Twitter Buzz

....

....

...

...

IMETOSHA!

IMETOSHA!

Featured post

KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO

Makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandes De la Vega alishindwa kujizuia na kwenda kumtuza mtoto Gozbert ...

Friday, 26 September 2014

KINANA ASEMA, MIGOGORO YA ARDHI INASABABISHWA NA VIONGOZI

Katibu Mkuu wa CCM, Kanali mstaafu Abdulrahman Kinana

NA MARY GEOFREY
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, amesema migogoro inayojitokeza katika maeneo mbalimbali nchini kati ya wakulima na wafugaji, inasababishwa na viongozi.

Kinana alitoa kauli hiyo wilayani Kilindi, Tanga, alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Kibrashi.



Kinana alisema baadhi ya viongozi ndiyo chanzo cha migogoro hiyo kwani wamekuwa wakiuza maeneo kutoka katika moja ya makundi hayo na kuwauzia wengine katika kundi hilo hilo.

Alisema,  pia wamekuwa wachonganishi wakubwa na pale kunapotokea mapigano, wamekuwa wakijifanya hawajui kinachoendelea.

Aidha, aliitaka serikali kupanga matumizi bora ya ardhi ili kuondokana na  migogoro ya kugombea ardhi kati ya wakulima na wafugaji katika maeneo mbalimbali  wilayani humo.

 “Ipo haja ya kupanga maeneo ya ufugaji na kilimo ili kuondokana na mauaji yaliyokithiri katika maeneo yote nchini, hakuna mahali nilipopita sijakuta migogoro,” alisema Kinana.

Pia aliitaka baadhi ya mikoa ambayo amekuta migogoro kati ya wakulima na wafugaji ikiwamo Manyara, Morogoro, Geita na Singida kwamba lazima itafutwe namna ya kumaliza migogoro hiyo kwa kuhakikisha maeneo ya wakulima yanafahamika, na wafugaji yanafahamika.

Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Suleiman Liwowa, alisema changamoto kubwa iliyopo katika wilaya hiyo ni pamoja na migogoro iliyopo kati ya wakulima na wafugaji.

Liwowa alisema, Serikali inajitahidi kulipatia ufumbuzi suala hilo na kumuahidi Kinana kuwa atalishughulikia suala hilo kadri itakavyowezekana ili migogoro hiyo isijirudie na kwamba kama chanzo ni viongozi wanaouza ardhi atafuatilia kwa ukaribu na akibaini sheria itachukua mkondo wake.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment