Tamasha la kila mwaka la Serengeti Fiesta, limepagawisha
maelfu ya wakazi wa mji wa Morogoro na kuacha simulizi kubwa na ya aina yake katika mji huo.
Baadhi ya wasanii waliofunika vilivyo katika tamasha hilo na
kukonga nyoyo za mashabiki ni pamoja na Mr. Blue, Makomando, Ommy Dimpoz na
Stamina.
Stamina ambaye ni mzaliwa wa morogoro alimpandisha
mwanamuziki mwingine nguli katika miondoko ya muziki wa kizazi kipya Fid Q bila
kutarajia na kufanya mashabiki waliofurika uwanjani hapo kupagawa kwa furaha.
Shoo ilianza
taratibu na kadri muda ulivyokwenda ndivyo mashabiki walivyozidi kupagawa. Wasanii
hao walikonga nyoyo za mashabiki wao vilivyo na kufanya uwanja wa Jamhuri
Morogoro kugubikwa na shangwe kila wakati.
Stamina pia
alipanda jukwani na Ney wa Mitego kutumbuiza kwa pamoja kibao chao maarufu kwa
jina la “Huko kwenu vipi”. Mashabiki
walisikika wakiimba sambamba na msanii Stamina ambaye ni mzaliwa wa Morogoro.
“Si kila siku shoo
zinazofanyika katika viunga vya mji wa Morogoro hupagawisha na kuvuta hisia za watu
wengi kama ilivyokuwa wakati wa tamasha la Serengeti Fiesta ,” alisema mmoja wa
mashabiki.
Bonanza ya mpira
wa miguu na mashindano ya Super nyota Diva yalifanyika kusaka vipaji vya muziki
mbali mbali kutoka sehemu tofauti
ya mkoa wa Morogoro na washindi walipatikana ambao watasafiri kwenda Dar
es Salaam katika shoo ya mwisho.
Wasanii wengine
waliopanda katika jukwaa ni pamoja na Young
Killa, Weusi, Afande Sele, Vanessa, Linah, Madee, Mo Music, Baraka Da Prince, Y
tony na John Maker.
Primetime
Promotions walipata sifa kubwa na kuwa gumzo kwa wakazi wa mji wa Morogoro
usiku huo kufuatia utaratibu mzuri waliokuwa wameupanga katika kufanikisha
tamasha hilo.
Akizungumza
baada ya shoo, Brand Manager of Serengeti
Premium Lager, Rugambo Rodney, alisema…. “Hakika nawashukuru wakazi wa mji wa Morogoro kwa kujitokeza kwa
wingi na kuonyesha umoja katika tamasha la Serengeti Fiesta mwaka huu kwani waliweza
kushikamana na kusapoti wasanii . Mikoa inayofuatia baada ya hapa ni Mbeya, Mtwara
na Songea napenda kuwaambia wakazi wa miji hiyo kuwa wajiandae kujionea shoo
nyingine kali kama iliyochezwa hapa Morogoro, ikiletwa kwenu na SBL.
No comments:
Post a Comment