Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Monday, 22 September 2014

DODOMA! DODOMA! MACHO NA MASIKIO YOTE DODOMA KUSIKILIZA RASIMU YA TATU YA KATIBA!


Macho na masikio ya Watanzania wote yameelekezwa Dodoma kusikiliza Rasimu ya Tatu ya Katiba Mpya wakati inapowasilishwa mbele ya Bunge Maalumu la Katiba.
Rasimu hiyo ilikabidhiwa jana na Kamati ya Uandishi kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Bunge hilo, Samuel Sitta, ambaye pia
ndiye Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba.
Tangu Jumanne iliyopita, Kamati ya Uandishi chini ya Mwenyekiti Andrew Chenge na Mgeni Hassan Juma na sekretarieti yake, ilikuwa na jukumu la kuandika rasimu hiyo ambayo ilikamilika Ijumaa.
Rasimu hiyo ya Tatu inatarajiwa kubeba sehemu kubwa ya maudhui ya Katiba inayopendekezwa, ambayo itapigiwa kura ya maoni na Watanzania baada ya Uchaguzi Mkuu ujao.
Kwa mujibu wa Ratiba hiyo, leo na kesho, wajumbe wa Bunge Maalumu watapata muda wa kuitafakari rasimu hiyo ya Katiba, kabla ya kurejea bungeni Jumatano na Alhamisi ijayo kuhakiki na kujadili ibara za rasimu hiyo.

Aidha, ratiba inaonyesha kwamba, Ijumaa Kamati ya Uandishi itarejea kibaruani kufanya marekebisho ya mwisho ya Ibara za Rasimu ya Mwisho ya Katiba kabla ya kuiwasilisha tena Bungeni Septemba 27, na Jumapili ya Septemba 28 kamati za Bunge Maalumu la Katiba, zitajielimisha kuhusu Rasimu ya Mwisho ya Katiba na taratibu za upigaji kura.
Kura ya kupata Katiba inayopendekezwa, kwa mujibu wa ratiba hiyo, inatarajiwa kuanza kupigwa kuanzia Jumatatu ya Septemba 29 mpaka Oktoba 2.
Wakati mchakato huo ukiwa katika hatua za mwisho, ule uoga wa kukosekana kwa theluthi mbili za kura kutoka Tanzania Bara za Zanzibar, uliosababishwa na kutokuwepo kwa baadhi ya wajumbe kutoka kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), umeanza kuondoka.
Tayari Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Asha Rose Migiro, ameshatoa tamko kuonesha kuwa wajumbe wa Ukawa, waliosusa wakitarajia kukwamisha kupatikana kwa Katiba inayopendekezwa, hawatakuwa na athari.
Kwa mujibu wa Dk Migiro, idadi ya wajumbe wote walikuwa 630, na Ukawa waliosusa ni 130 tu ambao ni sawa na asilimia 21 ya wajumbe wote.
Kwa maana hiyo wajumbe waliobaki ni 500, sawa na asilimia 79 ya wajumbe wote ambao ni zaidi ya theluthi mbili tayari. Dk Migiro aliweka wazi kuwa wajumbe wanaotoka Tanzania Bara ni 348 na kati yao, 125 wanatoka kundi la 201.
Kwa Zanzibar, takwimu hiyo inaonesha wapo wajumbe 152 ambao kati yao 64 wanatoka kundi la 201.

No comments:

Post a Comment