Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Thursday, 25 September 2014

CAG ASEMA, KIGOGO KASHFA YA EPA ALITENGA RUSHWA WA SHS. 30 BILIONI

CAG mstaafu, Ludovick Utouh

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) aliyestaafu Ijumaa iliyopita, Ludovick Utouh, amefichua kuwa mmoja wa watu waliohusika katika kashfa ya wizi wa fedha za Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) alitenga rushwa ya Sh. bilioni 30 kwa nia ya kuipata ripoti ya ofisi yake kwenda serikalini.

Akizungumza katika mahojiano maalum na NIPASHE yaliyofanyika kwenye ofisi yake jijini Dar es Salaam siku moja kabla ya kustaafu rasmi, Utouh alisema kuwa kwa bahati alipata taarifa za kuwapo kwa mpango wa kuwapo kwa kiasi hicho kikubwa cha fedha kilichotengwa kwa mtu yeyote atakayefanikisha jaribio la kuifikisha ripoti ya CAG kwa kigogo huyo wa EPA kabla ya kwenda serikalini na kumfikia Rais Kikwete, hivyo yeye akajikuta akiwa na hofu kubwa.



"Nilipata ripoti wakati wa EPA kwamba kuna mtu aliyekuwa ame-set aside (ametenga) bilioni 30 kwa mtu yeyote ambaye angempatia ripoti yangu mimi kabla haijaenda serikalini. Nilipata hiyo ripoti... sasa unapopata ripoti kama hiyo... unakuwa na wasiwasi," alisema Utouh.

Akieleza zaidi, Utouh alisema kuwa kutokana na uwapo wa tishio hilo, alilazimika kuchukua tahadhari ya ziada na kwamba kuna wakati alikuwa akijifungia ofisini muda wote kwa nia ya kujiweka salama na kwamba hata alipokuwa barabarani, muda wote alikuwa katika tahadhari kubwa.

"Mimi nilikuwa najifungia hapa ofisini kabisa kwa sababu, unajua na-make sure (nahakikisha) milango yote imefungwa. Ukitembea, ukiona gari inakuja, unamwambia dereva aangalie. Ilikuwa tension kali sana. Yaah... ni tension kali sana," alisema Utouh.

CAG huyo mstaafu alifichua ukweli huo baada ya kuulizwa ni wakati gani hasa ambao aliwahi kuishi kwenye mazingira magumu ya kiutendaji katika miaka yake minane ya kuwa na madaraka ya CAG.

"Ukweli ni wakati wa ukaguzi wa EPA... ilikuwa inasemwa sana kwenye vyombo vya habari. Ikaandikwa sana. Halafu kukawa na hisia.

Watu wanazungumza, hii ni ya fulani, sijui ya fulani, sijui ilifanyaje... sasa kwa hiyo unapokuwa katika hali ya aina hiyo... mhh - mhh - heh! Hujui sasa anayekuandama. Hujui anayekutafuta," alisema Utouh.

Sakat la EPA lilihusisha wizi wa takriban Sh. bilioni 133 katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje iliyokuwa katika Benki Kuu ya Tanzania.

Watu kadhaa wameshafikishwa mahakamani kutokana na kashfa hiyo, wengine wakifungwa na kiasi cha zaidi ya Sh. bilioni 60 kikirejeshwa na watu waliokwapua fedha hizo na kutumiwa na serikali kusaidia sekta ya kilimo kupitia dirisha maalum lililofunguliwa kwenye benki ya TIB.

 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment