ya kupinga ubaguzi huu lakini sikutaka kufanya kazi katika mazingira ambapo nilibaguliwa kwa kuwa na Tatoo na pia kwa kuwa nimejitoga, sipaswi kuifanya kazi hiyo.
Baada ya wiki moja nilikutana na mkuu wa shule na nikamjulisha kwamba naacha kazi.
Mkuu wa shule alitaka kukutana nami kuhusu maswala kadhaa lakini sikuhisi vyema kufanya kazi katika eneo ambalo watu wanabaguliwa kwa sababu ya kujitoga usoni na kujichora Tatoo.
Sidhani nina muda wa kujipigania kusisitiza kwamba mimi ni mfanyakazi mzuri na mtu mwenye heshima zake.
Inasikitisha sana kwamba mwaka huu wa 2014 watu wanabaguliwa kutokana na wanachokichagua kufanyia mwili wao.
Nina huzuni kuwa watoto wanakuwa wakifunzwa msimamo kama hii.
'Niliambiwa nifunike tatoo zangu,' anasema Sam wa Brisbane, Australia.
Nina shati la mikono mirefu na mwajiri wangu wa hapo nyuma aliniambia lazima nizifunike nyakati za kazi. Sikufurahia hata kidogo kwa sababu wafanyakazi wengine waliruhisiwa kuvalia herini ambazo pia ni mapambo ya mwili.
Kwa sasa nafanya kazi na kampuni ambayo haibagui watu walio na michoro ya tatoo. Mimi ni meneja wa mikataba katika hospitali. Kazi yangu ya hapo awali, nilikuwa afisaa msimamizi wa mipango ambako sera ya kazi ilisema kuwa watu wenye tatoo lazima wazifunike nyakati zote.
CREDIT: BBC
No comments:
Post a Comment