Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Tuesday, 23 September 2014

EBOLA BADO TISHIO NIGERIA


Jitihada zimeendelea kufanywa katika nchi kadhaa za Afrika magharibi na jumuia ya kimataifa kupambana na ugonjwa wa ebola ambao umeathiri nchi za Sierra Leone,Liberia , Guinea hali kadhalika Nigeria kwa kiasi kikubwa huku Serikali za nchi hizo zikifanya jitihada za kujinusuru na ugonjwa huo.
Baadhi ya shule nchini Nigeria zimefunguliwa baada ya kuchelewa kwa zaidi ya wiki mbili kwa lengo la kujaribu kuzuia maambukizi ya ugonjwa ebola lakini
shule zilizopo mjini lagos ambapo ndio kitovu cha ugonjwa huo zitaendelea kufungwa mpaka mwezi ujao .
Shirikisho la walimu nchini humo linaitaka serikali kuchukua hatua ili kuzuia tishio la maambukizi ya ugonjwa wa ebola kwa wanafunzi, na kusema kuwa wamesitisha mgomo
Wakati huo huo, Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kuwa maambukizi ya virusi vya ebola yamedhibitiwa nchini Nigeria na Senegal miongoni mwa nchi tano ambazo ugonjwa wa ebola umeua karibia watu 2800.
Raia wa Nchi jirani Sierra Leone walilazimika kujifungia ndani wa mda wa siku tatu kujinusuru na ebola zoezi ambalo viongozi wamesema kuwa limefanikiwa.
BBC/SWAHILI

No comments:

Post a Comment